Wakuu, nitumie mbinu gani hichi kikombe cha majukumu kinikimbie?

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,453
40,446
Kuna mchepuko wangu wa zamani (shepu matata) alinipigia simu mwezi uliopita, na kunijulisha nimpokee rafiki yake anakuja mkoa niliopo kwa ajili ya kushughulikia mambo yake.

Ingawa alinisii, nisimsaliti kwa sababu huyo rafiki yake ni pisi kali; mi nikamwambia haina shida, mi sina madhara kwa mashemeji , mpe tu namba yangu nitampokea.

Kweli baada ya dakika chache, nikapokea simu kutoka kwa shemeji na kunijulisha ataingia muda wa usiku kutokana na umbali wa huko anakotoka.

Imefika saa tano usiku, akanijulisha alishafika stendi; ikabidi niende kumpokea, nikamjulisha jinsi nilivyo n.k kwa sababu tulikuwa hatufahamiani; wakati anatoka kwenye geti la kutokea stendi, nikamuona mrembo ananifuata moja kwa moja, alikuwa amevalia full jinsi juu mpaka chini.

Kutokana na muonekano wake, nikasema huyu nisimpeleke home kwanza, ngoja nimpeleke kiwanja fulani chenye 'vibe' apige msosi; wakati anapiga msosi mimi napiga bia yangu taratibu huku tukibadilishana mawazo na kufahamiana zaidi.

Baada ya kumaliza kula, ikabidi nimbadilishie kiwanja kingine ambacho mle ndani kuna warembo wa kila aina wanaotikisa vyura vyao.

Tukaagiza vinywaji, yeye akaagiza bia moja akihofia labda akilewa nitamrarua. Nilipoona huyu sio mnywaji, tukatumia dakika chache tukarudi nyumbani.

Nikamuelekeza chumba cha kulala cha wageni, lakini roho yangu ikawa inaniuma, kwa nini anionyeshi ishara ya kunitamani? Wakati amejifunika shuka,nikamfuata na kushika shika baadhi ya sehemu huku nikimuuliza uko sawa?

Akanijibu yuko sawa, na hayuko tayari kumsaliti rafiki yake; mi nikamuuliza kwani alama itabaki?, akakataa kabisa.

Basi mimi nikaondoka na kurudi chumbani kwangu na kulala, ilipofika asubuhi, akaamka mapema na kujiandaa na baadaye akaja kuniaga anaondoka kwenda kwenye mishe zake, huku akinishukuru kwa mapokezi mazuri.

Baada ya hapo tukawa hatuwasiliani tena; sasa leo naona namba mpya inanipigia kwenye simu (namba yake niliifuta tangu alipoondoka), nami huwa nakawaida ya kutokupokea namba mpya kwa haraka.

Baada ya kukata, nikamtumia ujumbe, habari? Akanijibu, salama tu mpenzi mimi ni hhh. Nilipatwa na mshtuko wa ghafla, imekuwaje tena ananiita mpenzi.

Ikabidi nimpigie, akapokea kwa sauti ya mahaba, na kuniambia siku ile niliyompokea, kuna vitu alivipenda kutoka kwangu, kwa hiyo anahitaji muda mwingi aongee na mimi.

Nikatafakari kidogo huku nikiangalia hili jua lilivyokuwa kali, si ajabu kuna mtu anapangwa hapa.

Nikamuuliza hayo mazungumzo yanahusu nini hasa, akasema yanahusu maisha tu; nimpatie nafasi na muda kesho aongee na mimi kwa sababu ana mambo mengi sana, yana koma, kituo, vifungua usemi n.k Mi nikamjibu karibu, na kumpatia muda wa mazungumzo.

Nikamuuliza kiutani, utakuja lini tena huku? akajibu wikiendi ijayo.

Kwa mazingira haya wakuu, naona na huyu naye anataka awe mchepuko wangu; na kumiliki michepuko ni gharama.

Wakuu, nitumie mbinu gani hichi kikombe cha majukumu kinikimbie?​
 
Wakuu, nitumie mbinu gani hichi kikombe cha majukumu kinikimbie?

Yj4.gif
 
Back
Top Bottom