Walimu kwanini mnawadhalilisha watoto?

Cendy

JF-Expert Member
Mar 28, 2015
1,250
2,309
Habarini za weekend wanaJF;
Nimesikitishwa sana na hizi video au post ambazo Mwalimu anapost au anasambaza mitandaoni huku akiwa anafundisha, tena anaonesha jinsi gani mwanafunzi anayemfundisha ambavyo haelewi ambae ni Mtoto mdogo under 10, najiuliza hivi maadili mliofundishwa huko vyuoni yanawaelekeza mfanye hivi.

Je wazazi wa hao watoto wakiwafungulia mashitaka mtasema mnaonewa,

Assume ni mwanao Unaingia mitandaoni unakuta video inaonesha jinsi gani alivyo bashite,

Assume baada ya miaka 30 Uyo Mtoto anakuja kuwa mwanasiasa na video Kama hizi hujui kwa kiasi gani utamdhalilisha?

Ombi kwenu walimu watendeeni watoto wetu Kama mnavyotaka wa kwenu watendewe, Kama mnaona ni sawa rudini vyuoni mkasome hata business administration inatosha video

Video zimegoma ku-upload
 
Waalimu ni janga la uadilifu wa watoto nchini, yaani waalimu wengi ni vilaza na malimbukeni...samahani kwa hiyo kauli. Unajua huu mchezo wa kuchukua maksi za chini ndio wasomee ualimu...haiko sawa. Yaani kwenye Whatsap Nina waalimu ambao wanapost vipicha vya watoto yaani anafundisha anamuita Mtoto mmoja anaklmuelekeza ampige picha akiwa anafundisha...au anamuita mwalimu mwenzie ampige picha...au ampige picha akiwa anawachapa watoto...yaani waalimu ni shidaaaa!!!.. Sijui lakini huko tuendako....ila kwasasa waalimu ni vilaza
 
Mkuu kama ni ile video mtoto ana hesabu huku machozi yana mtoka,hakika ule ni udhalilishaji wa hali ya juu.Nakuombea hata wewe iendelee kukugomea maana utakuwa umeshiriki kumdhalilisha mtoto na wazazi wake pia
Hapana mkuu zipo video nyingi Sana siku hizi
 
Waalimu ni janga la uadilifu wa watoto nchini, yaani waalimu wengi ni vilaza na malimbukeni...samahani kwa hiyo kauli. Unajua huu mchezo wa kuchukua maksi za chini ndio wasomee ualimu...haiko sawa. Yaani kwenye Whatsap Nina waalimu ambao wanapost vipicha vya watoto yaani anafundisha anamuita Mtoto mmoja anaklmuelekeza ampige picha akiwa anafundisha...au anamuita mwalimu mwenzie ampige picha...au ampige picha akiwa anawachapa watoto...yaani waalimu ni shidaaaa!!!.. Sijui lakini huko tuendako....ila kwasasa waalimu ni vilaza
Wakiambiwa inaonekana wanaonewa
 
walimu wa siku hizi wapumbavu pumbavu tu hasa wa sekondari.

wavaa milegezo na modo.

wanachoweza ni kupambana na wanafunzi kwa viboko na kugombania mademu.
Maadili gani haya umefunzwa na wazazi wako ya kutukana watu?,au wewe ni mtoto uliyekulia mitaani??!!!
 
Walimu alikuwa mwalimu Nyerere na Yesu pekee ...hawa wasiku hizi ni waganga njaa tu.
 
Back
Top Bottom