Wale ambao wamejiajiri na wenye ndoto za kujiajiri hawajui pakuanzia

Mideko

JF-Expert Member
Mar 30, 2015
36,491
196,533
Watu wengi wanaajiri kwa sababu tofauti, wengine kwakuwa wanapenda, wengine ajira ngumu , mazingira n.k

Kuna vijana wengi ambao wapo mitaani hawajui pakunzia , ila kikubwa safari ya kujiajiri inahitaji kujitoa kwa hali na mali pale unapoianza, kuna kuchekwa na watu, ndugu jamaa na marafiki. Unaweza ukapoteza watu wako wakaribu inategemea na aina ya mradi ulianza nao ila yote kwa yote Hutakiwi kukata tamaa.

Safari yangu ya kujiajiri ilianzia hapa.

1. Biashara yangu ya kwanza nilikuwa nachukua korosho zilizobanguliwa mkoani mtwara kule zinauzwa kilo Sh 16000 kipindi cha msimu mpaka 20000 kama hakuna msimu
--nikawa naleta Dar nauza kilo 30000, nusu 15000, robo 7000. Na nafunga kwenye pakti nauza sh 2000 mpaka 5000

Hii biashara haikufanya vizuri. Nikaachana nayo ila sikukata tamaa.

2. Biashara ya pili nikaanza kutembeza mitumba nguo nachukua Karume, au Tandika kwenye minada ya nguo nikichukua nguo 2000 mtaani nauza 10000 mpaka 15000, wakati nikiwa naenda kufata mizigo nikakutana na mfanyabiashara mwenzangu yeye alikuwa anachanganya nguo za mitumba na handbag za mitumba akaniambia zinalipa na mimi nikajaribu.

3. Biashara ya tatu nikaanza kuunza handbag za mitumba nikawa nachukua Tandika sokoni, nikinunua handbag 15000 mpk 20000 nauza 40000 mpaka 50000. Nikinunua handbag 5000 mpak 10000 nauza 15000 mpaka 20000. Niliona mwanga wa biashara nilikuwa nauza pamoja na nguo nilivoona handbag zinalipa nikaacha biashara ya nguo nika dili na handbag tu.

Mtaji nilianza nao laki 1 nikafikisha laki 8
Nikaanza kukata mabalo mwenyewe, lakini mtaji ulikata kwani nilipata hasara sana. Nikarudi kwenye kutembeza kama kawaida.

3. Biashara yangu ya 3 ni ya mtandao nikaaza kuagiza bidhaa online kwenye mitandao ya Ebay na Aliexpress. Nilidili na vipodozi hasa vya wanawake vya kujichubua kwani huku kwetu kwa sasa ni dili.

Naagiza sabuni kwa 1.5 Usd nauza sh 15000
Serum haya ni maji au vidonge vinawekwa kwenye lotion naagiza kwa 2 usd bongo nauza 20000 mpaka 30000

Lotion naagiza kwa 5 usd nauza kwa 50000
Hii biashara imenipa mwanga na napata faidaa
Mpaka sasa bado sijafika napo kutaka japo namiradi zaidi ya hiyo hapo nimeonyesha tuu nilipoanzia.

Ushauri kwa mnaosubiri ajira msione aibu kwani kadri unavojichanganya ndipo unaongeza mwanya wa kufanikiwa na kuajiriwa tuache kulialia. Mimi elimu yangu ndogo ila namshangaa Graduate wa Tanzania akilalamika njaa.
 
Safi sana, tunaomba waliojiajiri wengine walete uzoefu wao najua wengi tutasaidika hasa ktk serikali hii ambapo ni ngumu sana kuajiriwa hakika bora kujiajiri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kinachowapa jeuri graduate ni degree na ukiangalia alichosomea ni kitu chenye ushindani kwenye soko la ajira hakika ameangamia

iPhone 6s
 
Back
Top Bottom