KERO Latra Temeke usafiri wa Vikunai na nauli zake hazieleweki

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

wmy

New Member
Aug 16, 2024
1
0
Wakazi wa Vikunai kata ya Toangoma, wilayani Temeke usafiri wetu umekuwa ni wa kubahatisa na nauli zake hazieleweki.

Kwa mfano kuna ruti za Vikunai - Stesheni via Kijichi na ruti ya Vikunai Stesheni via Zakhem vivyo hivyo kwa ruti za Gerezani hazifiki kabisa Vikunai huna zinaishia Zakhem kwa zil ile ruti ya Zakhem na zile za ruti ya Kijichi huishia mgeninani au Mbagala kuu na zile za Temeke nauli zake hutoza zaidi ya umbali kwa mfano bei elekezi ya Latra ni 600 kutoka Vikunai hadi mtoni mtongani na hivyo hivyo bei elekezi toka Temeke hadi kituo cha Kanisani ni 600 lakini wahudumu wa daladala hizo hutoza kiasi cha 700 ambayo ni nauli ya kutoka Temeke hadi Vikunai au Vikunai hadi Temeke.

Soma Pia: LATRA, mulikeni ukiukwaji mkubwa wa bei elekezi za nauli katika njia za Kibiti, Ikwiriri na Muhoro

Pia huna na tabia ya kukatiza safari na kushia Mbagala Zakhem, Mbagala kuu au mgeninani na shida hizi huwa nyakati za asubuhi na jioni wakati wananchi wanahitaji huduma hiyi. Vilevile bajaji zinazofanya safari za Vikunai tokea Zakhem bei zao hubadilisha kutoka na muda kwa mfano asubuhi hadi jioni bei ni 800 ikifika saa 12 jioni nauli ni 1000 saa 1 usiku 1,500 saa 2 usiku na kuendelea ni TZS 2,000 na kuendelea.

Tunaomba Latra ilifanyie kazi tatizo hili kwani bajaji hizo zimefanyia figisi haice ambazo zilikuwa zinafanya safari zake kwa bei elekezi ya Latra ili ziondoke watoe huduma wao wafanye wanavyo weza wao.

Tunaomba mamlaka husika kifuatilia jambo hili
 
Back
Top Bottom