Wakuu, waziri Sitta ananichanganya kuhusu Richmond. Ukweli ni upi?

Anaanza: anasema umuja wa ea ulipita ulikuwa ni wa viongozi ndiyo maana uliweza kufa, tofauti na umoja huu unajumisha watu na maamuzi yanaanzia chini kwenda juu. Kuhusu soko la pamoja amesema litarahisisha watu kupata huduma na bidhaa, ushuru wa pamoja, urahisi wa mipaka kuingia kwenye nchi husika bila vikwazo katika nyanja ya elimu ya juu na ajira.
 
Ameanza kwa kutofautisha jumuiya ya sasa na ile ya miaka ya sabini. Kwa ufupi anasemaaa, Jumuiya ile ilijikita kwa viongozi zaidi na siyo wananchi. Safari hii tunajikita kwa wananchi zaidi na ukiona sector binafsi zimeshirikishwa zaidi mf ni Kampala university. Hili ni upande wa soko la pamoja. Matangazo yanakatakata sana, lakini tuko pamoja...
 
Mapungu ya kuwashirikisha watu amesema serekali imetoa bilion moja kutoa elimu.
 
Anaweka bayana kuhusu swala la ardhi katika jumuiya. Ardhi itamilikiwa kwa sheria za nchi husika hii imeondoa wasiwasi wa watanzania kuhusu ardhi...
 
Suala la aridhi halipo kwenye juiya.
Ukizingatia tanz tuna ardhi nzuri zaidi ya nchi nyingine.
Kuhusu Sudan kuonyesha nia ya kujiunga na jumuiya amesema moja ya sharti la kuingia ni lazima tuwe tumepakana na nchi inayomba.
 
Jeshi la pamoja. Majeshi wanafanya mazoezi pamoja lakn bado hatujawa na jeshi moja amesema sitta.
 
Jibu rahisi ni kua Baba Mswahili na Mama Mswahili hawawezi kuzaa Mtoto Mzungu.
Yaani Richmond ya Kitapeli (kwa mujibu wa bunge)
haiwezi kuzaa Dowans ya Kihalali.
Ni sawasawa uuze mali ya wizi halafu kwenye mauziano mkaandikiane kwa mwanasheria, hiyo haiwezi kuja.
 
Mimi sioni anachoongea huyu Mzee, nadhani anachelewesha uhondo wa malipo ya Dowans...ila kabla hajapumzika awachinjie baharini mafisadi

Hivi vipi hili Gwiji likiamua kuvuta fomu ya Urais, Magamba si yatapeta kiulaini?


Wacha tumsikie mzee wa mikakati atasemaje leo!
 
Ni wakati gani ulipata wakati mgumu ukiwa spika? Jibu:- Ni wakati waziri mkuu anajiuzuru
 
Anasema siku ambayo anaikumbuka ni siku El alijiuzulu, anasema hakutegema kujiuzulu kwa El,
 
Anasema alilelewa na baba yake mkristo na mama muislam washika dini amefunzwa kutokuwa mnafki, mafisadi wanajulikana wezi wa EPA, anasema ukitazama umaskini wa watanzania ukishikilia sana hii sheria ya utawala bora na haki za binadamu utajikuta wakubwa hawashikiki kwenye ubadhilifu zaidi ya wanyonge hasa wezi wadogo.
 
Mafisadi wapo na wanajulikana hata kwa matendo tu. Pesa commodity import support toka Japan zimeliwa na mafisadi na wameharibu nyarka kule hazina. Rule of law kwa nchi maskini inaweza ikachukua sura ya kulinda mafisadi. Tumsaidie Rais wetu- Sitta.
 
Anasema dowans ni wahuni wasiostahili kulipwa ukiwemo wewe kama wanakuhusu hao Dowans!
 
Kuhusu Dowans msimamo hakuna haki kuwalipa wahuni dowans.
Richmund ilipatikana kwa kuvunja sheria kwani walioamua zabuni walipaswa kuwa tanesco na siyo wengine, timu iliyoundwa na serikali alipunguza vigezo vya zabuni toka 24 mpaka 4 ambapo navyo Richimund alishindwa. Mkata ulikuwa wa miezi 12 waziri akafanya kwa kihuni miez 24 tukawalipa hela na faida juu.
 
Kheee, baraza la mawaziri- mkataba miezi 12, waziri aliyejiuzuru miezi 24 yote kuhusu richmond. Kamgusia ali hadaiwi yule afandeeee...
 
Back
Top Bottom