Dr..inakuwaje mdada umri kati ya miaka20- 25 kutongozwa sana na wanaume watu wazima sana sana waliooa wenye familia huku vijana wanamuogopa hawamtongozi .
Asante mkuu
madam cute.
Very sorry kwa kuchelewa kukujibu.....nilikuwa busy kidogo!
Ila naomba nianze sasa kulijibu swali lako, sema nitaomba uniwie radhi kidogo, maana naenda kukujibu kwa kifupi, kama ifuatavyo:-
Awali ya yote naomba niweke bayana, kuwa scenario hiyo haimpati mwanamke pekee. Bali hata kwa upande wa kiume pia scenario hiyo inajitokeza, ingawa sio mara kadha wa kadha.
Kwa mwanamke, scenario hiyo inaanza kujitokeza kuanzia age ya 20 up to 26. Kwa upande wa mwanamke hii scenario, huwa na characteristic ya kuanza kwa kasi, then inaanza kunyong'onyea kadili siku zinavyokatika. Yaani pale inapoanza hapo kwenye age ya 20, huwa inakuwa na kasi sana. Ila kila muda unavyozidi kwenda, ndipo na scenario hiyo inavyozidi kupunguza kasi.....hatimahe upotea kabisa.
Ila kwa upande wa mwanaume, mara nyingi scenario hiyo inaanza kuonekana kuanzia age ya 23 up to 35. Na ina sifa kubwa ya kuanza kwa utaratibu sana, pale inapoanza kwenye hiyo 23. Ila kila muda unavyozidi kwenda, ndipo na scenario hiyo huzidi kukua mara dufu!
Hakika kwa pande zote mbili (mwanamke na mwanaume), scenario hiyo inasababishwa na muunganiko wa matokeo ya masuala mawili makubwa. Masuala hayo ni haya yafuatavyo:-
A. Asili ya kijinsia (biological & intellectual factors).
B. Mfumo wa maisha (personality)
Haya sasa, tuanze kuangalia udadavuliwaji wa masuala hayo sababishi.
A. ASILI YA KIJINSIA.
Hakika hiki ndio kisababishi cha kwanza, kinachopelekea kutokea kwa hiyo scenario. Lakini sababu hii, inatupa hasa jibu la kwanini scenario hiyo ujitokeza zaidi, kwa watu wenye range ya ages hizo tu. Kwa maneno mengine, kisababishi hiki kimejikita zaidi kuonyesha ni kwanini, hiyo scenario inawakumba wanawake wa age 20-26. While wanaume inawakumba, katika age ya 23-35.
-Sasa tukianza na upande wa wanawake, tunaona scenario hiyo inajitokeza kwa sababu ya uwepo wa matokeo chanya ya msingi mkubwa wa kijinsia, ambao tunasema ni BIOLOGICAL ISSUES. Hapa tunaangalia biological factors, zinazomfanya mtu wa jinsia ya kike, kutoka kwenye stage ya utoto na kuingia kwenye room ya kuwa mwanamke kamili. Hakika hapa ndipo mwanamke, anaanza kuwa na mng'ao, ambao unakuwa ni kivutio kikubwa kwa mwanaume yoyote yule. Hivyo ujikuta akiwavutia sana kimapenzi wanaume wengi, wenye sifa tofauti tofauti.
Ila ubaya au uzuri wa biological factors hizo, huwa zina asili ya kunyong'onyea, kila muda unavyoongezeka! Na hii tunaweza hata kuipima, kupitia maumbile ya mwili wa mwanamke. Kwa kawaida maumbile ya mwanamke wa kuanzia age 20's, ni tofauti na ya mwanamke wa age 40's.... Na ndio maana hapo juu tumeona, hata hiyo scenario pia ina sifa ya kupunguza kasi kwa mwanamke, kadili muda unavyozidi kwenda.
-Tukirudi upande wa mwanaume, tunaona scenario hiyo inasababishwa hasa na uwepo wa matokeo chanya ya msingi wa asili ya kijinsia katika INTELLECTUAL ISSUES. Hapa tunaongelea intellectual factors, zinazotuwezesha kupima uwezo wa mtu fulani, katika uwanja wa ufikiriaji na upambanuzi wa masuala mbalimbali. Hakika intellectual factors, ni moja ya factors pia zinazomfanya mtu wa jinsia ya kiume, kutoka kwenye room ya utoto na kuanza kuingia kwenye chapter ya kuwa mwanaume kamili.
-Pia tunaona uzuri au ubaya wa factors hizo, nyingi huwa zina tendency ya kukuza uwezo wa kifikiri wa binadamu. Sasa kwenye upande wa mwanaume pindi tu afikapo age ya kuanzia 23, tunaona uwezo wake wa kufikiri kama mwanaume unaanza kubadilika kitaratibu taratibu kwa kukua. Na hakika kila muda wa siku zinavyozidi kwenda, ndio na yeye anazidi kuimalika zaidi kifikra. Sasa tukiangalia hiki kwa makini, ndipo tunapata hoja ya swali la kwanini, mwanaume anazidi kuwa kivutio kikubwa cha wanawake wengi hasa waliomzidi umri, kadili ya jinsi ya yeye anavyozidi kukuwa kiumri!
B. MFUMO WA MAISHA.
Hapa katika mfumo wa maisha, tunaangali zaidi suala zima la personality. Personality inaweza kupimwa katika mambo kadha wa kadha, ikiwemo mamna mtu anavyoongea, anavyovaa, anavyo show his/her feelings etc. Hakika vipimo hivyo vya personality, ndivyo vinafanya tunasema "fulani anafaa kuwa kiongozi" au "fulani yupo kama kibaka" au "Mtu fulani anajisikia/anaringa" etc. Kwa kifupi, personality ndio kitu kinacho hamua mtu fulani awe na taswira ipi, katika jamii inayomzunguka.
Kwa msingi huo tunaona suala la personality, linaweza kupelekea pia mtu akajikuta anakumbwa na scenario hiyo ya kuogopwa na watu wa rika lake, katika muktadha mzima wa mahusiano ya kimapenzi.
Okay basi twende tukaone, how personality inaweza kuzalisha hiyo scenario. Na hapa nitaenda zaidi kuongea kwa upande wa mwanamke zaidi, kama swali lako mkuu
madam cute ulivyouliza.
Kwa kawaida mwanamke akifikwa na shida hiyo, ya kujikuta anaogopwa na wanaume wa rika lake, katika muktadha mzima wa mahusiano ya kimapenzi. Ni wazi mwanamke huyo ana personality kubwa, yaani ana muonekano wa matawi ya juu! Na taswira hiyo ya matawi ya juu, haiishii tu kwenye uzuri alionao. Bali pia inabeba hata namna anavyojiweka, kuanzia kukaa, kutembea, kuongea mpaka kuvaa kwake.
Hivyo vijana wenzake wa jinsia ya kiume au watu wanaolingana naye rika, wanakuwa ni watu wanaovutiwa sana kimapenzi na mwanamke huyo. Na akili mwao wanakiri wazi kwamba, hakika mwanamke huyo ni mzuri. Lakini shida inakuja pale, wanapoangalia personality nzima nzima ya mwanamke huyo husika. Hapo ujikuta psychologically, mwanaume anajivua wadhifa wa kuweza kumpata na kumfanya mlimbwende huyo kuwa mwenza wake, katika ulimwengu mzima wa mahusiano ya kimapenzi. Na hiyo yote inatokana na yale anayo yaona kwa mwanamke huyo. Na mbaya zaidi, endapo mwanaume huyo atakuwa tayari kasha kuwa affected kisaikolojia, juu ya hali yake duni ya kipato aliyo nayo!
Ila tukirudi kuona why watu wazima, ndio wanakuwa na courage ya kumtongoza mwanamke huyo. Hapa tunaona kuna vitu vingi sana, vinavyo build hiyo courage kwa wanaume wa age hizo. Awali ya yote tunaona inachangiwa na experience walizo nazo katika muktadha huo. Vilevile wengi wao wanakuwa na hali ya kujikubali psychologically, kwamba i can.....na hii ni matokeo ya uwezo wa kifedha au kitu fulani alichonacho etc. Hakika ndipo hapo, ile personality ya mwanamke iliyowatia hofu vijana au wanaume wa rika lake, inaposhindwa kutake place kwenye mind za watu hao wazima....
Kwa leo naomba niishie hapo
madam cute, in case una swali lolote.....you're welcome!
Asante.