Walimu na upuuzi wa dezo ya nauli

Nsimbi

JF-Expert Member
Sep 27, 2014
1,091
1,202
Kama gvt inawajali walimu basi iwalipe posho ya maana ya usafiri. Iwalipe madeni Yao Na iongeze mshahara Yao. Hakuna Mwalimu anayetaka dezo ya nauli ya daladala. Ni udhalilishaji Na upuuzi mtupu Mr Makonda. Nia huenda Ukawa nzuri lakini nauli si kipaombele... Priority ya walimu si kupata dezo!
 
Mi sio mwalimu lakini suala la eti nauli bure naona Kama cheap politics. Walipeni walimu mishahara minono. Yes you can. 'Sio chako' do something don't stand there like a statue!!!
 
Walimu watafadhaika, viwango vya ufaulu vitashuka zaidi. Tafadhali dc makonda usiwatumie walimu kujipatia umaarufu wa kisiasa, tekeleza ilani ya chama chako.
 
Kinachofanyika hapa ni kukwepa madai ya waalimu ya nyongeza ya mishahara,malimbikizo na posho.
Huu ni mpango mahususi wa kuwapumbaza walimu waone kama serikali inawajali.
Kama Makonda ana dhamira ya dhati kuwasaidia waalimu,apaze sauti kuitaka serikali kuwalipa mishahara inayoendana na mfumko wa bei ndani ya nchi,malimbikizo yao na posho.Bila ya kuongolea haya atakuwa ni mtafuta sifa.
 
Its divide and rule. Kila DC akiweka mfumo wa kuwapoza walimu ktk eneo lake watasahau madai yao ya msingi kuboresha hali zao. Lkn Makonda pia anaexploit vacuum ktk mfumo imara wa kusimamia hali bora za wafanyakazi kitaifa.
 
Wakati unasema hayo wenzio wa wilaya ya magu wameambiwa na dc kila jumamos waende shule kufanya usafi!!!
Wakafanye tu hakuna namna nyingine tena, na jumapili wakapalilie mahindi ya shule.
 
Hahahahahahaaaa,wakapalilie na mahindi?.
Hizi ni dharau,wakafanye usafi wa mji ama kusimamia usafi wa mazingira ya shule?
 
Kama kuna mwalimu anachekelea hiyo dezo ya nauli sio mzima, ni mara elf kumi angesema walimu wapewe posho ya nauli kuliko hizo biashara za kupanda hiace bure mi naona ni udhalilishaji tu
 
napataga tabu sana nikiwa naskia na kuona matatizo,shida,tabu,dharau,unyanyasaji wanaokumbananao walimu wakati na mimi nikijiandaa kuwa mwalimu
 
Niko na ticha hapa dah hataki hata kusikia habari eti za kupanda daladala bure, acheni kuzingua ongezeni walimu mishahara bana
 
Kwa mbali naona kama ni mkakati wa chama tawala kuwapofusha walimu juu ya madeni yao.
Hii mi CWT inafanya kazi gani?.
Kwa nini wakubaliane na huu udhalilishaji kwa waalimu?.
Nasubiria kwa hamu huu mpango ufike AR,nitafanya kampein kwa waalimu wa mji mzima kuupinga kama MKOBA na KUYENGA hawatajitokeza.
 
Huyo Dc Makonda anatafuta attention tu kwa migongo ya walimu anasaka umaarufu soon aonekane bora na kusaka Ubunge, Awaache walimu mana ata position yake hawezi kuwathiri jamaa ni kiazi sana juzi anadai bar zijengwe sehemu moja tu hizo ni akili kweli Ma DC wengine bna
 
Makonda anapenda sifa balaa. Kwa nini bure? Bure si heshima. Magufuli wape walimu mshahara wa maana. Wanastahili. Huruma za kinafiki hatutaki. Mwisho mtasema wapewe soda bure. Acha blablaaa
 
Hvi sisi tupewe dezo wakati watu wanapewa transport allowance? Halafu watu wanajua walimu wapo dar tu eeh?
 
Hata mimi kama ndiyo ningekuwa mwalimu wa Dar es salaam singeikubali hiyo ofa ya Makonda kwa sababu zifuatazo:
1.Si walimu pekee ndiyo wanaotakiwa kuwahi kazini
2.Walimu wasitumike kama mtaji au ngazi ya kupatia umaarufu wa mtu kisiasa kwakujifanya eti wanawajali sana
3.Walimu hawaja wahi lalamika kuwa kikwazo kikubwa kwao ni nauli ya kwenda nakurudi kazini
4.Walimu hawapokei mishahara midogo kiasi cha kukosa nauli
5.Matatizo ya walimu kwa serikali ni mengi,lakini usafiri wa kwenda kazini siyo moja wapo
6.Kama nia yake ni nzuri angewaingizia katika mishahara yao hiyo nauli ili walimu wajue usafiri utakao wafisha shuleni.
7.Imekuwa kawaida kuwataja walimu,polisi na manesi katika mitaji ya kisiasa kama kejeli,ukiidai serikali madeni kama huku kwetu wanataka barua ya madai eti iambatane na bank statement ilihali wakijua kabisa kama deni lina miaka 6,bank statement inaweza kugharimu hata laki 5.Nilimwona mzee mmoja aliambiwa bank statement ya mwaka 1 atoe 85,000 mpka akaamua kuacha madai yake.
Najua makonda anania njema lakini njia ile inaweza kusababisha usumbufu na kebehi kwa walimu,badala yake apiganie masilahi ya hao walimu yaboreshwe na siyo kuwafanya walimu kama watoto yatima au ombaomba,kwani wapo watumishi wanamishara midogo kuliko hao walimu lakini hawasemewi.
 
Hivi Rais mwetu Mwl.Dr.JPM hawama Disii unawaacha ya nini huku wanatudhalilisha!Naomba ifikapo juma tatu ijayo,uwe umeshawarudisha kwwnye kazi zao za awali,na wala usiwapangie kazi zingine
 
Kama gvt inawajali walimu basi iwalipe posho ya maana ya usafiri. Iwalipe madeni Yao Na iongeze mshahara Yao. Hakuna Mwalimu anayetaka dezo ya nauli ya daladala. Ni udhalilishaji Na upuuzi mtupu Mr Makonda. Nia huenda Ukawa nzuri lakini nauli si kipaombele... Priority ya walimu si kupata dezo!
Huna Mada zingine tofauti na hili la walimu? Mbona lilishajadiliwa kitambo humu hili swala??

Walimu wameipokea Fursa na wanapanda daladala bure!

Kama vipi na wewe somea ualimu upande daladala bure!
 
Back
Top Bottom