Uchaguzi 2020 Walidhani wananchi wanataka ndege kumbe wananchi wanataka uhuru kwanza

Wananchi huwa hawaeleweki akiwapa uhuru mnataka ndege hamtaki uhuru akiwapa ndege hamtaki ndege mnataka uhuru kwahiyo kaamua aforce kimoja
 
Unatembea kwenye lami , gari zuri , kwenye madaraja makubwa na kupanda ndege lakini nakula Milo miwili asubuhi chai na kitumbua kimoja ,mchana nashindia maji hafu mpaka usiku napiga ugari na bamia mix nyanya chungu au chainizi. Aisee kwa maisha haya sijui kama ndakuchagia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kati ya Jambo linaloigharimu CCm kila siku Ni kuwekeza kwa Mwenyekiti na dola kuliko kuwekeza kwa wananchi.

Wananchi kwa namna Hali ilivyo wanatambua hata ungekuwa na utajiri mkubwa kiasi gani lakini watu wakakosa Uhuru ipo siku utajiri huo utapotea.

Tunajenga vitu na ni Jambo jema ila tulipokosea nikuthamini vitu tukasau utu. Hakuna daraja wala ndege wa jengo lolote linaweza kuthaminishwa na utu..nafsi ya mtu ni ghali kuliko kitu chochote.

Mnaendelea kuwekeza kwenye vitu bila uungwaji mkono wa watu Jambo linalovikosesha vitu hivyo thamani.

JK alijenga mwendo kasi akaweka na mfumo mzuri wa kuhudumia watu, awamo ya tano imeachana kabisa na miundombinu hiyo nakujikita kwen
Mtageukana mwaka huu. Nyimbo za Stigler na SGR zimefeli.
 
Kama Mungu mwenyewe anataka tuishi kwa kumtumikia ila tukiwa na uhuru wa kuamua tupendacho yeye nani tumkumbatie tu wakati hata ninapoandika comment hii nawaza huenda kesho sitaandika tena kutokana na wale watu wabaya!?
Kwa kweli kwenye kura nitakoleza kabisa kuisaka nchi ya amani na haki
 
Kati ya Jambo linaloigharimu CCm kila siku Ni kuwekeza kwa Mwenyekiti na dola kuliko kuwekeza kwa wananchi.

Wananchi kwa namna Hali ilivyo wanatambua hata ungekuwa na utajiri mkubwa kiasi gani lakini watu wakakosa Uhuru ipo siku utajiri huo utapotea.

Tunajenga vitu na ni Jambo jema ila tulipokosea nikuthamini vitu tukasau utu. Hakuna daraja wala ndege wa jengo lolote linaweza kuthaminishwa na utu..nafsi ya mtu ni ghali kuliko kitu chochote.

Mnaendelea kuwekeza kwenye vitu bila uungwaji mkono wa watu Jambo linalovikosesha vitu hivyo thamani.

JK alijenga mwendo kasi akaweka na mfumo mzuri wa kuhudumia watu, awamo ya tano imeachana kabisa na miundombinu hiyo nakujikita kwen
We Bite wewe, mbona unataka nitamani kuingia ktk ndoa za mitaala kwa kuguswa na wanamama jasiri na wa kipekee wenye uelewa wa ziada wa mambo muhimu yanayohusu kesho ya mama Tanzania. Kongole nyingi sana kwako.
 
Back
Top Bottom