Walichofanya polisi arusha ni sahihi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Walichofanya polisi arusha ni sahihi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Madikizela, Jan 15, 2011.

 1. Madikizela

  Madikizela JF-Expert Member

  #1
  Jan 15, 2011
  Joined: Jul 4, 2009
  Messages: 319
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Nimekuwa nikifuatilia maoni mbali mbali kuhusu fujo zilizotokea Arusha, wachangiaji wengi wamekuwa wakilaumu polisi tena bila kuficha ushabiki wao kwa CDM. Binafsi mimi si shabiki wa chama chochote kile, na hivyo kwa mtazamo wangu baada ya kuangalia TBC muda mfupi uliopita nimeona kuwa polisi walifanya sawa na kama mauaji yalikuwa si ya kukusudia.

  Hivi katika hali kama ile ya padre mwenzagu slaa kuamuru kuwatoa mahabusu kwa nguvu ilikuwa ni sahihi?. nimekuwa nikuvutiwa sana na siasa za CDM lakini sasa huku wanakoelekea wananipa simanzi.

  Najua wengi watasema " Angeuawa ndugu yako n.k" lakini hii ni forum ya GREAT THINKERS tuache ushabiki wa siasa tujadili ukweli na haki ili kuweza kuiimarisha CDM ambayo imeanza kujenga imani kwa Wa Tanzania
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Jan 15, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Padri unaficha jina, kumbe unagopa wanadamu wanaoua mwili! Fake padre
   
 3. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #3
  Jan 15, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Mods ziunganisheni hizi threads zimekuwa utitiri!
   
 4. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #4
  Jan 15, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Polisi waliandaa taarifa kwa makusudi ya watu kama wewe ili uweze kuamini kuwa walichofanya kilikuwa sahihi. Endelea kuamini kwa sababu hilo ndilo lengo lau, ila ingekuwa vizuri ungesikia na upande wa pili unasemaje,
   
 5. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #5
  Jan 16, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,307
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  hali hiyo ilitokea baada ya watu kupigwa na polisi bila sababu na kuharibu mali za watu wakiwemo wana cdm kwa maksudi. Mbaya zaidi ni kumjeruhi josephine na kumpandisha kwenye landrover lao ki udhalilishaji na hadi kubaki nusu uchi.Pia kuwakamata mwenyekiti wa cdm na mbunge wa arusha bila sababu ya msingi. nasikitika inteliensia haikunusa kuwa hili lingeleta vurugu. pia Sheria ya nchi hairuhusu askari wa kiume kuarrest mwanamke lakini kwa josephine ilhfanyika. Wewe ungekuwa dr. Slaa ungekuwa kwenye position ipi ? Na kama polisi ni wakweli na walilenga kuwapa wananchi ukweli,mbona walifuta picha zote kwenye kamera za wanahabari kwa nguvu? Walitaka kuficha nini? Mbona kwenye mkanda wao sijaona ile gari nyekundu ikivunjwa kioo na police? Wanajaribu kutumia mbinu za kizamani kudeal na watu wa kisasa. Hawatatufikisha. Huko mbeya slaa alikuwepo? Unatetea wauaji mkuu!?
   
 6. V

  Vipaji Senior Member

  #6
  Jan 17, 2011
  Joined: Jun 11, 2009
  Messages: 115
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kufa kwa raia si swala la Chadema. Ukifikiri sana waliopata hasara baada ya kuuawa jamaa zao ni watoto na wake zao, machozi yao ni laana ambayo inaitafuna nchi wala sio Chadema tu kama maswala nyeti kama haya hayawezi kukemewa na wakubwa. Sitegemei kumpamba muuaji hata siku moja hata akiua kwa jiwe. Ukizingatia waliokuwa wanaandamana hawakuwa na silaha.

  Ndiyo maana kikatiba kibali cha maandamano ya vyama hawatoi Polisi.

  Hata Polisi wajisafishe namna gani lakini bado wao ni wauaji na wezi na ndiyo wanaowalinda mafisadi.

  Angalia Tukio la Ubaruku Mbeya, Tukio la juzi hapa DSM kijana aliyepigwa risasi na kutelekezwa, kule Shinyanga kulikuwa na maandamano ya Chadema?. Damu hii lazima wailipe, bila kuomba radhi tutaanza na sisi kuwavuna mmoja baada ya mwingine kuanzia familia zao hadi kieleweke.
   
 7. NGUZO

  NGUZO JF-Expert Member

  #7
  Jan 17, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 253
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Mimi pia ni mmoja wa watu walofuatilia taarifa kwa karibu, jamani tukubali Viongozi wa CHADEMA hawakwepi lawama hapa, walochochea watu waende kuwatoa kina Mbowe kwa nguvu kituo kikuu cha polis, pamoja na kupigwa mabomu ya machozi, risas za baridi lakini waaapi, jamaa wakawa wanaenda tu kukivamia kituo kikuu ambacho kilikuwa na siraha nzito nzito, hivi kweli hawa jamaa wangezifikia siraha hizo kungekuwa na usalama? nadhani Maaskofu wetu wameumbuliwa vibaya na video hii, ngoja tusikie watatoka na lipi kutetea Uovu huu uloletwa na viongozi wa CHADEMA.
   
