Wakuu, nishaurini kuhusu Shule ya bweni kwa mtoto wa nursery

Ronee

Senior Member
Jun 1, 2018
156
155
Naimani afya zenu ni njema kabisa wakuu, kuhusu mengineyo inshallah Allah atafanya wepesi.

Wakuu 'junior' wangu sasa amefikia umri wa kuanza shule, changamoto inayonikabili ni kuhusu upatikanaji wa shule hizi za mchepuo wa kimombo ktk mazingira niliyopo kwa sasa, huduma hiyo hamna.

Hivyo basi nimeazimia 'junior' akapambane na maisha ya boarding ktk umri huo! Je, athari za kimalezi kwa kumpeleka mtoto mdogo boarding school ni kubwa kuliko faida kama inavyoelezwa na wengi? Ukweli ukoje?

Ikumbukwe sina option zaidi ya hiyo vinginevyo basi 'junior' achukue kidumu na mfagio avuke barabara jambo ambalo sijaliafiki.

Karibuni wakuu mnipe mawazo yenu kwa mliowahi kumbana na situation hii, pia wenye uzoefu mbalimbali. (huyu 'junior ni binti).
 
Kama unampeleka boarding hakikisha hiyo shule ina waalimu wa malezi ya watoto waliosomea na kubobea, hutojuta.

Akipata shule nzuri ya boarding ni bora kuliko akae nyumbani wakati wazazi wenyewe mnaondoka nyumbani saa 11 asubuhi na kurudi saa 5 za usiku.

Ni bora aende boarding atapata elimu bora na extra curricular activities kuliko kukaa nyumbani na house girl wakiangalia tamthilia za bongo movie.
 
Nashauri mtoto anatakiwa kwenda boarding kuanzia form 1, chekechea hadi anapomaliza darasa la 7 anahitaji malezi ya wazazi wake. Atapata wapi upendo wa wazazi kama tangu anaanza shule yeye yupo boarding?
Mkuu hoja hii ndio inayonidhoofisha, lakini ni kweli kwamba shule hizo za boarding hazina watoto, na je wote wamekuwa na tabia mbaya ama kupoteza 'bond'na wazazi wao?
 
Mkuu huku ni kumyima mtoto malezi angali bado mdogo na hili hupunguza ukaribu kati ya mzazi na mtoto.

Angalau angekuwa kidato cha Kwanza na kama kuna ulazima shule ya msingi basi yawe madarasa ya juu kuanzia darasa la 5 mpaka la 7.
 
Kama unampeleka boarding hakikisha hiyo shule ina waalimu wa malezi ya watoto waliosomea na kubobea, hutojuta.

Akipata shule nzuri ya boarding ni bora kuliko akae nyumbani wakati wazazi wenyewe mnaondoka nyumbani saa 11 asubuhi na kurudi saa 5 za usiku.

Ni bora aende boarding atapata elimu bora na extra curricular activities kuliko kukaa nyumbani na house girl wakiangalia tamthilia za bongo movie.
Mkuu una hoja ya msingi nitaitafakari zaidi, kimsingi nikiangalia hata tabia za watoto wa hizi shule za umma ambao wanashinda na wazazi bado zinasikitisha kbs!
 
Mi huwa nashangaaga sana wazazi kupata ujasiri kuwapeleka watoto zao wadogo shule za boarding.Kipindi cha utoto ndo kizuri kumjua mwanao na kuanza kumfundisha taratibu za kimaisha pamoja na kumgombeza akikosea.

Mtoto wako umesema ni wa kike,ebu fikilia kapata hedhi(period) yupo shule,anaweza kupata emotional support anayohitaji ambayo kama angekuwa nyumbani mama ake au hata wanawake wa family wangeweza kumsaidia, sasa unataka kazi hii ufanyiwe na wengine.

Mtoto wako atakosa home life, Bullying na abuse ni uwezekano, pia kuna hisia kuwa kawa abandoned na wazazi hizi huwasumbua wakiwa wakubwa.
 
Mkuu huku ni kumyima mtoto malezi angali bado mdogo na hili hupunguza ukaribu kati ya mzazi na mtoto.

