Wakuu tupunguze ubinafsi

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,453
40,442
Binadamu wanachangamoto nyingi katika maisha, mtu anaweza kupambana katika maisha yake mwanzo mwisho bila kupata ushirikiano kutoka kwa ndugu zake au ukoo anaotoka. Wanaweza kuwepo waliofanikiwa, lakini wanakuwa hawako tayari kuwasaidia ndugu wengine waweze kufanikiwa.

Kwa waliopo mijini, unaweza kuona mtu anamafanikio makubwa na inapotokea yeye kufariki na kurejeshwa kwao kwa maziko, unakuta yeye alivyokuwa akiishi ni tofauti na ndugu zake wengine. Unakuta ndugu zake wamechokachoka wana afya dhaifu kutokana na umasikini.

Kuthibitisha hili fanya utafiti mdogo, nenda kwenye misiba ya watu waliofanikiwa......ukiona walioshiba na afya njema jua hao ni marafiki, na ukiona watu waliochokachoka jua hao ni ndugu.

Wakuu tupunguze ubinafsi.
 
Ni kweli, kuna baadhi ya watu wamejaaliwa kipato lakini ni wazito kuwasaidia ndugu zao, sijui mtu anaonaje kumsaidia ndugu yake?
Badala yake anawasaidia watu baki na kuwaacha ndugu zake.

Na msaada sio lazima kumpa pesa, bali unaweza kutafutia nafasi nzuri na yeye akatafuta riziki yake.

Na huu ndio msaada bora.
 
Nadhani watakuwa na ubinafsi uliopitiliza
 
Haujui history za watu ndugu.... hao unaowaona wamechoka yawezekana hawakutaka au walipendwa sana na wazazi, wakaacha shule, hawakutaka kazi, wakabweteka, wengi nao ukikaa nao karibu mnalost nyote kwa pamoja ndio maana wengi huwaacha wakizaliana na baadae wanatia huruma wakati ukweli wa mambo wanaujua. Waafrica tunamatatizo mengi sana.... uzazi wa mpango hatutaki, kazi hatutaki, uchawi sisi na majjngu juu.
Wengi wa hao waliochoka wanastahili.
Tuache kuwashutumu waliofanikiwa kwani ni matunda ya jitihada zao katika maisha...... huwa nawakubali sana matajiri maana wananipa uchu wa kupata changu.
SIKUUMWA KULALAMIKA, NAPAMBANA NA HALI YANGU.
NB: MASIKINI WENGI WAJEURI
 
ha ha ha ha lakini ni kwa nini inakuwa hivi
 
Nadhani pia,ili kuondoa lawama ni bora umuwezeshe akiharibu ndio liwe funzo kwake.
 
Nacho wapendea wajaluo hata Kama ndugu zake wanamteta kiasi gani akipata mali lazima awakumbuke hata kuwajengea nyumba nzuri za kuishi wengine unafiki tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…