Nataka kuwekeza kwenye Ujenzi, naomba ushauri

TUKANA UONE

JF-Expert Member
Jan 3, 2018
1,816
5,151
Ukihitaji salamu rudi kijijini kwenu, kwangu utaambulia chuya ukalishie kuku!

Wakuu nimekuja kwenu nahitaji ushauri wa kitaalamu na kitaaluma kutoka kwenu,natambua ya ksmaba humu jukwaani wapo wadau ambao sekta ya ujenzi wamesomea na wanaifahamu kinagaubaga.

Mimi kama mbangaizaji na mganganjaa wa mtaani natamani nijishikize kwenye biashara ya ujenzi!.

Kuna pesa ninayo na nyingine natarajia kuipata hivi karibuni,sasa nikaonelea biashara nzuri ya kufanya ni kumiliki mitambo ya ujenzi ili iniingizie faida hata kama ikiwa kidogo lakini itakuwa bora kuliko kuweka hela benki wakazitumia wao kujenereti faida bure!

Pesa niliyonayo na ambayo natarajia kuipata nahitaji kununua mitambo ifuatayo ili inisaidie kwenye biashara zangu.

1.Excavators - 2

CM20180212-41328-33143.jpeg


2.Bulldozer - 1
Bulldozer.jpg


3.Graders - 2


images (1).jpeg


4.Loaders - 1


images (2).jpeg


5.Compactors - 1


images (3).jpeg


6.Water Bowser - 1



images (4).jpeg


7.Heavy Duty Sino Truck - 3


images (5).jpeg




Nahitaji kufanya yafuatayo:-

1.Kuvikodisha kwa makampumi mbalimbali ya Ujenzi ili niwe najipatia faida.

2.Kuanzisha kampuni ya Ujenzi ambayo nitaajiri wasomi na wataalamu wenye ujuzi wa mambo ya ujenzi wa mabarabara na nitakuwa nawalipa kulingana na tenda tutakayokuwa tunapata.

Wakuu nahitaji ushauri kutoka kwenu

Je,Nitatupa tu hela hakuna faida?

Je,niingie hivyo hivyo kichwa kichwa nitajua hukohuko?

Je,nitafute wataalamu wa mambo ya ujenzi ili tukae chini tuyajenge tuone faida itapatikanaje ili tugawane?

Au nitatupa tu pesa?

Nahitaji kuajiri wabongo wenzangu kadiri iwezekanavyo ili tugawane hiki kidogo tupewacho na Mola wetu.


Ushauri wako ni muhimu sana mkuu!.
 

Attachments

  • CM20180212-41328-33143.jpeg
    CM20180212-41328-33143.jpeg
    31.6 KB · Views: 3
Back
Top Bottom