Angalau angekuwa kidato cha Kwanza na kama kuna ulazima shule ya msingi basi yawe madarasa ya juu kuanzia darasa la 5 mpaka la 7.
Lipi ni jema sasa mkuu, apate elimu hii ya jua kali ili kulinda ukaribu wa mzazi na mtoto na malezi bora au aende akapate elimu itakayonjenga vizuri kuyakabili mazingira yake.
 
Narudia tena usimpeleke mtoto mdogo boarding, sijui kwanini wazazi tunakimbia majukumu yetu ya kuwa na watoto wetu tunaamua kuwapeleka boarding. Watoto boarding wanapitia maisha magumu, manyanayaso, mateso ambayo wewe kama mzazi hutokaa uyajue. Mtoto aende boarding walau sekondari au hata 5-6 akiwa ashajitambua.

Hivi jamani kuna haja gani ya kumeleka mtoto boarding wa Nursery, mtoto mdogo tu ambaye anahitaji kuwa karibu na wazazi.

Kama una pesa ya kumpeleka boarding basi unaweza kumpeleka Nursery ya kutwa maana pesa inaweza hata kuwa sawa au pungufu kwasababu ya schoolbus itachezea milion moja mpaka mbili kwa shule zetu hizi za kawaida ukitaka za kishua inaweza fika hata milion 3 - 4

Siku hizi dunia imebadilika kuwaachia walimu wakulelee mtoto 100% kwa mwaka eti unamuona mara 4 kwa muda mfupi mfupi utakuja jikuta una mtoto shoga bila wewe kujua kumbe kaanza haribiwa toka mdogo we hukuwa na taarifa.
 
Mtoto anahitaji mapenzi na malezi ya wazazi wake. Hakuna sababu yoyote ya kumpeleka huko akalelewe na watu wasio mhusu. At least angekuwa form one.
Mkuu hoja hii ndio inayonidhoofisha, lakini ni kweli kwamba shule hizo za boarding hazina watoto, na je wote wamekuwa na tabia mbaya ama kupoteza 'bond'na wazazi wao?
 
Mi huwa nashangaaga sana wazazi kupata ujasiri kuwapeleka watoto zao wadogo shule za boarding.Kipindi cha utoto ndo kizuri kumjua mwanao na kuanza kumfundisha taratibu za kimaisha pamoja na kumgombeza akikosea. Mtoto wako umesema ni wa kike,ebu fikilia kapata hedhi(period) yupo shule,anaweza kupata emotional support anayohitaji ambayo kama angekuwa nyumbani mama ake au hata wanawake wa family wangeweza kumsaidia, sasa unataka kazi hii ufanyiwe na wengine.Mtoto wako atakosa home life,Bullying na abuse ni uwezekano,pia kuna hisia kuwa kawa abandoned na wazazi hizi huwasumbua wakiwa wakubwa.
Mkuu hebu fikiria tatizo la kimazingira, wazazi ambao wanaishi mbali na huduma ya hizi shule tunazoamini zinatoa elimu bora, je watoto wao wasipate fursa kabisa ya kunufaika na elimu hiyo kwa sababu za kimalezi?
 
Kwa majibu yako hapo juu inaonekana tayari una solution basi tu kutuchora wananzengo. Peleka tu boarding si utalia wewe na mkeo sie washika vidumu na mifagio hayatuhusu
Mkuu numbisa ni kweli nilikuwa na fikra flani lkn kuomba ushauri ni muhimu ili tuweze kupima maamuzi yetu kupitia uzoefu wa wengine. Ninachokifanya ni kuangalia mizania kati ya hasara ya kimalezi na faida kwa mtoto.
 
Muache avuke barabara aende na kidumu shuleni. Unaweza mtafutia mwalimu wa English class kila jioni anapokua ametoka shuleni.

Kupeleka boarding kwa umri ni sawa na umeruhusu kwa 75% mtoto under 10 years ajitegemee, matokeo yake ndio mtoto anakuja kuwa na tabia fulani ambazo zinaweza kuwa sawa kwako na ata kwake, ila sisi tukaona teyari pale hatuna binti.
 
Bora aaende kidumu na mfagio kuliko kwenda kumpeleka mtoto wa nursery boarding school. Siamini pia kwa Tz hii kuna kijiji hakina hata nursery nzuri yani chaguo la kwanza na la mwisho ni kidumu na mfagio
 
Back
Top Bottom