Wale tunaopenda kupika

Napenda kupika vitoweo
Vitafunwa na bila kusahau wali
Na mapishi mengineyo ya mchele

Sipendi kupika ugali
 
Hata sijui kwanini maana sometimes nakaaga na kijitabu cha mapishi kabisa ili niende step by step lakini mwisho wa siku natoa kaukau si kaukau,chapati si chapati ili mradi tafrani tu
Pole sana the secret is unaposukuma kwa mara ya pili ile duara usiifanye nyembamba sana itakuwa kaukau na usiifanye nene sana haitaiva ndani,kitu kingine wakati unakanda tumia maji ya moto kiasi siyo ya baridi au ya vuguvugu ili unga uive.ukiwa una kanda tumia mafuta ya kumiminika ya choice yako,chunvi na ukipenda sukari kidogo ili kubalance taste.Unga wako asiwe mgumu tumia maji nusu lita kwa unga kilo moja,then kama utaona ni mlaini kidogo weka unga mpaka uone umekuwa haunati kwenye mikono.Kuwa makini Usifanye huu unga kuwa mgumu.Ukitumia maji ya moto mwanzoni tumia mwikokuukorogea maana utakuwa haushikiki unaunguza kidogo kwa mikono yako laini mizuri Mareth na sipendi uwe na mikono migumu naipenda jinsi ilivyo.Wakati unakanda usiweke mafuta mengi maana round two utaweka tena mafuta na kupika utapikia mafuta,mafuta sio mazuri sana Mareth.Ukiwa mkando wako upo tayari usukume round moja kubwa kwenye meza safi ya jikoni kama unayo,ukiwa umepata hii round huna haja ya kuifanya iwe duara safi Mtoto mzuri.Then ukipata hii duara rough paka blueband itapakae kwenye hii duara isipakaa layer kubwa yaani rashiarashia ila itapakae vizuri.Kata strips ndefu ndefu nyingi kiurefu mpaka umalize hilo duara lote.Usikate stips nyembamba kiupana zile na upana mzuri kidogo,kwa wastan strips kumi hadi kumi na mbili kwa unga kilo moja.Then Unazunguusha kuanzia chini kwenda juu kupata viduara vidogo.Visimamishe hivi viduara uwe unaona ule mzunguuko,vifanye flat kwa kutumia kiganja,then dust na unga kidogo.Kwenye kibao chako na msukumio dust unga kidogo ili chapati yako isinate kwenye vitendea kazi vyako.sukuma upande mmoja juu chini juu chini ili upante kitu chenye urefu lakini mapana kidogo.zunguusha kibao chako usukume ule upande mwingine ambao haukuwa na urefu,this is the secret of getting the chapati round.Juu chini kama upande huu mwingine mpaka tound iwe sawa na ule upande wa mwanzo.lakini unaposukuma uhakikishe chapati yako umedust unga juu na chini na unaweza kugeuza juu kukawa chini na chini kukawa juu wakati wa kusukuma.Weka kikaangio kwenye jiko lenye moto wa wastan na kisha Paka mafuta kikaangio chako,mafuta kidogo,kikaangio kikipata moto,sio moto saana then kwa kutumia napkin paper yafute yale mafuta na weka chapati yako,kila baada ya muda izunguushe bila kuigeuza,then igeuze uingalie kama imebrown ile ya kufifia,ukiona imepata rangi ya kufifia igeuze upande wa pili mpaka ipate rangi kama upande wa kwanza.ikipata rangi hiyo,geuza chapati ule upande wa kwanzalakini kwa chini tia mafuta kidogo kuipa chapati yako rangi ya golden brown kisha malizia upande wa pili kwa utaratibu kama wa upande wa mwanzo.itoe chapati iweke kwenye hot pot na funika,kila mara mara kabla hujaweka chapati ya pili futa kikaangio na tissue paper.Kuna tofauti ya Tissue paper na toilet paper mkuu.Tissue nazozizungumzia ni zile white plain square shape,au zinaitwaga paper napkin ambazo utazikuta hata bar kwa ajili ya kufutia vumbi glass unapoletewa kinywaji.Zoezi la kufuta liendelee kila mara kabla ya kuweka chapati nyingine.Tengeneza chai yako ya tangawizi,mdalasini,karafuu,iliki na mchaichai isiwe na sukari,kila mtu atajiwekea sukari mwenyewe,mimi sipendi chai ya maziwa pliz ya rangi inapendeza na chapati.Nakuja saa saa 4 nikute umejaribu tunywe chai pamoja.;););););););););););):D:D:D
 
napenda sana kupika. chapati za kusukuma aiseeh kwangu ni changamoto.

ila changamoto nyingine baada ya kupika ni kuosha vyombo aiseeh hii kazi huwa naiona ngumu sana. hii changamoto ndo unifanya nisiwe napika.
 
Tembea ujionee, kwanza majani kiafya sio mazuri,Jaribu hivi chukua mdalasini iliki,pilipili manga,karafuu theni twanga vyote kwa pamoja Kwenye kinu kidogo.
Bandika maji yako ya Chai jikoni ya kianza kuchemka weka huo mchanganyiko wa viungo vichemke vizuri utaona vyatoa rangi haina haja ya majani, kwanza chai yawa na harufu nzuri na yanukia
naja kunywa chai yako
 
Chapati uikande na mafuta size na ikiwa laini haikusubui hata kutoa ile round wala huangaiki ukiweka nia utaweza kila kitu kwa nia hakuna kimachoshindikana chini ya jua labda kutafta pumzi tu
Mie nakumbuka siku ya kwanza najifunza Kupika chapati acha yaani zilikua ngumu hizo kona sasa hazifai lakini saiv acha kabisa napika lakini zina nyambuka kama gazeti
 
Nyama ya kusaga
nunua nyama yako ya kusaga au kasage nyama yako
unaweza ichanganya na vitunguu swaum kidogo au hata tangawizi na chumvi kiasi
chemsha jikoni hua haichelewi kuiva hii epua weka pembeni
katakata vitunguu maji vyako kwa mtindo wa pembenne, karoti pia, hoho na uchanganje na ile nyama yako iliyokwish iva

kuna manda za aina mbili zile tunanunua ready made na za kutengeneza mwenyewe

za kutengeneza mwenyewe
chungua unga wangao kanda kama vile chapatti usiwe mwingi chumvi si lazima
kata vitonge vidogo vidogo kisha sukuma kwenye kibao cha chapatti
kile kitonge cha kwanza unachosukuma usisukume sana nyunyizia mafuta kidgo na viunga kwa mbaali
chukua kitonge kingine wekea juu yake sukuma kwa pamoja kupata round nzuri (fanya hivi kwa matonge yaliyobaki) waweza sukuma hata kwenye sinia pia ukaigeuza chini juu weka kikaangio kwenye moto kubabua manda zako usiunguze ipua kata manda zako utaona zinababuka babua kuzifatisha kwa utaratibu tengeneza kifuko

chukua unga wangano changanya na maji kupata uji mzito kiasi

kunja manda kupata shape ya kuwekewa nyama yako na ule mchanganyiko kwa ujumla

utatumia uji huo kushikiza hiko kifuko (sjui utakuwa umenielewa)
 
Siku nikizipika nitakupa feedback
 
Back
Top Bottom