Wali wa kitunguu

Khantwe

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
59,412
119,143
Hello guys,

Kwa wale wanaopenda kula kama mimi nimeona niwashirikishe hili pishi rahisi sana. Mwaka jana mwishoni katika kuhangaika na maisha nilienda mkoa mmoja ndanindani huko. Kule nilikuta wanapika wali wa kitunguu kwa kweli niliupenda. Pengine wengine mnajua ila nina uhakika wapo ambao hawafahamu. Twende pamoja.

1. Andaa kitunguu maji katakata vipande vya kawaida.

2. Tia mafuta kwenye sufuria unayotaka kupikia wali (hakikisha umeandaa maji ya moto pembeni).

3. Tia vitunguu kwenye mafuta yaliyochemka, kaanga mpaka viungue (sio viive, vinatakiwa viungue).

4. Tia mchele, geuza hadi vitunguu vichanganyike na vitunguu (mchele ubadilike rangi). Baada ya hapo tia maji na endelea na hatua zingine kama kawaida.

Wali unakuwa na ladha fulani hivi ya kuvutia, mimi niliupenda najua na wewe utaupenda
 
Niliwahi kuona mtu alipika huo wali ukabadilika na kua wa brown alisema wao wanaita pilau, binafsi ulinishinda ila napika wali wa kitunguu, kitunguu hakiivi sana, napenda viwe vinaonekana nikila.

Boost your Immune System to fight a Covid-19.
 
Nialike siku moja mkuu nije kuonja mapishi
 
Ukiunguza vitunguu kidogo lazima ubadilike rangi unaelekea kufanya pishi la pilau, mimi huwa napika hivi nikiweka vitunguu kwenye mafuta naweka na mchele hapo hapo,vitunguu havibadiliki rangi hivyo wali una kuwa mweupe vile vile wenye vitunguu vinavyoonekana.
Nami naona hii ya kwako iko poa.
Ya kuunguza vitunguu inakuwa haieleweki kama mtoto wa pilau au wali mweupe.
 
Niliwahi kuona mtu alipika huo wali ukabadilika na kua wa brown alisema wao wanaita pilau, binafsi ulinishinda ila napika wali wa kitunguu, kitunguu hakiivi sana, napenda viwe vinaonekana nikila.

Boost your Immune System to fight a Covid-19.
Unapenda ule wali wenye vitunguu visivyoiva sana vinakuwa vyeupe vyeupe na vile vimstari vyao....Huo huwa unanishinda Miss..Tena nikiwa nakula nikakutana nacho cha hivyo mdomoni hadi appetite inachange.
 
mwenye mji wake keshasema ugonjwa tumeushinda.

vyakula nipendavyo ni wali wa kitunguu kwa main rost.
Hapo umenifikisha, maini roast yatupiwe na njegere kiasi, unaweza kuweka tui zito kiduchu kutafuta fleva ya nazi na maini yakawa na muonekano bomba wenye ladha taaamu.

Tatizo nakaa sigimbi huko ndani ndani, siku nikija kwa jiji la Makonda nitakupa mualiko wa nguvu.
 
Unapenda ule wali wenye vitunguu visivyoiva sana vinakuwa vyeupe vyeupe na vile vimstari vyao....Huo huwa unanishinda Miss..Tena nikiwa nakula nikakutana nacho cha hivyo mdomoni hadi appetite inachange.
Naam huo huo, hahaha kama ukiona tu kitunguu appetite inakata je ukiona hiliki kwenye wali utakula kweli?

Subiri nikupe mualiko wa chakula cha wali wa vitunguu chagua mboga uipendayo tu, hiyo dhana itaisha mbona.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom