Walimu nao wapewe Posho za mwezi kama maaskari

Habar zenu mabibi na mababu..

Mwalimu ni mtu anaesaidia wengine kupata ujuzi, maarifa na tunu. Mwalimu ndie anaezalisha Madaktari, manesi, bwana afya, wanasiasa, wafanyabiashara n.k, na wote mnaweza kukubaliana nami kuwa bila mwalimu huenda usingeweza kusoma, kuhesabu na kuandika.

Pamoja na uzito huo alonao mwalimu lakini hakuna watumishi wa serikali wenye hali mbaya ya kiuchumi kama walimu yaani mishahara ni midogo, mikopo kwenye mabenki, hakuna nyongeza ya mshahara, hakuna kupanda madaraja, hana cha kulipwa over time, hakuna cha pesa za semina kama zamani, hakuna ata kudunduliza kupata hela ya tuisheni yani ni shida tupu zimewajaa.

Mbaya zaidi kwenye sekta ya ualimu kila mtu ni bosi wako yani hata mwenyekiti wa mtaa anaweza kuja ofisini kwako na akakugombesha na hata kukutia makofi, ni sekta ambayo imeshushiwa heshima kwa kiasi kikubwa sn.

Leo hii ukimkuta mwalimu barabarani anaongea peke yake unaweza kusema amemeza notes kumbe ni msongo wa mawazo unampeleka puta Vibaya mno akifikiria ni miaka mitano sasa lakini bado mshahara ni ule ule hakuna ata senti ya nyongeza, hajapanda daraja, anachopokea mwisho wa mwezi ni laki mbili akikatwa mkopo alochukua benki, huku ukizingatia gharama za maisha zimepanda na familia imeongezeka.

Kiukweli ukipasua vifua vya walimu utakutana na masononeko makubwa mnoo, walimu wamechooka sana ule uvumilivu walokuwa wanasifiwa nao sasa haupo tena nao ni binadamu, walimu wameshachoka na kutothaminiwa maslahi yao ni ule uoga tu wa kutosema hadharani wakihofia kupoteza ata hako kibarua. Leo hii bora ya bwana afya anaweza pata posho ya kukagua nyama na akarudi na kilo ya nyama nyumbani, heri ya maaskari wenye posho kila mwezi, heri ya watumishi wengine wenye hadi marupurupu ya overtime.. Leo hii kwa shida anazonuka mwalimu tukitaka kuwavalisha kiatu hiki cha mwalimu watumishi wengine wa serikali basi lazima kiwabane tu.

Asilimia 100% walimu waliamini kuwa kupata Rais ambae ni mwalimu kungepelekea kuboreshewa maslahi yao na mazingira ya kazi kwani anayajua yote yaliyomo kwenye sekta ya ualimu lakini mambo yamekuwa tofauti kabisa mpaka walimu wanawaza ni nani sasa atakuja kuwa mtetezi wao kama sio mwalimu mwenzao.! Mara nyingi Mh Rais Magufuli amekuwa akinukuliwa akisema kuwa serikali yake haitawaacha walimu (maneno ambayo yamezoeleka masikioni mwa walimu mwaka wa 6 huu) tena anaenda mbali kwa kusema kuwa yeye ni mwalimu, mkewe ni mwalimu, waziri mkuu ni mwalimu, mkewe ni mwalimu, huku baraza lake la mawaziri likiwa limesheheni walimu mbalimbali, lakini yote haya haijawahi kamwe kuwa chachu ya kuthaminiwa maslahi ya walimu. Kiasi kwamba walimu sasa wanamkumbuka na kumlilia mh Kikwete kwa namna alivyokuwa akiwapandishia watumishi mishahara yao.

Mheshimiwa Rais Magufuli walimu wako wamekata tamaa na wamechoka na maneno yako ya matumaini yasiyozaa matunda kila siku kuwa serikali yako iko pamoja na walimu lakin wapi! kiasi kwamba wanafanya kazi ilimradi siku ziende tu lakini hawana motisha yoyote wanayoipata ili kufanya kazi kwa moyo wote. Tena walimu wako wanatamani muda wako wa kuongoza (kutawala) uishe ata kesho ili wabadilishe upepo angalau Raisi ajae anaweza kuwaona na kujali maslahi yao.

