Walimu msikubali haya

Tanzania Nchi Yetu Sote

JF-Expert Member
Mar 12, 2017
505
871
Nimeona habari kwenye gazeti moja yenye kichwa cha maneno WALIMU "KUULAMBA" FULANA ZA MWAKA JANA MEI MOSI. Maelezo ya habari hiyo yanaonesha kuwa ukata umesababisha wahusika kushindwa kuzalisha fulana za mwaka huu na hivyo kuwataka walimu kuvalia zile za mwaka jana.

Kama kweli ni hivyo na walimu wakaitikia kuzivaa hakika utakuwa ni udhalili wa hali ya juu na kujishushia hadhi kulikopitiliza.

Kama hakuna pesa za kuzalisha fulana mpya za mwaka huu ni vyema walimu wakavaa mavazi yao ya kawaida na kuhudhuria maadhimisho hayo.

b80c3a9e0e4e454953e6533731ac31a9.jpg
 
Tutafua tu,kwanza kabisa namfata dogo aniletee nitamrudishia jumanne.Milijua tutapata mpya nikampatia.
Sasa nao makato yote yale ka shati tu bila suruali kameshindikana!
Mtatuchosha.
 
Kwani hizo fulana zinawasaidia nini walimu?
Watatue kero za walimu kama ni fulana watavaa zao au mashati yao.
Kwani bila kuvaa sare hio mei mosi haiwezi kufanyika?
Msituchoshe
 
Kila mwezi CWT wanaramba hela ya hicho chama lakini wanashindwa kununua T-shirt jamani! Kuna Vyama kama TUGHE wengine hata sio wanachama kwa maana hawachangii kila mwezi ila mei mosi bila kujali ni mchangiaji au la! Watu wanapigwa fulana,kofia,mwanvuli na pengine kitenge,sasa hao CWT wanaramba hela per month halafu wanaleta ngonjera zao hizo kweli walimu wapole sana.
 
Back
Top Bottom