Walaji wa nguruwe wapewa tahadhari kutokana na uwepo wa minyoo hatari inayoleta kifafa cha binadamu

“Nguruwe msimle; ana kwato zilizogawanyika lakini hacheui; kwenu ni najisi. Kwa sababu wanyama hao ni najisi msile nyama yao wala msiguse mizoga yao” (Walawi 11: 7 – 8).
 
Mwenyezi mungu kila kitu alichokiharimisha lazima kiwe na madhara kwa mfano pombe,uzinzi,nguruwe nk
 
kifo hakina huruma, tuache hofu tule maisha sababu kuna watu hata coca cola wanadai ina madhara tusinywe.
tule nguruwe sababu wengi hatutakufa sababu ya nguruwe, ila kisukari, h.i.v, ini, ajali mbalimbali ikiwemo kuuawa baada kufumaniwa, sonona.
 
Wivu wa kiserikali ili watu wale nyama za wanyama wengine maana kitimoto kwenye mabucha yakulipa kodi hakipo na serikali ishagundua ni nyama inayoliwa sana hivyo wanataka kutisha watu.
Nani alishapelekwa hospital ikadhibitika kweli ana matatizo yaliyotokana na ulaji wa kitimoto
Licha ya hivyo kama ni kweli basi asilimia kubwa ya watanzania tungekuwa na kifafa
 
Wakuu unajua dunia kweli ipo fea sana hawa bandugu wanasema mara nguruwe wana minyoo, mara oh tusile hiki kina virus sasa cha ajabu uyu jamaa kitimoto tangu miaka iyo wazee wetu wanakula na cha ajabu sasa watu wala hawadanji, utashangaa watu wanakufa na kisukar, presha mara kansa.
 
Wizara ya Afya imewatahadharisha walaji wa nyama ya nguruwe juu ya uwepo wa minyoo aina ya tegu ambayo husababisha kifafa kwa binadamu, na kuwa hatari kubwa ipo kwa wanaokula nyama au mboga ambazo hazijapikwa vizuri. Serikali imesema inaendelea na utafiti wa namna ya kuizuia. View attachment 1274055
Hii machinjio iko wapi maana niko kwenye maandalizi ya kuanza mradi wa kufuga hii kitu
 
MINYOO aina ya tegu inayotoka kwenye nyama ya nguruwe (cysticercodis) imedaiwa kuwa tishio kwa walaji wa nyama hiyo na kusababisha kifafa kwa binadamu.
ed11969a359cebc33e8c32bf3e769648

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile, alitoa tahadhari hiyo wakati akifungua mkutano wa kwanza wa kimataifa jana wa kujadili minyoo ya tegu wa nguruwe, jijini hapa.

Dk. Ndugulile, alisema serikali haijapata chanjo ya kumzuia mnyoo huyo wa nguruwe na ipo katika utafiti wakuangalia namna ya kumdhibiti.

Alisema walaji wa nguruwe wafahamu kuwa kuna minyoo inayopatikana kwenye nyama hiyo kupitia mayai na inaweza kumuathiri binadamu endapo atakula nyama isiyopikwa vizuri na mboga ambazo hazijaoshwa na kupikwa vizuri.

Dk. Ndugulile alisema athari zinazotokana na kula nyama hiyo ni kubwa ikiwamo kupata ugonjwa wa kifafa, tatizo ambalo limeshaingia nchini na limeanza kuathiri zaidi mikoa ya Manyara, Njombe, Mbeya, Sogwe na Arusha, huku asilimia 16 ya wananchi wanaoishi mikoa hiyo wakiathirika kwa ugonjwa huo.

"Jinsi ya kutokomeza ugonjwa huu wa minyoo wa tegu wa nguruwe, ni wafugaji kufuga kisasa na kuacha wanyama wao kuzurura ovyo kwa sababu huacha kinyesi chenye mnyoo huyo katika mboga,” alisema.

Pia, aliwataka wafugaji kupata ushauri kitalaamu wa mifugo na wachinjaji wasichinje bila kizingatia utaalamu unaosimamia wanyama hao.
Aliwataka wanaokula nyama hiyo kuhakikisha inapikwa vizuri na kuiva.

Hata hivyo, alisema wafugaji wanaweza kuzuia kwa mifugo yao kuzagaa na kupima mnyama kabla ya kuchinja.

Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya magonjwa ya binadamu (NIMR), Prof. Yunus Mgaya, alisema wanatekeleza mradi huo kwa kukusanya taarifa za mnyoo huyo mbaye anapatikana kwa kula mboga zilizobeba mayai yaliotokana na vinyesi vya nguruwe au kinyesi cha binadamu.

"Mradi huu unatekelezwa na nchi zingine mbili Afrika Msumbiji na Zambia na tunashirikiana na wadau wetu wa utafiti wa Ujerumani kutoka Chuo Kikuu cha Munchen,” alisema.

Kaimu Mkuu wa idara ya tiba ya mifugo na afya ya jamii ambaye pia ni Mkurugenzi wa mtandao wa utafiti wa kisayansi Prof. Helena Ngowi, alisema mnyoo huyo ni hatari kwa sababu anaweza kuleta adhari katika utumbo na ubongo wa binadamu.
Tenia Saginata anapatikana kwenye ngo'mbe. Tenia Solium anapatikana kwenye nguruwe. Teniasis disease zote madhara na kuambukiza ni sawa. Tofauti spices za parasites hupatikana kwenye ngo'mbe na nyingine nguruwe.
 
Wivu wa kiserikali ili watu wale nyama za wanyama wengine maana kitimoto kwenye mabucha yakulipa kodi hakipo na serikali ishagundua ni nyama inayoliwa sana hivyo wanataka kutisha watu.
Nani alishapelekwa hospital ikadhibitika kweli ana matatizo yaliyotokana na ulaji wa kitimoto
Huyo Dr. Yusus Mgaya ni Muislam mwenye kuwashwa washwa.
 
Mkuu hao cysticercodis unaweza kuwapata hata kwa Kula mboga za majani hasa hizi zinazomwagiliwa maji yasiyoeleweka kwa hiyo sio nyama ya nguruwe pekee.
 
Mgalatia utamwambia nini kuhusu mbuzi katoliki akuelewe?
Sasa hivi watasema muanzisha uzi lzm awe Muislamu.
Yaani km ukimwi ungewekwa kwenye kiti moto leo watu wangeenda kuzikiwa Bagamoyo manake makaburi mjini yangekuwa fulu fulu.

Teh teh teh.
 
“Nguruwe msimle; ana kwato zilizogawanyika lakini hacheui; kwenu ni najisi. Kwa sababu wanyama hao ni najisi msile nyama yao wala msiguse mizoga yao” (Walawi 11: 7 – 8).
Bibie mbona nyie mnabugia nyama ya ngamia na sisi hatusemi? Biblia imeharamisha nyama ya ngamia kabla ya nguruwe.
 
Back
Top Bottom