Walevi wanaume watatu; Watoto hospitali

Walevi wanaume watatu; Watoto hospitali

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
15,465
Reaction score
29,654
Walevi wanaume watatu baada ya kinywaji cha masaa kadhaa walianza kuwakebehi wake zao;

Mlevi wa Kwanza: Mke wangu ni mjinga sijapata kuona. Eti anataka tununue mabati ya kuezekea nyumba hata kiwanja cha kujengea hiyo nyumba hatuna.


Mlevi wa pili: I say afadhali wako. Mie wa kwangu ndio mjinga usiseme, maana kila wakati anafikiri yeye ni mwana anga wa Apolo yuko mwezini wakati wote tupo hapa hapa duniani, na hata ndege hajawahi panda!


Mlevi wa tatu: Yaani nyote nyie wake zenu tisa kwa ujinga, wakwangu bwana jana alikuwa anasafiri, akapaki kondom za kiume kwenye begi la safari wakati dushulele hana, ninalo mie na sikuwa na mpango wa kumuachia aende nalo safari!


Watoto hospitali

Watoto wawili wadogo wa kike na kiume walikuwa wanasubiri kumuona daktari. Yule wa kike akawa analia chini chini.

"Kwa nini unalia?" mtoto mvulana akamuuliza yule mtoto wa kike

"Nimekuja kupima damu naogopa dokta atanikata kidole"
Kusikia hivyo, yule mtoto wa kiume nae akaanza kulia.

"Na wewe kwa nini unalia" akauliza mtoto wa kike
"Mie nimekuja kupima mkojo, basi dokta atakata nanii yangu"
 
Back
Top Bottom