MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,976
Watanzania hatujawahi kufikiria ukanda katika maisha yetu ya kijamii na kisiasa. Mimi kuna watu ninafanya nao kazi/biashara hata siwafahamu kabila lao achilia mbali sehemu wanayotoka.
Walichofanya CHADEMA kupitia kwa Tundu Lissu kinafanya tuanze kuuliza maswali ambayo wao wenyewe wana majibu kwa sababu wanaziangalia siasa nchini kwa jicho la ukanda na ukabila.
CHADEMA inayolalamika kuwa Rais Magufuli anapendelea kanda ya Ziwa imesahau kuwa ilipeleka majina mawili ya Ezekiel Wenje na Lau Masha ambao ni wanachadema kutoka kanda ya Ziwa ili wakachaguliwe kuwa wabunge wa bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati ina wanachama katika maeneo mengine ya nchi.
Kupeleka bungeni watu wawili wanatoka katika kanda moja na dini moja hawakuona kama ni kupendelea kanda ya Ziwa?
CHADEMA haikuona kuwa kufanya hivyo ni kuendelea kutoa nafasi/vyeo/madaraka kwa watu wa kanda ya ziwa? Au huo ukanda wanauona kwa wengine tu?
Kama vigezo vya kuwateua havikuhusu ukanda, kwa nini wanadhani wengine watateua kwa vigezo vya ukanda?
Kilichoshangaza zaidi, CHADEMA ilipewa nafasi mbili za kuteua majina na ikatumia nafasi hizo kuteua majina ya watu wa kanda ya ziwa na wenye imani ya dini moja. Kwa nini hawakuteua majina kutoka kanda zingine ili ‘’kupunguza’’ wanaoteuliwa kutoka kanda ya Ziwa kama wanajua kuwa Rais Magufuli anapendelea watu wa kanda ya ziwa?
Wabunge hawakuwapa kura za ushindi kina Wenje na Masha ili kuingia EALA kwa sababu wanatoka kanda ya Ziwa bali walikataliwa kwa sababu wabunge walijua hawatoshi.
Mwandishi wa vitabu wa Kimarekani E. W. Howe aliwahi kusema, ‘’A thief believes everybody steals’’.
Mimi ninasema, mbaguzi hudhani kila mtu ni mbaguzi.
Ezekiel Wenje na Lawrence Masha wakiwa kanisani.