Hivi karibuni waziri wa elimu ameibuka na hoja ya kuwataka walimu wafanye mtihani ili waweze kuajiriwa, nawabieni ndugu zangu walimu mnaosubiri ajira huu ni mtego mkiingia katika huu mtego mtadhalilishwa na kutukanwa sana, jiulize swali dogo tu imekuwaje wizara imeshindwa kuvuamini vyombo vyake kama NECTA na TCU iamue kutunga mitihani yenyewe, mtego.
Ukweli ni kwamba serikali inataka kukwepa jukumu lake la kuajiri, inataka kupunguza walimu waliojaa mtaani ilihali shule hazina walimu, mkifanya hii mitihani idadi kubwa itafelishwa halafu wanasiasa wataibuka na kusema walimu hawana uwezo ni vilaza na jamii itawaamini na kuwaona nyie ni mbumbumbu kweli.
Kama serikali inataka kuajiri walimu walio bora ni bora ingesema walimu wafanyiwe usaili kama zinavyofanya shule za private kuliko hiyo mitihani yao ya sasa, huwezi kupima ubora wa mtu aliyekaa mtaani miaka nane(8) kwa mtihani tu.
Kama serikali inataka walimu bora basi ikubali kuingia gharama iwarudishe vyuoni hata kwa mwaka mmoja hawa walimu waliopo mtaani iwajengee uwezo upya, na sio kuleta mitihani ya siku moja ili kupima uwezo wa walimu.