Gai da seboga
JF-Expert Member
- Apr 19, 2019
- 482
- 969
Habar zenu mabibi na mababu,
Mwalimu ni mtu anaesaidia wengine kupata ujuzi, maarifa na tunu. Mwalimu ndie anaezalisha Madaktari, manesi, bwana afya, wanasiasa, wafanyabiashara n.k, na wote mnaweza kukubaliana nami kuwa bila mwalimu huenda usingeweza kusoma, kuhesabu na kuandika.
Pamoja na uzito huo alonao mwalimu lakini hakuna watumishi wa serikali wenye hali mbaya ya kiuchumi kama walimu yaani mishahara ni midogo, mikopo kwenye mabenki, hakuna nyongeza ya mshahara, hakuna kupanda madaraja, hana cha kulipwa over time, hakuna cha pesa za semina kama zamani, hakuna ata kudunduliza kupata hela ya tuisheni yani ni shida tupu zimewajaa.
Mbaya zaidi kwenye sekta ya ualimu kila mtu ni bosi wako yani hata mwenyekiti wa mtaa anaweza kuja ofisini kwako na akakugombesha na hata kukutia makofi, ni sekta ambayo imeshushiwa heshima kwa kiasi kikubwa sn.
Leo hii ukimkuta mwalimu barabarani anaongea peke yake unaweza kusema amemeza notes kumbe ni msongo wa mawazo unampeleka puta Vibaya mno akifikiria ni miaka mitano sasa lakini bado mshahara ni ule ule hakuna ata senti ya nyongeza, hajapanda daraja, anachopokea mwisho wa mwezi ni laki mbili akikatwa mkopo alochukua benki, huku ukizingatia gharama za maisha zimepanda na familia imeongezeka.
Kiukweli ukipasua vifua vya walimu utakutana na masononeko makubwa mnoo, walimu wamechooka sana ule uvumilivu walokuwa wanasifiwa nao sasa haupo tena nao ni binadamu, walimu wameshachoka na kutothaminiwa maslahi yao ni ule uoga tu wa kutosema hadharani wakihofia kupoteza ata hako kibarua. Leo hii bora ya bwana afya anaweza pata posho ya kukagua nyama na akarudi na kilo ya nyama nyumbani, heri ya maaskari wenye posho kila mwezi, heri ya watumishi wengine wenye hadi marupurupu ya overtime.. Leo hii kwa shida anazonuka mwalimu tukitaka kuwavalisha kiatu hiki cha mwalimu watumishi wengine wa serikali basi lazima kiwabane tu.
Asilimia 100% walimu waliamini kuwa kupata Rais ambae ni mwalimu kungepelekea kuboreshewa maslahi yao na mazingira ya kazi kwani anayajua yote yaliyomo kwenye sekta ya ualimu lakini mambo yamekuwa tofauti kabisa mpaka walimu wanawaza ni nani sasa atakuja kuwa mtetezi wao kama sio mwalimu mwenzao.! Mara nyingi Mh Rais Magufuli amekuwa akinukuliwa akisema kuwa serikali yake haitawaacha walimu (maneno ambayo yamezoeleka masikioni mwa walimu mwaka wa 6 huu) tena anaenda mbali kwa kusema kuwa yeye ni mwalimu, mkewe ni mwalimu, waziri mkuu ni mwalimu, mkewe ni mwalimu, huku baraza lake la mawaziri likiwa limesheheni walimu mbalimbali, lakini yote haya haijawahi kamwe kuwa chachu ya kuthaminiwa maslahi ya walimu. Kiasi kwamba walimu sasa wanamkumbuka na kumlilia mh Kikwete kwa namna alivyokuwa akiwapandishia watumishi mishahara yao.
Mheshimiwa Rais Magufuli walimu wako wamekata tamaa na wamechoka na maneno yako ya matumaini yasiyozaa matunda kila siku kuwa serikali yako iko pamoja na walimu lakin wapi! kiasi kwamba wanafanya kazi ilimradi siku ziende tu lakini hawana motisha yoyote wanayoipata ili kufanya kazi kwa moyo wote. Tena walimu wako wanatamani muda wako wa kuongoza (kutawala) uishe ata kesho ili wabadilishe upepo angalau Raisi ajae anaweza kuwaona na kujali maslahi yao.
Mheshimiwa Rais John Magufuli ikikupendeza walimu nao wapate posho za kila mwezi kama maaskari ili iwe sehemu ya kuwapa motisha wachape kazi kisawasawa, na ni imani yangu walimu wakiwekewa utaratibu wa kupata posho walau laki mbili basi tutaingia katika Mapinduzi makubwa ya elimu mana walimu watafanya kazi kufa kupona na kutakuwa na ushindani na hari ya kufundisha. Mhe Raisi wahurumie Walimu wenzako wanashindwa kukwambia ukweli kwasababu wanakuogopa.
~Gai da Seboga (Mwalimu wa Kujitolea)