 8. t

  talumba mkiwa Member

  #8
  Jan 17, 2011
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tuwe wa kweli chadema ni chama makini lakini kwa hili walikosea maana kama wangeweza kuingia kituoni wangechukua silaha arusha pasingekalika maana wenye vurugu kama hizo wezi wenye nia na kuiba silaha wasingekosekana
   
 9. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #9
  Jan 17, 2011
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,480
  Likes Received: 2,074
  Trophy Points: 280
  ile video imechakachuliwa kwa ajili ya watu kama nyie ambao hamkufatilia toka mwanzo mkaona vitu halisi vilivyotendeka. Sikujua kama walivyo edit ile video wangekamata akili za baadhi ya watu wa JF (Great Thinkers)
   
 10. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #10
  Jan 17, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  tafuta taarifa za upande wa pili-then compare na hizo ulizoona kwenye tbc utapata jibu-usipende kurely on single source
   
 11. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #11
  Jan 17, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  MADIKIZELA tafadhali rekebisha kauli yako kwenye hiyo RED maneno uliyoongea! natumaini wewe ni mamluki wa chama fulani! na ninavyohisi hiyo TV uliyokua unaangalia bila kukosea ni ile mliyomchakachua TIDO MHANDO pole sana na endelea kuangalia TBC 1 upate habari za kiupotoshaji!
   
 12. W

  WAKIJIJI Member

  #12
  Jan 17, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Taarifa huru ni hii ya Tanzania Daima natumaini ni gazeti makini na linaaminika kwa wanachadema, nanukuu:

  SLAA, MBOWE WAKAMATWA

  Na waandishi wetu, Arusha.

  Mbowe na wabunge hao ndio walikuwa wa kwanza kukamatwa jana mchana wakati wakiongoza maandamano hayo huku Dk Slaa akiwa amekamatwa jioni ya saa mbili kasorobo usiku pamoja na mbunge wa Moshi mjini, Philemon Ndesamburo.

  Kabla ya Dk Slaa na Ndesamburo kukamatwa walihutubia maelfu ya wananchi waliokuwa wamefurika katika viwanja vya NMC eneo la Unga Limited lakini baadae walitangaza kuuvunja mkutano huo na kuamuru umati wote uelekee kwenye kituo kikuu cha polisi walikokuwa wameshikiliwa Mbowe na viongozi wengine ili wakafuatilie kwa pamoja hatima ya viongozi wao.

  Source: Tanzania Daima, ukurasa wa 2, alhamisi tarehe 6 Januari. 2011
  MSOMI ni mtu mwenye kuvutiwa na fikra na mwenye mbinu za kizisarifu na kuzitumia vilivyo (fikra hizo) baadhi au zote. Profesa Ali Mazrui.
   
 13. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #13
  Jan 18, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,499
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Huhitaji kuwa mtaalamu kugundua kuwa video ya polisi ilichakachuliwa. Kama uliangalia vizuri, uliona majeruhi wakiokotwa kwenye viwanja vya polisi? Je maiti zilikutwa wapi? Ile ya mkenya iliokotwa wapi?
  Hivi ulitegemea pilisi waonyeshe video ya kuwaumbua wao?. Mbona hawakuonyesha arrest ya Josephine na walivyokuwa wakimpiga?
  Always try to read between the lines or look carefully between pictures.
  Na kama ingekuwa video ni sahihi, kwa nini polisi wachukue siku zote hizo kuionyesha? Si walikuwa wanaifanyia editing ili kuichakachua?
  Nakuhakikishia zipo video sahihi zimeshatumwa kwa Ocampo!!. Wewe, mpaka JK kufikia mahali pa kujaribu kujiosha (na kuwabembeleza) kwa mabalozi wa nje, ujue kuna jambo. Video zilizoonyeshwa Australia uliziona?
   
 14. Zegreaty

  Zegreaty JF-Expert Member

  #14
  Jan 18, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 638
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kama mtu makini basi usingekubali kutoa hitimisho kwa sinema ile iliyotolewa na polisi na kuoneshwa,tukio la zaidi ya masaa 10,ukalitazame kwenye sinema ya dakika 10,halafu eti na wewe unajiita mtu makini?unamuuita mtu padre?unaonesha jinsi gani ulivyokuwa mamluki na mbinafsi wa kuvaa midwanda ya kilimo kwanza aka kijani na njano........
  mtake msitake mwisho wenu umefika..........................................:ban:
   
