kijana mkimya
JF-Expert Member
- Sep 10, 2015
- 277
- 121
Wakuu nimempa mimba mtoto wa watu. kutokana nampenda sana huyu binti nikaona isiwe tabu nifanye process za kufunga nae pingu za maisha japo ilikuwa ngumu kwa wazazi wake kukubali moja kwa moja lakini tumeelewana na wakanitoza faini.
Tumekubaliana akijifungua salama tutafunga ndoa Mungu akipenda, kitu ambacho kinanichanganya hawa wazazi wa mke wangu mtarajiwa. wanasema mtoto akizaliwa hawezi kutumia jina langu kama baba yake inabidi atumie ukoo wa mama yake!! kwasababu mtoto tumemzaa kabla ya kufunga ndoa, mtoto wa zinaa.
Haya mambo hawajaniambia mwenyewe , wamemfikishia binti yao aniambie.
Wakuu, je hii ni sahihi hata kama baba wa mtoto amekubali kosa na kuamua kufunga ndoa? sielewi hii familia ina nia gani au ina lengo gani.
Nafahamu dini inasema hivyo lakini nimekubali kumuoa binti yao. Sielewi tatizo linatoka wapi hapa? wakuu wanaofahamu haya mambo naomba wanidadavulie kifasihi zaidi.