Walimu kwanini mnawadhalilisha watoto?

Habarini za weekend wanaJF;
Nimesikitishwa sana na hizi video au post ambazo Mwalimu anapost au anasambaza mitandaoni huku akiwa anafundisha, tena anaonesha jinsi gani mwanafunzi anayemfundisha ambavyo haelewi ambae ni Mtoto mdogo under 10, najiuliza hivi maadili mliofundishwa huko vyuoni yanawaelekeza mfanye hivi.

Je wazazi wa hao watoto wakiwafungulia mashitaka mtasema mnaonewa,

Assume ni mwanao Unaingia mitandaoni unakuta video inaonesha jinsi gani alivyo bashite,

Assume baada ya miaka 30 Uyo Mtoto anakuja kuwa mwanasiasa na video Kama hizi hujui kwa kiasi gani utamdhalilisha?

Ombi kwenu walimu watendeeni watoto wetu Kama mnavyotaka wa kwenu watendewe, Kama mnaona ni sawa rudini vyuoni mkasome hata business administration inatosha video

Video zimegoma ku-upload

Mimi nadhani wizara husika ambayo ni wizara ya elimu na Tamisemi amabo ni wasimamizi wa shule waweke terms and condition kuhusu video zinazoweka mitandao na walimu. Tumewapelekea watoto ili wafundishwe kusoma na si kudhalilishwa, video nimeoina yule mototo siyo kuwa hajui kusoma bali inaonekana mwalimu wake ni katili kiasi kuwa yule mototo anamuogopa, ndo maana unaona anajaribu kusoma huku aitumia nguvu nyingi sana kuhakikisha hakosei. Alafu unakuta mwalimu kama huyu hata cheti anachotumia cha mtu mwingine. Hata yeye angekuwa genius asingekuwa mwalimu wa shule ya msingi. Bahati mbaya sana hatumjui lakini naamini kama amemaliza form 4 miaka ya 2000 kurudi chini sifa ya kwenda ualimu ilikuwa ni DDDDDDD (7Ds) anamdhalilishaje mototo ambaye anaonekana anaelewa? huu ni upuuzi na ushamba. Maafisa elimu pigeni marufuku simu shuleni make walimu ambao ni watu wazima wanashindwa kubehave ama kuwa na moral ambayo inaendana na kazi zao basi wasaidiwe kubehave. Inakera sanaa.
 
Back
Top Bottom