Mheshimiwa Rais John Magufuli ikikupendeza walimu nao wapate posho za kila mwezi kama maaskari ili iwe sehemu ya kuwapa motisha wachape kazi kisawasawa, na ni imani yangu walimu wakiwekewa utaratibu wa kupata posho walau laki mbili basi tutaingia katika Mapinduzi makubwa ya elimu mana walimu watafanya kazi kufa kupona na kutakuwa na ushindani na hari ya kufundisha. Mhe Raisi wahurumie Walimu wenzako wanashindwa kukwambia ukweli kwasababu wanakuogopa.

~Gai da Seboga (Mwalimu wa Kujitolea)
Askari yupo kazini 24hrs
Weekend yupo kazin
Sikukuu pasaka Eid, Christmass sijui muungano yupo kazini
Ana shift za kuingia kazin usiku.
Akihitajika kazin hata saa 8 usiku lazima awepo.
 
Askar hawez mfikia Mwalimu kwa mshahara Hilo Nina uhakika nalo kabisa .kinachomboost askar Ni ile posho ambayo kwenye mafao Haina madhara yoyote Yale .

So hapa kwa upande wa mafao mwalim lazima ampige gepu kubwa Sana askar ila nae askar anakuja mpiga gepu Mwalimu kwenye kaposho tu .

Take home ya askar anaeanza Kaz Ni around 350 wakat Mwalimu grade A 360,Diploma 450,bachelor 550 hizo Ni makadirio maana sijaweka visent .
Unajua askari mwenye bachelor analipwa kiasi gani?
Mwalimu inajulikana ni 700k+ na sio 550k unyosema
 
Mwalimu wa chet ndie analipwa 360 take home ila degree anayeanza Kaz Ni 716000 take home Ni laki tano na vitoto huko ,askar Hana mshahara wa kumzid Mwalimu hata yule wa chet tu wanaringana ,askar ana boostiwa na posho anayopata ambayo Ni around 300k lakin kwenye mafao askar hamgus mwalimu hata kidogo
Unafahaku askari wanakipwa mshahara kuoibgana na elimu yake? Askari wenye vyeo sawa na elimu tofauti mishahara yao ni tofauti pia.
Constable mwenye form 5 ana mshahara wake certificate ana wake au diploma mpaka bachelor ni tofauti
 
Habar zenu mabibi na mababu..

Mwalimu ni mtu anaesaidia wengine kupata ujuzi, maarifa na tunu. Mwalimu ndie anaezalisha Madaktari, manesi, bwana afya, wanasiasa, wafanyabiashara n.k, na wote mnaweza kukubaliana nami kuwa bila mwalimu huenda usingeweza kusoma, kuhesabu na kuandika.

Pamoja na uzito huo alonao mwalimu lakini hakuna watumishi wa serikali wenye hali mbaya ya kiuchumi kama walimu yaani mishahara ni midogo, mikopo kwenye mabenki, hakuna nyongeza ya mshahara, hakuna kupanda madaraja, hana cha kulipwa over time, hakuna cha pesa za semina kama zamani, hakuna ata kudunduliza kupata hela ya tuisheni yani ni shida tupu zimewajaa.

Mbaya zaidi kwenye sekta ya ualimu kila mtu ni bosi wako yani hata mwenyekiti wa mtaa anaweza kuja ofisini kwako na akakugombesha na hata kukutia makofi, ni sekta ambayo imeshushiwa heshima kwa kiasi kikubwa sn.

Leo hii ukimkuta mwalimu barabarani anaongea peke yake unaweza kusema amemeza notes kumbe ni msongo wa mawazo unampeleka puta Vibaya mno akifikiria ni miaka mitano sasa lakini bado mshahara ni ule ule hakuna ata senti ya nyongeza, hajapanda daraja, anachopokea mwisho wa mwezi ni laki mbili akikatwa mkopo alochukua benki, huku ukizingatia gharama za maisha zimepanda na familia imeongezeka.

Kiukweli ukipasua vifua vya walimu utakutana na masononeko makubwa mnoo, walimu wamechooka sana ule uvumilivu walokuwa wanasifiwa nao sasa haupo tena nao ni binadamu, walimu wameshachoka na kutothaminiwa maslahi yao ni ule uoga tu wa kutosema hadharani wakihofia kupoteza ata hako kibarua. Leo hii bora ya bwana afya anaweza pata posho ya kukagua nyama na akarudi na kilo ya nyama nyumbani, heri ya maaskari wenye posho kila mwezi, heri ya watumishi wengine wenye hadi marupurupu ya overtime.. Leo hii kwa shida anazonuka mwalimu tukitaka kuwavalisha kiatu hiki cha mwalimu watumishi wengine wa serikali basi lazima kiwabane tu.

