Safari_ni_Safari
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 23,265
- 17,135
Hata mie napenda serikali moja ila kwa hapa tulipofikia sidhan
Dah...safi sana!
Tume ya Mabadiliko ya Katiba imewasilisha maoni ya Watanzania walio wengi waliotaka serikali kuu moja yenye maeneo nyeti machache ya utawala.Hivi kuna yeyote mwingine kama mimi anayetaka serikali kuu moja tu?
Tume ya Mabadiliko ya Katiba imewasilisha maoni ya Watanzania walio wengi waliotaka serikali kuu moja yenye maeneo nyeti machache ya utawala.
Sijui unapata wapi mawazo kwamba hakuna waliotaka serikali kuu moja.
Ni kama nilivyosema, serikali kuu iliyopendekezwa na walio wengi, asilimia 61 ya Watanzania Bara, ni moja, itakayoshughulikia masuala machache yasiyo ya Muungano, kama Ulinzi na Usalama. Na kutakuwa na mkuu mmoja wa serikali kuu moja, Rais wa Jamhuri moja ya Muungano.#Katiba Bungeni: Warioba aibua mjadala wa serikali tatu
Tanzania bara:
13% walipendekeza serikali MOJA
24% walipendekeza serikali mbili
61% walipendekeza serikali TATU
Zanzibar:
34% walipendekeza serikali mbili
60% walipendekeza muungano wa mkataba
0.1%(watu 25) walipendekeza serikali moja
Wanachama wa JF nao walifunguka hapa
Ni kama nilivyosema, serikali kuu iliyopendekezwa na walio wengi, asilimia 61 ya Watanzania Bara, ni moja, itakayoshughulikia masuala machache yasiyo ya Muungano, kama Ulinzi na Usalama. Na kutakuwa na mkuu mmoja wa serikali kuu moja, Rais wa Jamhuri moja ya Muungano.
Well, kwa sababu wangechukua mapendekezo ya Wazanzibar Tume ingeulizwa kwa nini hawakuchukua mapendekezo ya Watanganyika.Kama wa Bara asilimia 61 walitaka Serikali Tatu na Zanzibar asilimia 60 walitaka Muungano wa Mkataba kwanini TUme ya Warioba iliamua kuchukua mapendekezo ya watu wa Tanganyika badala ya wale wa Zanzibar?
Ndio, lakini serikali kuu uliyoiongelea, iliyopendekezwa na wengi, ni moja, itakayosimamia machache ya pande zote.licha ya Warioba mwenyewe kusema asilimia 61 walipendekeza serikali TATU
Nyani Ngabu mimi binafsi ni muumini wa serikali moja lakini kinachosababisha mjadala kuwa wa serikali mbili au tatu ni kutokana na msimamo wa chama tawala juu ya serikali mbili ambayo ni sera yao rasmi sambamba na vyama vikuu vya upinzani kusimamia serikali tatu.Zimekosekana taasisi zenye ushawishi ili kuibua mjadala wa serikali moja.
Lakini kuna baadhi ya vitu kuhusu serikali moja ni dhahiri haitekelezeki kwa mfano Wazanzibar wanataka serikali yao yenye mamlaka kamili kama nchi hili ni gumu kulibadili kwa hapa tulipofikia.Watanganyika ni rahisi kuwashawishi kukubali serikali moja lakini si Wazanzibar hivyo kupona kwa muungano ni kuwa na mfumo au muundo ambao hautawameza.
Fact ya ugumu wa kuwashawishi Wazanzibar kukubali serikali moja ndio inayonifanya binafsi kukubali option ya serikali tatu kama ilivyopendekezwa na tume badala ya hiki kiini macho cha serikali mbili ambacho hata kama imedumu kwa miaka 50 lakini ilipofikia hatuwezi kujidanganya tutakwenda tena miaka mingine 50 kwa mfumo huu huu tukabaki salama.
Ushauri wa muundo wa serikali 3 wa Tume ukubaliwe na ubalishwe tu pale wazanzibari watakapopendekeza muungano wa serikali moja.
Ndio, lakini serikali kuu uliyoiongelea, iliyopendekezwa na wengi, ni moja, itakayosimamia machache ya pande zote.
Hivi kuna yeyote mwingine kama mimi anayetaka serikali kuu moja tu?
Yaani ni serikali moja tu, la sivyo muungano unakufa.
Manake ninaowasikia wengi wao ni ama serikali mbili au tatu.
Wa serikali moja wako wapi?
Hapana, serikali kuu iliyopendekezwa na wengi ndio moja, hii itakuwa na mamlaka katika mambo machache yanatakayoanishwa. Hakutakuwa na serikali kuu nyingi nyingi na waliopendekeza serikali kuu moja si wachache.uko sahihi. Serikali ni moja tu.
kuna yeyote mwingine kama mimi anayetaka serikali kuu moja tu?