Walevi bwana!!

Walevi bwana!!

hahahahahaaaa!!! Waungwana mmenifurahissha sana hapa.
Afrodenzi umesema kitu ya maana sana aseee........kuna jamaa yetu, dah!! Kudadeki, anapiga simu huyo...wakati wa bill tu.
 
Ukiwa kwenye ibada unafanya ya kwenye ibada, ukiwa baa unafanya ya kwenye baa. Ya nini kuchanganya masomo?
Na pesa ya pombe kwa mswahili haina bajeti, inategemea umekutana na nani baa
 
mkuu, tatizo la watu wasiokunywa pombe ni kwamba, wanaona wanywaji wanapoteza fedha zao, na kwamba wakitaka fedha wanataka wapewe tu kwasababu wanafikiri wanajua what is best for you. Hata ukiwa huna, wanaona unadanganya.

Sisi hata tukiwa hatuna mia, hatushindwi kunywa hata kulewa tukitaka......sisi ni waungwana sana, tunapendana sana tukiwa counter.

Poleni nyie msiopendana.
 
Afu inanishangaza
bia za home huwa hazina povu kabisa
hadi uende baa ndo zinanoga
 
Hawa jamaa wanapopiga "round" kwenye vikao vyao huwa hawana hiyana katika kutoa pesa. Tatizo linakuja pale inapohitajika pesa kwa matumizi mengine nje ya kununua pombe wanakuwa wagumu kweli, sijui tatizo ni nini!

Mimi sio mlevi, ila kuna kanuni inasema: nunua kinywaji chako otherwise usije bar. Na ukija na nikakununulia jiandae kuninunulia next time. Kwa kukunulia kinywaji unataka ninunue chakula cha familia yako?
 
Kwakuwa hamjui utamu wa pombe ndio maana.
 
Ukiwa kwenye ibada unafanya ya kwenye ibada, ukiwa baa unafanya ya kwenye baa. Ya nini kuchanganya masomo?
Na pesa ya pombe kwa mswahili haina bajeti, inategemea umekutana na nani baa

id yako inajieleza!
 
Shetani tu anawadanganya, sura ya Mungu inawapima sana walevi sema hawajui na hawawezi kumtambua anakujaje hata siku moja, anakuja kwako kukuomba msaada wa kawaida unakataa hata kumtengea au unampa 500, anakuja mtu mwingine anakuomba umkatie chupa kadhaa za bia unamkatia ambayo ni sawa au karibia na 5,000 hivi au zaidi, Mungu humjali yupi kati ya hao? Mungu hata siku moja hawezi kutoa msaada wa bia! fikiria hapo.....!!
 
Back
Top Bottom