 15. akajasembamba

  akajasembamba Senior Member

  #15
  Jan 18, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 161
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kituo cha polisi kisingefuatwa kama maandamano yangeruhusiwa na pia kama viongozi wa chadema wasingekamatwa, wa kubeba lawama zote ni yule aliyezuia maandamano ambayo ni haki isiyo jadiliwa ya binadamu! Hilo la kuelekea kituo cha polisi si geni na wala lisikuzwe! Limeshatokea Moshi Mjini wakati wa uchaguzi Mgombea Udiwani wa Chadema aliwekwa ndani na wafuasi wa Chadema walijaa kuzunguka kituo hakuna jiwe wala changarawe iliyorushwa na alipopewa dhamana wakaondoka!Tatizo la polisi wakiona umati wa watu wamejikusanya na wapo tayari kutembea kwa miguu yao kuonyesha mapenzi kwa chama tofauti basi lazma wawa discourage na kuwahumiliate ili ionekane wapinzani wa chama tawala wapo wachache na hawana mapenzi na chama chao, ule usemi wa chokochoko za watu wa chache ili uzidi kuendelezwa.Lawama ni kwa wote walioharamisha haki ya kuandamana.
   
 16. K

  Kimanzi Member

  #16
  Jan 18, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe mkuu una matatizo kweli. Polisi wamepiga watu risasi, wakaua harafu unasema walikuwa sahihi! Sahihi katika kuua. Kwa mfano Josephine ilikuwaje akapigwa namna ile? Alikuwa jambazi? Je aliongea nini akiwa anapigwa? Bado unasema padre mwenzako eti kaamuru kuwatoa mahabusu! wewe ni padre? Basi una hatari kweli. Polisi walitakiwa kulinda maandamano hadi mwisho,kama ingetokea waandamanaji wakafanya fujo hapo tungeweza kuwalaumu waandamanaji na si vinginevyo.
  Afterall kwani taarifa ya IGP ya kuzuia maandamano wewe unafikiri aliitowa katika muda muafaka? Je alikuwa tayari kugharamia pesa iliyokwishatumika katika kuandaa mkutano?
  Raia yeyote hata Rais amesema ni bahati mbaya... Sasa wewe unasema eti Polisi walikuwa sahihi, tena eti umeangalia video.. ya Polisi pale TBC1, shame on you..
   
 17. l

  lebabu11 JF-Expert Member

  #17
  Jan 18, 2011
  Joined: Mar 27, 2010
  Messages: 1,651
  Likes Received: 518
  Trophy Points: 280
  Ndg,

  Yaelekea hujui unachosema ni sahihi ni kipi.
  Je ni sahihi kisheria na kimaadili polisi kupiga raia wanaoandamana hata kama maandamano yangekuwa siyo halali?
  Je ni sahihi kisheria na kimaadili polisi kupambana na kuua raia wasio na silaha kwa kutumia risasi za moto?
  Je ni sahihi kisheria na kimaadili polisi kuharibu magari ya raia kama ilivyoonekana kupitia tv kwa kisingizio cha kuvunja maandamano?
  Tafadhali jibu maswali hayo uthibitishe ukweli na haki au usahihi unaomaanisha.
   
 18. K

  Kidogo chetu JF-Expert Member

  #18
  Jan 18, 2011
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 771
  Trophy Points: 280
  pande zote haziwezi kukwepa lawama tuache ushabiki wa kijinga
   
 19. MJINI CHAI

  MJINI CHAI JF-Expert Member

  #19
  Jan 18, 2011
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 1,801
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  Don't come with simple mind...bana this is JF
   
 20. MJINI CHAI

  MJINI CHAI JF-Expert Member

  #20
  Jan 18, 2011
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 1,801
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  Mkuu taarifa zilizotolewa na chombo kimoja cha habari, inaonyeshakusadikika ya kuwa Dr. Slaa aliamuru watu waliopo kwenye mkutano waende Polisi wakawatoe Viongozi wao waliokamatwa na akawauliza Vijana waliopo pale kuwa majumbani kwenu hamna Baba anaefanana na MH Ndesamburo kwani polisi wamempiga mabomu ya machozi na kurudia rudia maneno hayo, sasa swali!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
  1. vijana wa kawaida watawezaje vipi kuwatoa viongozi/watuhumiwa wao pale Polisi bila ya kuvunja kituo cha Polisi? na kama kingevunjwa nini kingetokea?
  2.kama jengo la polisi lingevunjwa na nadhani kuna Nyaraka nyingi muhimu (kama silaha nk nk ) nini kingetokea? kwa nyaraka hizo kuwa mikononi mwa watu ambao sio wahusika inawezekana hata hii leo tunapoandika haya sijui tungekuwa wapi?
  3. lengo hasa la Dr lilikuwa ni kuwatoa viongozi kweli? au Kafara, kushinikiza Serikali ya mseto, au ni kuwaonyesha waTZ kuwa unapoambiwa kitu changanya na zako? maana nadhani kwa vijana wale hata yeye analijua hili wasingeweza kuwatoa

  mwisho imefika wakati wa kupima tunayoambiwa/tunachotaka kufanya, hasa kipindi hiki ambacho kina mkangajiko wa maisha kuna Falsafa moja inasema kuwa mwangalifu unapokuwa na FURAHA au SHIDA
   
Loading...