Asilimia 100% walimu waliamini kuwa kupata Rais ambae ni mwalimu kungepelekea kuboreshewa maslahi yao na mazingira ya kazi kwani anayajua yote yaliyomo kwenye sekta ya ualimu lakini mambo yamekuwa tofauti kabisa mpaka walimu wanawaza ni nani sasa atakuja kuwa mtetezi wao kama sio mwalimu mwenzao.! Mara nyingi Mh Rais Magufuli amekuwa akinukuliwa akisema kuwa serikali yake haitawaacha walimu (maneno ambayo yamezoeleka masikioni mwa walimu mwaka wa 6 huu) tena anaenda mbali kwa kusema kuwa yeye ni mwalimu, mkewe ni mwalimu, waziri mkuu ni mwalimu, mkewe ni mwalimu, huku baraza lake la mawaziri likiwa limesheheni walimu mbalimbali, lakini yote haya haijawahi kamwe kuwa chachu ya kuthaminiwa maslahi ya walimu. Kiasi kwamba walimu sasa wanamkumbuka na kumlilia mh Kikwete kwa namna alivyokuwa akiwapandishia watumishi mishahara yao.

Mheshimiwa Rais Magufuli walimu wako wamekata tamaa na wamechoka na maneno yako ya matumaini yasiyozaa matunda kila siku kuwa serikali yako iko pamoja na walimu lakin wapi! kiasi kwamba wanafanya kazi ilimradi siku ziende tu lakini hawana motisha yoyote wanayoipata ili kufanya kazi kwa moyo wote. Tena walimu wako wanatamani muda wako wa kuongoza (kutawala) uishe ata kesho ili wabadilishe upepo angalau Raisi ajae anaweza kuwaona na kujali maslahi yao.

Mheshimiwa Rais John Magufuli ikikupendeza walimu nao wapate posho za kila mwezi kama maaskari ili iwe sehemu ya kuwapa motisha wachape kazi kisawasawa, na ni imani yangu walimu wakiwekewa utaratibu wa kupata posho walau laki mbili basi tutaingia katika Mapinduzi makubwa ya elimu mana walimu watafanya kazi kufa kupona na kutakuwa na ushindani na hari ya kufundisha. Mhe Raisi wahurumie Walimu wenzako wanashindwa kukwambia ukweli kwasababu wanakuogopa.

~Gai da Seboga (Mwalimu wa Kujitolea)

Ok wewe anzisha tu tuisheni uone utapata miposho hadi uyakatae
 
We Lofa Acha kuongopea watu!!! Hivi unaujua mshahara wa askar wwe!!!

Askari analipwa kutokana na Cheo alichonacho pamoja na Elimu yake!!

Kiufupi Askari mishahara imepishana ... Unaweza mkuta askari hana cheo ..lakin elimu yake anakula sawa na mweny nyota:

Uwezi linganisha mshahala wa Askari Form four ..coplo na Mwalimu senior mwenye Bachelor'
Nikikwita pimbi ntakuwa nimekosea? Badala ujib hoja uankuja na matus na hapa lengo Ni kufahamishana tu Sasa ukianza matus utatukanwa pia alaf ujione Boya tu katkat ya wanaume
 
Kwa hiyo walimu na askari ndio wanaongoza kupokea mishahara midogo?
Ni sawa tu sema askar ana faida maana wanakuwa na uhakika wa pesa zingine za ziada za kudhurum watu mbal na hapo nao Ni njaa Kali tu ,tunao kitaa hasa wanakaa kituon muda wote Wana njaa balaa Bora wale wa Doria na barabaran hao hawana njaa kiivo
 
Kuna mahali umesema kila mtu ni boss wa mwalimu.

Hapa ndio nimeamini walimu mna tatizo, hivi ni kwamba hamjui mnawajibika kwanani?.

Poleni ndugu zangu walimu
 
We Lofa Acha kuongopea watu!!! Hivi unaujua mshahara wa askar wwe!!!

Askari analipwa kutokana na Cheo alichonacho pamoja na Elimu yake!!

