Wale wa serikali moja.....

Wale wa serikali moja.....

Mimi ni mtanganyika nisiyetaka munuungano, sitaki serekali moja wala mbili wala tatu. Nataka nchi yangu ya tanganyika na sio muungano wa kulazimishana. Viongozi wa tanganyika wanaiogopa zanziba wanafanya kwa matakwa ya zanziba. Viongozi wa tanganyika hawajielewi wanashabikia muungano usiokuwepo. Kama ni undungu tunao hata na kenya Burundi, Congo, Uganda, Malawi, Msumbiji kwanini iwe tu zanziba
 
Ushauri wa muundo wa serikali 3 wa Tume ukubaliwe na ubalishwe tu pale wazanzibari watakapopendekeza muungano wa serikali moja.
 
Hivi kuna yeyote mwingine kama mimi anayetaka serikali kuu moja tu?
Tume ya Mabadiliko ya Katiba imewasilisha maoni ya Watanzania walio wengi waliotaka serikali kuu moja yenye maeneo nyeti machache ya utawala.

Sijui unapata wapi mawazo kwamba hakuna waliotaka serikali kuu moja.
 
Tume ya Mabadiliko ya Katiba imewasilisha maoni ya Watanzania walio wengi waliotaka serikali kuu moja yenye maeneo nyeti machache ya utawala.

Sijui unapata wapi mawazo kwamba hakuna waliotaka serikali kuu moja.

#Katiba Bungeni: Warioba aibua mjadala wa serikali tatu



Tanzania bara:

13% walipendekeza serikali MOJA
24% walipendekeza serikali mbili
61% walipendekeza serikali TATU

Zanzibar:

34% walipendekeza serikali mbili
60% walipendekeza muungano wa mkataba
0.1%(watu 25) walipendekeza serikali moja

Wanachama wa JF nao walifunguka hapa
 
Last edited by a moderator:
#Katiba Bungeni: Warioba aibua mjadala wa serikali tatu



Tanzania bara:

13% walipendekeza serikali MOJA
24% walipendekeza serikali mbili
61% walipendekeza serikali TATU

Zanzibar:

34% walipendekeza serikali mbili
60% walipendekeza muungano wa mkataba
0.1%(watu 25) walipendekeza serikali moja

Wanachama wa JF nao walifunguka hapa
Ni kama nilivyosema, serikali kuu iliyopendekezwa na walio wengi, asilimia 61 ya Watanzania Bara, ni moja, itakayoshughulikia masuala machache yasiyo ya Muungano, kama Ulinzi na Usalama. Na kutakuwa na mkuu mmoja wa serikali kuu moja, Rais wa Jamhuri moja ya Muungano.
 
Last edited by a moderator:
Ni kama nilivyosema, serikali kuu iliyopendekezwa na walio wengi, asilimia 61 ya Watanzania Bara, ni moja, itakayoshughulikia masuala machache yasiyo ya Muungano, kama Ulinzi na Usalama. Na kutakuwa na mkuu mmoja wa serikali kuu moja, Rais wa Jamhuri moja ya Muungano.

Haya, sawa. Uko sahihi, ulikuwa sahihi, na mara zote huwa uko sahihi. Hakuna cha serikali tatu na hakuna waliopendekeza serikali tatu (licha ya Warioba mwenyewe kusema asilimia 61 walipendekeza serikali TATU). Hongera!
 
Kama wa Bara asilimia 61 walitaka Serikali Tatu na Zanzibar asilimia 60 walitaka Muungano wa Mkataba kwanini TUme ya Warioba iliamua kuchukua mapendekezo ya watu wa Tanganyika badala ya wale wa Zanzibar? au kutafuta 'compromise of sort'? Siyo kwamba mapendekezo ya Wazanzibari kwa mara nyingine tena yamepuuzwa...?
 
Kama wa Bara asilimia 61 walitaka Serikali Tatu na Zanzibar asilimia 60 walitaka Muungano wa Mkataba kwanini TUme ya Warioba iliamua kuchukua mapendekezo ya watu wa Tanganyika badala ya wale wa Zanzibar?
Well, kwa sababu wangechukua mapendekezo ya Wazanzibar Tume ingeulizwa kwa nini hawakuchukua mapendekezo ya Watanganyika.

Hivyo ni bora kuchukua mapendekezo ya walio wengi, yani asilimia 61 dhidi ya 60, vitu vingine vyovyote vikichukuliwa kuwa sawa, kama vile idadi ya watu kila upande.

Ambayo hata hivyo si sawa. Hata mapendekezo ya asilimia 10 ya Watanganyika yangechukuliwa bado wangekuwa wengi kuliko asilimia 100 ya Wazanzibari kama wote wangefikiri pamoja.

Kwa hiyo kuna sababu zisizohesabika za kuchukua mawazo ya Watanganyika.

licha ya Warioba mwenyewe kusema asilimia 61 walipendekeza serikali TATU
Ndio, lakini serikali kuu uliyoiongelea, iliyopendekezwa na wengi, ni moja, itakayosimamia machache ya pande zote.
 
