Khantwe
JF-Expert Member
- Dec 20, 2012
- 59,413
- 119,279
Hello guys,
Kwa wale wanaopenda kula kama mimi nimeona niwashirikishe hili pishi rahisi sana. Mwaka jana mwishoni katika kuhangaika na maisha nilienda mkoa mmoja ndanindani huko. Kule nilikuta wanapika wali wa kitunguu kwa kweli niliupenda. Pengine wengine mnajua ila nina uhakika wapo ambao hawafahamu. Twende pamoja.
1. Andaa kitunguu maji katakata vipande vya kawaida.
2. Tia mafuta kwenye sufuria unayotaka kupikia wali (hakikisha umeandaa maji ya moto pembeni).
3. Tia vitunguu kwenye mafuta yaliyochemka, kaanga mpaka viungue (sio viive, vinatakiwa viungue).
4. Tia mchele, geuza hadi vitunguu vichanganyike na vitunguu (mchele ubadilike rangi). Baada ya hapo tia maji na endelea na hatua zingine kama kawaida.
Wali unakuwa na ladha fulani hivi ya kuvutia, mimi niliupenda najua na wewe utaupenda