Kiufupi Askari mishahara imepishana ... Unaweza mkuta askari hana cheo ..lakin elimu yake anakula sawa na mweny nyota:

Uwezi linganisha mshahala wa Askari Form four ..coplo na Mwalimu senior mwenye Bachelor'
Ma askari mbona mna hasira na sie waalimu kila mtu ashinde mechi zake.
 
Unafahaku askari wanakipwa mshahara kuoibgana na elimu yake? Askari wenye vyeo sawa na elimu tofauti mishahara yao ni tofauti pia.
Constable mwenye form 5 ana mshahara wake certificate ana wake au diploma mpaka bachelor ni tofauti
Form five ni kitu gani kuna elimu ya form five?
 
Kuna mahali umesema kila mtu ni boss wa mwalimu.

Hapa ndio nimeamini walimu mna tatizo, hivi ni kwamba hamjui mnawajibika kwanani?.

Poleni ndugu zangu walimu
Labda wasio jitambua aje ata nani toto lake jinga aone kama yeye ni boss wangu
 
Utakufa maskini iwapo utaendelea kulia lia na kujiona mnyonge. Unapoteza muda wako kumpigia mbuzi gitaa! Kujiongeza kwa wafanyakazi wote hakukwepeki kwa sasa!

Ni bora kuhamishia nguvu na akili zetu kwenye mambo yetu binafsi badala ya kazi yenye manyanyaso. Dawa ya moto ni moto tu. Huduma zikiendelea kudorora, akili zao zitawakaa sawa tu.

Fungua biashara, anzisha shughuli za kilimo na ufungaji, endesha boda boda, nk. Ili kujiongezea kipato. Ukipata wasaa wa kumuibia muda mwajiri, iba kama huna akili nzuri vile! Ndivyo wanavyotaka tufanye.

Haiwezekani miaka zaidi ya sita tuishi kwa mishahara ile ile!
Kuna walimu wa shule x mzembe wa mwisho anavuna gunia 600 za mahindi kwa mwaka sidhani kama wale walimu wanaweza kuja kuandika haya humu.
 
Hakuna wakati binadamu anaridhika hata angepewa mamilioni ya hela angetaka aongezewe tu...

Sasa kama walimu wanataka mishahara ya nyongeza labda wangeacha kazi kama wanayopata sasa haiwatoshi ili wawapishe wenye kutaka ajira na hiyo mishahara midogo, my take: "walimu tuwe na mioyo ya shukrani"
 
Uelewa wako ndio tatizo ,tumeshuhudia askar wengi wakistaf wanavyotia huruma ,na ingekuwa Haina maana hiyo kitu nadhn tusingeshuhudia askar kibao wakistaf na kukatalia kwenye kota za polisi.

Huwez kujua faida ya mafao pengine had uwe na mzaz ambaye ashapata mafao.

Wazaz wang wote wawil walikuwa walimu na wamestaf mzee alilamba 106m huku bimkubwa akilamba 102m na ukiwaona Bado Ni shupavu na wanachapa Kaz za shamban ambazo kwa vijana wa Sasa hawawez ,kwa hapo kwann mafao yasizungumziwe na Kwann yasionekane Yana faida kwa maisha ya baadae.

Turud kwa askar ambao tunao kitaa yaan ukimwona askar aliyestaf alaf ukamringanisha na mwalim hapo ndio utaelewa nn namanisha .kwa kifup askar walio weng wanamaliza vibaya Kaz zao huku walimu wakimakiza vizur baada ya utumish wao .
ni ukweli
 
Mwalimu huwez kujilinganisha na Askari asee had utake posho Kama wao, afadhali manesi kidogo watapata angalau hoja ya kutetea wazo kama hili tena kdogo , wewe mwalimu huna hoja ya kutetea wazo lako.
Mi naona mwalimu una muda mwingi wa kufanya kaz zako binafs fungua hata biashara ukimaliza muda wa kaz komaa na biashara yako kwasababu wewe una masaa maalum ya kuwepo kazin. Kumbuka mshahara hauwez kukutajirisha na hata hiyo posho ukipewa utalalamika haitoshi kama unabisha watafute hata hao Askari uwaulize kama hizo posho znatosha

Hapo kwenye suala la kila mtu ni boss kwa mwalimu hilo nalikubali, walimu ni waoga mno huwa hawajiamin hilo Sasa ni tatizo binafsi, akiona mtu kanyonga tai na suti ye anajua ni boss wake na unaweza hata kwenda shule kuwapiga mkwara wakijua we ni boss wao
 
Back
Top Bottom