Nyani Ngabu mimi binafsi ni muumini wa serikali moja lakini kinachosababisha mjadala kuwa wa serikali mbili au tatu ni kutokana na msimamo wa chama tawala juu ya serikali mbili ambayo ni sera yao rasmi sambamba na vyama vikuu vya upinzani kusimamia serikali tatu.Zimekosekana taasisi zenye ushawishi ili kuibua mjadala wa serikali moja.

Lakini kuna baadhi ya vitu kuhusu serikali moja ni dhahiri haitekelezeki kwa mfano Wazanzibar wanataka serikali yao yenye mamlaka kamili kama nchi hili ni gumu kulibadili kwa hapa tulipofikia.Watanganyika ni rahisi kuwashawishi kukubali serikali moja lakini si Wazanzibar hivyo kupona kwa muungano ni kuwa na mfumo au muundo ambao hautawameza.

Fact ya ugumu wa kuwashawishi Wazanzibar kukubali serikali moja ndio inayonifanya binafsi kukubali option ya serikali tatu kama ilivyopendekezwa na tume badala ya hiki kiini macho cha serikali mbili ambacho hata kama imedumu kwa miaka 50 lakini ilipofikia hatuwezi kujidanganya tutakwenda tena miaka mingine 50 kwa mfumo huu huu tukabaki salama.

wazenji siwaelewi. eti wanataka muungalo alafu serekali yao bado iwe na mamlaka kamili. hii ni contradicting statement. mimi nataka yalitokea kati ya pakistani na india baada uhuru yatokee bongo.
 
Ushauri wa muundo wa serikali 3 wa Tume ukubaliwe na ubalishwe tu pale wazanzibari watakapopendekeza muungano wa serikali moja.

serkali tatu za nini. embu nieleze faida yoyote tanganyika imeipata na huu muungano. nangojea kuwa fukuza wapemba kariakoo Tanganyika itakapo kuja
 
Ndio, lakini serikali kuu uliyoiongelea, iliyopendekezwa na wengi, ni moja, itakayosimamia machache ya pande zote.

Uko sahihi na mimi nilikosea kuwa na wazo kuwa kuna mambo ya serikali tatu. Narudia tena, uko sahihi. Serikali ni moja tu. Sawa ndugu Anheuser?
 
In order...top to bottom.

1. Nchi moja, Serikali Moja.

2. Nchi Mbili, Serikali Tatu...haki sawa kila upande (arthi, makazi n.k).

3 Kila Nchi Kivyake...!!
 
muungano upi unaotajwa hapa mbona muungano wazanzibar waliuvunja tangu 1984?
 
Hata mie nataka moja tu, ila hiyo moja ikishindikana ndo zije tatu, haiwezekenani nchi moja ndani ya muungano ina katiba na mamlaka yake kamili wakiti nyingine haina mamlaka hayo

Hivi kuna yeyote mwingine kama mimi anayetaka serikali kuu moja tu?

Yaani ni serikali moja tu, la sivyo muungano unakufa.

Manake ninaowasikia wengi wao ni ama serikali mbili au tatu.

Wa serikali moja wako wapi?
 
....hivi inashindikanaje kuwa na nchi moja(JMT) na serikali 3.....kama issue ni kuulinda muungano!....yani kunakua na nchi moja ya JMT...alafu serikali 3(yani JMT,ZNZ na Tanganyika)...kwa maana ya kwamba hapa zenj inabidi wakubali kuwa serikali (si nchi)ndani ya JMT....kunakuwa na rais mmoja tu wa JMT...na mawaziri wakuu wa serikali 3...madaraka yao wale wanaotajwa kuwa marais wa Tannganyik na ZNZ wanakuwa mawaziri wakuu wa serikali hizo na madaraka yao yanabaki hivyo hivyo)....hii option zenj wataikubali...Maana zenj wao concern yao ni power status...sasa kuondoa hii ni kuwapa mawaziri wakuu wa serikali za ZNZ na Tanganyika status kama ya rais....yale madaraka ya marais wa ZNZ na Tanganyika yaliyoainishwa kwenye rasimu wanapewa mawaziri wakuu wa pande zote....na nafasi ya waziri mkuu wa JMT inabaki kama ilivyainishwa kwenye rasimu.. makamu rais wawili wa JMT (kutoka kila upande wa muungano).....alafu kunakuwa na mabaraza ya wawakilishi ya pande mbili kama kwenye rasimu...na pia bunge moja la JMT kama sasa.....i think the CA members should think on these lines...
 
uko sahihi. Serikali ni moja tu.
Hapana, serikali kuu iliyopendekezwa na wengi ndio moja, hii itakuwa na mamlaka katika mambo machache yanatakayoanishwa. Hakutakuwa na serikali kuu nyingi nyingi na waliopendekeza serikali kuu moja si wachache.

kuna yeyote mwingine kama mimi anayetaka serikali kuu moja tu?
 
Mimi nataka serikali moja, ila ili iwe hivyo inabidi kwanza uhakikishe extinction ya wanasiasa wote pamoja na ndgugu zao na marafiki zao wote halafu uanaze na jamii ambayo haijui maana ya madaraka. Sasa kwa vile ni vigumu sana kuwafuta wanasiasa wote , basi nadhani ni afadhali nusu shari kuliko kamili.
 
Back
Top Bottom