Wale ambao Mama zetu wametangulia mbele ya haki

Hapa kila mtu namwona anamapenzi na mamake hongereni. Ila mi na mamangu tumechokana kila kukicha ni stress tupu. Malezi yake yamefanya Sina bond na yeye hata kidogo, moyo wangu hauwezi sema kwamba nampenda, na wala simchukii ila huwa ananitia hasira na negative energy, sidhani kama siku akifa ntaumia au ntamkumbuka.
 
Mama ni mama tu.
Katika mabaya kumi sidhani Kama hakuna jema hata moja alilowahi kukufanyia.
Jifunze kumthamini mama yako..kuna watu wanatamani wangekuwa naye Hata huyo unayemuona hafai.
Siku ukimpoteza hutaongea haya unayoyaongea.
Thamani ya kitu huonekana kikitoweka.
Jifunze kuona thamani ya kitu kingali kipo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa sababu yuko hai
 
Nikikumbuka siku nakuchukua hospitali, madaktari wakisema urudi tu nyumbani hamna namna...ugonjwa(cancer) umeenea mwili mzima, ukibaki hospitali gharama zitaongezeka...Nililia sana, nawe ulilia sana....ukiniambia, "mwanangu God Heals, madokta wameshajua hali ni mbaya...sina mda wa kuendelea kuishi. Umenipambania tangu siku ya kwanza miaka 5 iliyopita....leo imefikia." Uliongea kwa uchungu sana...tukarudi nyumbani....ukanisihi mengi sana, ukanikumbusha mengi sana, na ukaniomba niendelee kuwapenda wadogo zangu.

Ukanitania....ukilazimisha furaha, "mwanangu God Heals naondoka bila kumwona mjukuu wangu...ningependa sana kumbeba mme au mke mwenzangu, ila naondoka bila kumwona mjukuu..." Tukacheka huku mioyo ikiuma sana. Lilikuwa tabasamu la mwisho....

Nakumbuka kesho ukaomba nimpigie dada aje nyumbani, aje na mjukuu wako....kweli nilifanya hivyo...nao wakafika.... Tukaongea tukiwa na hudhuni sana... ukawa unajitahidi kutabasamu huku ukilalamika moyo unakuuma, mara mbavu, mara miguu, mara kichwa, mara mikono.... Ukatuangalia wote, kila mmoja kwa wakati wake... Ukiwa mbele ya mumeo kipenzi, watoto wako watatu, mjukuu wako mmoja, ukaanguka chini... ukajilaza... na hukufumbua macho tena.

Ni miaka 6 sasa imepita, Pumzika kwa amani mama, pumzika salama...katika siku hii sina pa kushika kila nikikumbuka maneno yako, na wakati ule mgumu, wa mwisho pale hospitali. Tutakumbuka kwa nasaha zako. Hakika ulikuwa mwema kwetu.
Lala salama mama yetu kipenzi.
Daah!!so sorry, R.i.p mama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka mwaka 2017 April naenda ripoti kazini (First appointment)na ww unaenda Ocean road kupata matibabu ya mionzi ukiwa na mzee , Baada ya siku kama mbili mzee akarudi kazini Mwanza akakuacha uendelee na matibabu chini ya uangalizi wa mdgo angu, Baada ya siku kadhaa ulipatwa na maumivu makali sana ya kichwa ambayo hukuwahi yapata maishani hvo ukashindwa hata kutumia simu na ukawa unazirai, then after miguu nayo ikashindwa kufanya kazi ukawa mtu wa kubebwa hapo ndipo mzee ilimbidi akimbie fasta hosptalini kukuuguza , ilifikia kipindi madaktari waka conclude kuwa umekufa baada ya kuzimia kwa muda mrefu na taratibu za kukupeleka monchwari zilikuwa zimeshaanza ndipo mzee ikabidi akucheki vizur but ulionesha dalili za uhai ikawa case kubwa sana kwa yule daktari aliye andika repoti ya kifo chako maana baada ya muda ulizinduka na hali ikaendelea, But finally madaktari walitushaur turudi nyumbani tu ukafie huko maana Cancer ilikuwa imeshasambaa ndipo tukapata Msamaria mwema akatupa gari na akajaza mafuta tayar kwa safar ya mwanza, ulifika nyumbani ukiwa mwenye tabasamu sana japo hukuweza kuongea vzur ulikaa takribani week moja ndipo umauti ulikufika mapema siku ya ijumaa saa saba mchana.Daah!!so sad yan mama amenipambania toka utotoni mimi napata kazi na wewe anafariki yani hakupata hata sh.kumi kutoka kwenye mshahara wangu.Daaah!!pumzika kwa amani mama angu kipenz cha watu
R.i.p Suzanne.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
R.I.P mama mwaka 2000 namaliza olevel ndio tunaonana toka miaka ya 90s! ulilia sana mama maana miaka 10 hatukuonana hapo dada yangu kipenzi alishatangulia mbele za haki.

