Wakuu wa Mikoa/Wilaya Kuweka watu ndani: Mahakama Kuu yatupilia mbali mapingamizi ya Serikali

Mhhhhhh, hako ka sheria kanapendwa na wengi kweli, ukiona adui yako kapewa rungu na upo chini ya himaya yako jisepee mapemaaaaa
 
Kwa hisani ya watu wa marekani
unnamed.jpg
 
Huyo wakili msomi Petiro sijui Petro kaishiwa bando au tatizo ni hii lugha iliyokuja na mashua ndio umemtoa nduki? Hebu Petro E. Mselewa uje uvunje vunje makali ya hii lugha buana
 
Ruling ni kuwa kwa vile shauri hili linagusa suala LA kikatiba litapelekwa katika panel ya majaji watatu ambao watakuwa na uwezo Wa kufutilia mbali au kubadili kipengele hicho. Jambo hilo ndio lilikuwa limewekewa pingamizi na mlalamikiwa yaani AG
 
Hii inamaanisha nini labda msomi nguli Petro E. Mselewa atuambie

Tofasiri isiyo rasmi...


IN THE HIGH COURT OF TANZANIA

AT DAR ES SALAM MAIN REGISTRY

MISC. CIVIL. CAUSE NO. 27 OF 2017

JEBRA KAMBOLE………………………………………………………….APPLICANT
VERSUS
THE ATTORNEY GENERAL…………………………………………….RESPONDENT

Tarehe ya Hukumu 15/8/2018
HUKUMU

TEEMBA, J

Mwombaji ameleta maombi haya chini ya kifungu cha 26 (2) na 30 (3) & (4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977; Sehemu ya 4, 5 & 8 ya Sheria ya Utekelezaji wa Haki za Msingi na Wajibu, (of the Basis Rights and Duties Enforcement Act, Cap 3 [RE 2002; na Sheria ya 4 ya Sheria za Utekelezaji wa Haki za Msingi na Kazi (2014) [GN.No.304 ya 2014].Mwombaji katika shauri hili anapinga uhalali wa kikatiba wa kifungu cha 7 na 15 cha Sheria ya tawala za Mikoa, (Regional Administration Act, Cap 97 [RE 2002) na anataka mahakama hii itoe tamko kwamba vifungu hivyo vya sharia ni batili na vinakinzana na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Upande wa pili wa Jamhuri, walipinga shauri hilo kwa hoja kwamba maombi hayo hayana sifa na vigezo. Upande wa jamhuri, walitoa taarifa ya awali ya kupinga maombi haya ambayo ndo chanzo na sababu ya hukumu hii.
Kwa misingi ya mamlaka ya hapo juu, ni maoni yangu kwamba hoja iliopo haiingii chini ya ufafanuzi huo. Hivyo basi nakubaliana na uwasilishaji wa mleta maombi kwamba ombi hilo ni dutu na lina msingi wa kisheria. Kwa hiyo ni maombi sahihi mbele ya mahakama hii.
Mwisho na kwa kumalizia, mapingamizi matatu (03) juu ya hatua za kisheria kama yalivyowasilishwa upande wa serikali hayana mashiko na hivyo basi yanatupiliwa mbali. Gharama zilipwe na upande wa utetezi.


Imeamliwa na:-

R.A.TEEMBA, J

15/8/2018
 
Mkuu, katika kizazi hiki na kijacho..hatatokea Mwalusanya Mwingine as Judicial judge or magistrate whatsoever. Kizazi kile cha dhahabu cha Justice Lugakingira, Mwalusanya and Samatha hakitatokea tena. Not now, not ever!
na kweli! Hao ni tunu hazitatokea tena! Kama ndio akina Kabudi, ndio wataalamu wa sheria, basi THE DOOMED JUDICIARY! MWALUSANYA, KATITI, LUGAKINGIRA, MROSO, SAMATHA
 
Kwetu Mbeya tumepelekewa RC mwehu jamani!
Sielewi how mtu kama Chalamila anakuwa RC
Ni kichaa huyu jamaa
Kaamuru kijiji kizima kiwekwe mahabusu na kweli Polisi wanafika kijijini wanakamata watu wote wanawaweka mahabusu
Ndiyo tulipofikia?
 
na kweli! Hao ni tunu hazitatokea tena! Kama ndio akina Kabudi, ndio wataalamu wa sheria, basi THE DOOMED JUDICIARY! MWALUSANYA, KATITI, LUGAKINGIRA, MROSO, SAMATHA
na kweli! Hao ni tunu hazitatokea tena! Kama ndio akina Kabudi, ndio wataalamu wa sheria, basi THE DOOMED JUDICIARY! MWALUSANYA, KATITI, LUGAKINGIRA, MROSO, SAMATHA
Uko sahihi. Nashangaa wanaomtukuza kabudi.
 
Back
Top Bottom