Walimu kudai motisha wakati wanafunzi 85 wamepata daraja sifuri ni sawa

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,902
51,995
Nilipitia matokeo ya kidato cha nne shule ya sekondary nachingwea ya 2015 ambako wanafunzi 85 kati ya wanafunzi 133 waliofanya mtihani wamepata DIVISION ZERO

Hivi walimu kama hao wakiomba wapewe motisha kuna uhalali hapo? Motisha hutolewa kwa mtu anayefelisha watoto?

Walimu wenyewe wajitathmini waangalie matokeo ya mitihani ya shule zao kabla ya kudai wapandishwe vyeo au wapewe motisha.

Kuanzia leo mimi Yehodaya nikiwa na akili timamu kabisa naagiza KILA MWALIMU aambatanishe matokeo ya mitihani ya shule yake kwenye maombi yake ya kupandishwa mshahara au cheo au kupewa motisha.

Ombi lolote ambalo halitakuwa na nakala ya matokeo ya mtihani halitashughulikiwa
 
Km mwanafunzi hajiwezi utamfantaje?tusiwadharau walimu km ndo wanafelisha wanafunzi,tukumbuke nasi tumetoka hukohuko na walimu hao ndo wametufundisha mpk umepata kazi nzuri nje ya ualimu,tusiseme tu ili kufurahisha watu,tuwathamini walimu wetuuu
 
Hakuna relationship Wa correlation ktk nchi hii hasa kwa govt schools kati ya poor performance and teachers salary. Hayo unayongea ni sawa na kuulizwa we dini gani ukatibu mi mwanaume au mwanamke.
Madaraja wapewe tu performance ni wwe mwenyewe mwanafunzi ujue kipi kimekupeleka shula
 
Nilipitia matokeo ya kidato cha nne shule ya sekondary nachingwea ya 2015 ambako wanafunzi 85 kati ya wanafunzi 133 waliofanya mtihani wamepata DIVISION ZERO

Hivi walimu kama hao wakiomba wapewe motisha kuna uhalali hapo? Motisha hutolewa kwa mtu anayefelisha watoto?

Walimu wenyewe wajitathmini waangalie matokeo ya mitihani ya shule zao kabla ya kudai wapandishwe vyeo au wapewe motisha.

Kuanzia leo mimi Yehodaya nikiwa na akili timamu kabisa naagiza KILA MWALIMU aambatanishe matokeo ya mitihani ya shule yake kwenye maombi yake ya kupandishwa mshahara au cheo au kupewa motisha.
Ww kama nani? uwezo wako wa kufikiri umeishia hapo? pole sana
 
walimu wanaidai serikali mabilioni ya pesa na serikali haiwalipi......mazingira mabovu ya kufanyia kazi......unategemea watafanyaje kazi...serikali iboreshe mazingira ...iwalipe madeni yao...la sivyo wa kulaumiwa ni serikali ya CCM
 
Sijajua ufahamu Wa mtoa mada kuhusu shule na elimu...ni ajabu kufikiri kazi ya kufaulu ni ya mwalimu pekee.
Kwahiyo wewe ukitenda dhambi tumlaumu kiongozi wako wa dini?
 
Mtoa mada huna akili kabisa, hata mchele huoshwa na kuchujwa kabla ya kupikwa, ndio sembuse wanafunzi, huko private wanachuja, vipi serikalini, nako wanachujwa? Badala ya kuwaambia ukweli walioua mfumo wa elimu ya nchii hii, mmekalia kulaum walimu. Poor you!
 
Wanastahili maana kama siyo jitihada zao darasa zima lingepata Div. Zero...
 
Na mkiendelea kunyanyasa walimu,mwakani shule za serikali zote zitakuwa ni ziroooo zirooooo kama Chris Brown, wapeni hela zao wanazowadai ndo muulize kuhusu uwajibikaji wao .......Over
 
Kama wapo waliofaulu maanake walimu wanatimiza wajibu wao wa kufundisha.

Wazazi wenyewe wanazaa mazezeta tu halafu wanayanyonyesha miezi mitatu wanawaachia house girls,unategemea nini?matokeo yake yamedumaa akili so mengi hayafundishiki.

BTW:Kazi ya mwalimu ni kufundisha,kufaulu ni juhudi,uwezo,bidii na msukumo binafsi wa mwanafunzi katika masomo.
 
Hivi walimu kama hao wakiomba wapewe motisha kuna uhalali hapo? Motisha hutolewa kwa mtu anayefelisha watoto?

Ni kweli, lakini kumbuka hata hospitali nako si wote wanaokwenda kutibiwa wanapona,
 
Back
Top Bottom