Tetesi: Walimu Kilindi Tanga watakiwa kujihamisha wenyewe

Nguva Jike

JF-Expert Member
Jan 22, 2018
856
1,006
Habari za jioni.

Walimu kadhaa waliohamishwa wakiwemo walimu wa Parakuyo primary school ambao shule yao imetwaliwa na mamlaka ya Handeni Mji kutokana na mabadiliko ya kimipaka yaliyomalizwa tangu mwezi Julai 2023.

Hayo inasemekana yamesemwa na mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilindi Mh.Msigwa alipoombwa kutoa ufafanuzi juu ya lini stahiki za madai hayo ya uhamisho zitatolewa ili walimu wahamishe vyombo vyao na familia zao kutoka Parakuyo primary school.

Ufafanuzi huo uliombwa kutokana na walimu wa Handeni Mji kutaka walimu wenzao watoe vyombo ili waingize vyao jambo ambalo walimu wa Parakuyo wamepinga vikali pamoja na kupewa vitisho.

Rai yangu ya kistarabu ni kuomba mamlaka zinazohusika watatue suala hili kihekima ili kuepusha mgogoro unaoweza kuzuilika.Baadhi ya walimu wa Parakuyo walihamishiwa shuleni hapo mnamo December 2022 bila kulipwa na bila wao kuomba kituo hicho.

Sheria za kiutumishi zinatamka kuwa mtumishi aliekaa kituo cha kazi kwa zaidi ya miaka mitano anatakiwa alipwe hata kama ataomba mwenyewe kuhama.Fikiria mwalimu kajihamisha mwenyewe mwaka jana na mwaka huu tena ajihamishe mwenyewe CWT MLAANIWE LAANA KUU AMEN.

Barua hii aione mh katibu tawala mkoa wa Tanga mezani.Mkurugenzi amesema Halmashauri haina pesa za kuwalipa hivyo wajihamishe wenyewe mpaka pesa itakapopatikana ndo watalipwa.
 
.

Sheria za kiutumishi zinatamka kuwa mtumishi aliekaa kituo cha kazi kwa zaidi ya miaka mitano anatakiwa alipwe hata kama ataomba mwenyewe kuhama.
Mkuu kasome tena sheria za kazi na utumishi,sheria inasema kuwa mtumishi anaweza lipwa fedha ya uhamisho ikiwa amekaa kwa kituo chake cha kazi zaidi ya miaka mitano hata kama ataomba yeye kuhama, elewa neno anaweza lipwa, hivyo sheria haijeweka ulazima kama ilivyo kwa mtumishi ambaye atahamishwa na mwajiri wake
 
Mkuu kasome tena sheria za kazi na utumishi,sheria inasema kuwa mtumishi anaweza lipwa fedha ya uhamisho ikiwa amekaa kwa kituo chake cha kazi zaidi ya miaka mitano hata kama ataomba yeye kuhama,elewa neno anaweza lipwa,hivyo sheria haijeweka ulazima kama ilivyo kwa mtumishi ambaye atahamishwa na mwajiri wake
Sawa Sheria za kazi zinasemaje endapo mtumishi atahamishwa kutoka kituo A kwenda kituo B?
 
Back
Top Bottom