Wazo Langu
JF-Expert Member
- Mar 21, 2011
- 1,381
- 841
Mimi nilisoma advance ila niliipenda sana ile shule kwa sababu nyingi kama;
1.Hakukuwa na matabaka sana.
2.Mkuu alikuwa peace kipindi hiko ni Mwl Urasa msaidizi Mwl Anania.
3.Ufundishaji ni mzuri mfano Sir Mathias alikuwa mtata ila anajua kufundisha.
4.Kiwanda cha Serengeti kilikuwa kinatoa harufu nzuri yani naimis sana.
5.Shule ilikuwa karibu na ofisi ya Mzee kwaiyo nilikuwa nashushwa na gari la mzee getini(mana mimi ni wakishua) wanafunzi wananishangaa.
6.Kubwa kuliko ni, watoto wa kike wa o-level walikuwa wanatukubali advance yani ukikaa kwenye vimbweta lazima wakuletee swali, mimi nilipata kama wanne hivi mmoja nipo nae hadi leo tumeshakuwa.
Vitu vilivyokuwa vinanikera.
1.Ajali kwenye high way(machinjoni)pale pamepoteza maisha ya wanafunzi wengi.
2.Bifu kati ya boys wa o-level yani wavaa kaki na boys wa advance.
3.Advance kupewa madarasa ya kawaida wakati o-level wanakaa ghorofani.
Dah Kibasila high school naikumbuka sana, nilipomaliza nilisikitika.
Kuhusu Advance kupewa madarasa ya chini na olevel kupewa ghorofa hilo ni sawa. O'level ipo mpaka mingi na tulikua tunasomea jengo la ghorofa wakati huo pale kwenye majengo ya advance kulikua na mti mkubwa tulikua tunakaa tunapaita Kibasila Beach. Ni Mwl. Kivugo tu ndio alikua anaweza kufika kibasila beach kuvunja kijiwe.
Harufu ya kimea pale Serengeti aisee inapendeza.
Ila mlikua washamba kuweka bifu na madogo.
Hahahaa... wa Kishua kuachwa getini wakati kuna wanafunzi walikua wanakuja na ndinga zao wanapaki chini ya Mkungu.