Ukaniuliza vp mama yako wa kambo hakutesi? maana sina baba mwingine zaidi yako! ohoooo thanks God mama wa kambo alikuwa mzuri ananijari kuliko mshua maana sio kwa bakora za father.

Majibu yakatoka niko vyema tukaagana nakumbuka yulipishana mambo mengi sana tulilia kwa pamoja na kufatijiana.

Nisamehe mama nakumiss sana japo sijawahi wala kiexperience malezi yako,una wajukuu wa 3 sasa toka kwangu achiilia mbali dada zangu kwa wajukuu zako.

Tar 13/03/2010 ulinitoka mama niko dar we mkoani nikashindwa kukuzika ila nililia sana kwenye kaburi lako.

maana toka 2000 mapaka 2010 mauti yako sijakuona mama yangu.

Imekuwa kiumbe nadra sana ktk maisha yangu.

R.I.P mama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pumzika kwa amani mama, uliniacha nikiwa na miaka 20, sasa hivi nina watoto, natamani ungekuwepo walau wakuite bibi, natamani ungekuwepo unione vile nafuata uliyonifunza katika maisha....
Ulikuwa rafiki yangu, nakumbuka nilipokuwa nasoma O-level shule ya day, mimi ndio nilikuwa nakaa na pesa zako za biashara, weekend unanituma nikafunge mzigo.
Nilipokuwa A level, nikirudi home unaniambia biashara imekuingizia kiasi gani kwa kipindi nilipokuwa shule. Baada ya kumaliza form 6 ukanikabidhi biashara niwe msimamizi, Tulifanya kazi kwa bidii mpaka naenda chuo nilikuwa na pesa nyingi kwenye account. Sasa hivi ndio nimegundua kumbe ulikuwa unanifundisha kuwa independent...malezi yako yamenifanya kuwa strong! I will be a good mom to my kids also, i loove youuu ...
Uwiiii machozi yananitoka.
Pole mkuu
 
Mama ni mama tu.
Katika mabaya kumi sidhani Kama hakuna jema hata moja alilowahi kukufanyia.
Jifunze kumthamini mama yako..kuna watu wanatamani wangekuwa naye Hata huyo unayemuona hafai.
Siku ukimpoteza hutaongea haya unayoyaongea.
Thamani ya kitu huonekana kikitoweka.
Jifunze kuona thamani ya kitu kingali kipo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mmmmh!! Humjui mamangu wala familia yangu. Huijui abuse wewe wala huijui traumatic experience, hujakulia kwenye toxic family inayoleta matatizo ya kisaiklojia. Huijui Post traumatic disorder wala depression wewe. Huwezi kuelewa.
 
Samahani Kama nitakuwa nimekukwaza.
Ila jitahidi kumpenda mama yako hivyohivyo,,ndio huyohuyo uliyenaye.

Kuna muda wazazi wanaweza kutukwaza Sana lakini huna budi kusamehe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom