Katika kitabu cha Mambo ya Walawi 11 ndipo utaona katazo la vitu vinavyopaswa kuliwa. (Hili ni agano la kale)
Baada ya kifo cha Yesu na ufufuko wake sheria nyingi za agano la kale ama zilibadilishwa au kufutwa.
Moja wapo ya sheria hizo ni hii ya kula nguruwe.
Na badiliko hili unalipata katika kitabu cha Matendo ya Mitume 10:9-15 (agano jipya)
"..... 12. Ambayo ndani yake walikuwamo aina zote za wanyama wenye miguu minne, na hao watambaao, na ndege wa angani. 13. Kisha sauti ikamjia kusema, ondoka Petro, uchinje ule. 14.Lakini Petro akasema, hasha, Bwana, kwa maana sijakula kamwe kitu kilicho kichafu au najisi. 15. Sauti ikamjia mara ya pili ikimwambia, Vilivyotakaswa na Mungu, usiviite wewe najisi."