Wale ambao Mama zetu wametangulia mbele ya haki

God Heals

JF-Expert Member
Aug 7, 2015
687
1,000
Nikikumbuka siku nakuchukua hospitali, madaktari wakisema urudi tu nyumbani hamna namna...ugonjwa(cancer) umeenea mwili mzima, ukibaki hospitali gharama zitaongezeka...Nililia sana, nawe ulilia sana....ukiniambia, "mwanangu God Heals, madokta wameshajua hali ni mbaya...sina mda wa kuendelea kuishi. Umenipambania tangu siku ya kwanza miaka 5 iliyopita....leo imefikia." Uliongea kwa uchungu sana...tukarudi nyumbani....ukanisihi mengi sana, ukanikumbusha mengi sana, na ukaniomba niendelee kuwapenda wadogo zangu.

Ukanitania....ukilazimisha furaha, "mwanangu God Heals naondoka bila kumwona mjukuu wangu...ningependa sana kumbeba mme au mke mwenzangu, ila naondoka bila kumwona mjukuu..." Tukacheka huku mioyo ikiuma sana. Lilikuwa tabasamu la mwisho....

Nakumbuka kesho ukaomba nimpigie dada aje nyumbani, aje na mjukuu wako....kweli nilifanya hivyo...nao wakafika.... Tukaongea tukiwa na hudhuni sana... ukawa unajitahidi kutabasamu huku ukilalamika moyo unakuuma, mara mbavu, mara miguu, mara kichwa, mara mikono.... Ukatuangalia wote, kila mmoja kwa wakati wake... Ukiwa mbele ya mumeo kipenzi, watoto wako watatu, mjukuu wako mmoja, ukaanguka chini... ukajilaza... na hukufumbua macho tena.

Ni miaka 6 sasa imepita, Pumzika kwa amani mama, pumzika salama...katika siku hii sina pa kushika kila nikikumbuka maneno yako, na wakati ule mgumu, wa mwisho pale hospitali. Tutakumbuka kwa nasaha zako. Hakika ulikuwa mwema kwetu.
Lala salama mama yetu kipenzi.
 
KITAULO

JF-Expert Member
Apr 27, 2018
1,566
2,000

POLE SANA NDUGU...SHE IS WATCHING YOU OVER wherever she is
 
red apple

JF-Expert Member
Dec 6, 2012
508
1,000
Pumzika kwa amani mama, uliniacha nikiwa na miaka 20, sasa hivi nina watoto, natamani ungekuwepo walau wakuite bibi, natamani ungekuwepo unione vile nafuata uliyonifunza katika maisha....
Ulikuwa rafiki yangu, nakumbuka nilipokuwa nasoma O-level shule ya day, mimi ndio nilikuwa nakaa na pesa zako za biashara, weekend unanituma nikafunge mzigo.
Nilipokuwa A level, nikirudi home unaniambia biashara imekuingizia kiasi gani kwa kipindi nilipokuwa shule. Baada ya kumaliza form 6 ukanikabidhi biashara niwe msimamizi, Tulifanya kazi kwa bidii mpaka naenda chuo nilikuwa na pesa nyingi kwenye account. Sasa hivi ndio nimegundua kumbe ulikuwa unanifundisha kuwa independent...malezi yako yamenifanya kuwa strong! I will be a good mom to my kids also, i loove youuu ...
Uwiiii machozi yananitoka.
 
red apple

JF-Expert Member
Dec 6, 2012
508
1,000
Nikikumbuka siku nakuchukua hospitali, madaktari wakisema urudi tu nyumbani hamna namna...ugonjwa(cancer) umeenea mwili mzima, ukibaki hospitali gharama zitaongezeka...Nililia sana, nawe ulilia sana....ukiniambia, "mwanangu God Heals, madokta wameshajua hali ni mbaya...sina mda wa kuendelea kuishi. Umenipambania tangu siku ya kwanza miaka 5 iliyopita....leo imefikia." Uliongea kwa uchungu sana...tukarudi nyumbani....ukanisihi mengi sana, ukanikumbusha mengi sana, na ukaniomba niendelee kuwapenda wadogo zangu.

Ukanitania....ukilazimisha furaha, "mwanangu God Heals naondoka bila kumwona mjukuu wangu...ningependa sana kumbeba mme au mke mwenzangu, ila naondoka bila kumwona mjukuu..." Tukacheka huku mioyo ikiuma sana. Lilikuwa tabasamu la mwisho....

Nakumbuka kesho ukaomba nimpigie dada aje nyumbani, aje na mjukuu wako....kweli nilifanya hivyo...nao wakafika.... Tukaongea tukiwa na hudhuni sana... ukawa unajitahidi kutabasamu huku ukilalamika moyo unakuuma, mara mbavu, mara miguu, mara kichwa, mara mikono.... Ukatuangalia wote, kila mmoja kwa wakati wake... Ukiwa mbele ya mumeo kipenzi, watoto wako watatu, mjukuu wako mmoja, ukaanguka chini... ukajilaza... na hukufumbua macho tena.

Ni miaka 6 sasa imepita, Pumzika kwa amani mama, pumzika salama...katika siku hii sina pa kushika kila nikikumbuka maneno yako, na wakati ule mgumu, wa mwisho pale hospitali. Tutakumbuka kwa nasaha zako. Hakika ulikuwa mwema kwetu.
Lala salama mama yetu kipenzi.
Daaah pole sana ndugu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom