Wakuu kwanini Jamii yetu inapenda kumuita Muuguzi wa kiume Daktari?

Pure Scientific

JF-Expert Member
Nov 19, 2015
692
546
Wakuu Habari za usiku,

Mimi ni mwanafunzi wa Uuguzi na ukunga (Nursing and Midwifery) ambaye ninahakikisha unazaliwa vizuri bila shida yoyote na hata ukizaliwa pindi utakapoumwa nakuhudumia na pia nina hakikisha una kufa kwenye Kifo kizuri (Peaceful death)

Tuachane na hayo nimekuwa nikijiuliza yafuatayo kuhusu kada yetu

1. Kwanini jamii inapenda kumwita Nurse wa kiume daktari popote pale anapokuwa nje ya kuvaa hata uniform zinazoashiria yeye ni Nurse?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza kabisa wanaoelewa hizo code za nguo ni nyie mliopo kwenye hiyo field. So mtu wa nje sio rahisi kufahamu huyu ni muuguzi au ni daktari.

Pili elimu kwa raia ni ndogo wao wanajua hata mfagizi hospitali ni daktari ambae siku hiyo kapangiwa zamu ya usafi.

Elimu ndio shida.
 
Kwanza kabisa wanaoelewa hizo code za nguo ni nyie mliopo kwenye hiyo field. So mtu wa nje sio rahisi kufahamu huyu ni muuguzi au ni daktari.

Pili elimu kwa raia ni ndogo wao wanajua hata mfagizi hospitali ni daktari ambae siku hiyo kapangiwa zamu ya usafi.

Elimu ndio shida.
Sio hivyo hata watu wa Karibu kama family, friends nao wanakuita hivyo japo ni skilled person

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio hivyo hata watu wa Karibu kama family, friends nao wanakuita hivyo japo ni skilled person

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna afisa Ustawi WA jamii Yuko hospital naye tunamuita docta ili kumvimbisha kichwa.Unajua manesi WA kiume ili jina hawalipendi Sasa Kwa Sisi tulioenda darasani tunawainua Tu ili wajisikie vizuri.

Ila kama alivyosema Dada hapo juu,watu wengi hawajui kutofautisha Kati ya nesi na daktari hasa huku mikoani.
 
chaliifrancisco,
Ni ile heshima tu ya watu waliojijengea juu yenu kutokana na unyeti wenu. Pili Nurse kwa mazoea yetu limekaa kikikekike na Doctor limeka kiume zaidi.

Hii ilizoeleka kuanzia miaka mingi ambapo ilikua ni nadra sana kukutana na Daktari wa Kike na pia kuwepo na idadi kubwa ya manurse wa kike.

Hivyo ikajenga picha kua Madaktari wote huwa ni wanaume na Manurse wote huwa ni wanawake.

Hivyo ni mazoea tu yamwendelezo huu. Japo siku hizi kuna ufahamu kidogo wa jinsi ya kumtambua daktari na nurse bila kujali jinsia zao.
 
Wakuu Habari za Usiku...

Mimi ni mwanafunzi wa UUGUZI NA UKUNGA(NURSING AND MIDWIFERY) ambaye nina hakikisha unazaliwa Vizuri bila shida yoyote na hata ukizaliwa pindi utakapoumwa nakuhudumia na pia nina hakikisha una kufa kwenye Kifo kizuri (Peaceful death)

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hakunaga kifo kizuri ndo maana hata ukifa ukiwa unacheka, msibani kwako watu watalia.
 
Nyamsusa JB,
Kwa kuongezea , hizo kazi kwa asili huku kwetu Afrika , Tanganyika ikiwa mfano.

Zilikuwa zikifanywa na wanawake wa kizungu ambao waliwafundisha wanawake wa Kiafrika.

Vilevile Mama zetu ndiyo waliokuwa na jukumu la kuzalisha wamama wenzao kwa njia za jadi.

Ni mageuzi ya Dunia ndiyo yamewezesha wanaume kufanya kazi hizo.

Watumishi wa kiume hosp tunajumuisha kwa Umoja wenu kuwa ni Madaktari iwe Mfamasia au Mhasibu
 
Kuna afisa Ustawi WA jamii Yuko hospital naye tunamuita docta ili kumvimbisha kichwa.Unajua manesi WA kiume ili jina hawalipendi Sasa Kwa Sisi tulioenda darasani tunawainua Tu ili wajisikie vizuri.Ila kama alivyosema Dada hapo juu,watu wengi hawajui kutofautisha Kati ya nesi na daktari hasa huku mikoani.
Unajua kumwita Nurse wakiume kwa jina inaonekana kama unadharau na wengi wao hawapendi kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni ile heshima tu ya watu waliojijengea juu yenu kutokana na unyeti wenu. Pili Nurse kwa mazoea yetu limekaa kikikekike na Doctor limeka kiume zaidi.

Hii ilizoeleka kuanzia miaka mingi ambapo ilikua ni nadra sana kukutana na Daktari wa Kike na pia kuwepo na idadi kubwa ya manurse wa kike. Hivyo ikajenga picha kua Madaktari wote huwa ni wanaume na Manurse wote huwa ni wanawake. Hivyo ni mazoea tu yamwendelezo huu. Japo siku hizi kuna ufahamu kidogo wa jinsi ya kumtambua daktari na nurse bila kujali jinsia zao.
Upo sahihi mkuu historia ya muuguzi ilianza kwa mwanamke kuanzia ulaya na Africa pia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom