Duka la Dawa Muhimu za Binadamu (Pharmacy): Utaratibu wa kufuata na mtaji wa kuanzisha biashara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Duka la Dawa Muhimu za Binadamu (Pharmacy): Utaratibu wa kufuata na mtaji wa kuanzisha biashara

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by mjasiria, Feb 17, 2011.

 1. m

  mjasiria JF-Expert Member

  #1
  Feb 17, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 3,790
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Wakuu nina maswali kadhaa kuhusu hii biashara.
  1. Je, ninahitaji vibali gani? Na vinapatikana katika ofisi zipi na pia itakuwa msaada sana kama itawezekana kuweka gharama zinazolipwa kwa kila kibali.
  2. Je, mtaji kiasi unatosha kufungua biashara hii.
  Natanguliza shukrani zangu.

  --------
  Michango ya wanaJF
  1.
  2.
  3.
  Kutoka TFDA

  Ushuhuda baada ya kufuata ushauri wa wanaJF
   
 2. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #2
  Feb 18, 2011
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mkuu kila kitu kinawezekana na kwa mtaji wa kiasi ulichosema, naamini lengo litatimia.

  Wahusika wakuu wa hii kitu ni TFDA ambao ofisi zao zinapatikana mabibo external.

  Nenda katika ofisi zao watakupa majibu ya maswali yako yote na mengine ambayo haukuuliza hapa.

  Naogopa kukupa majibu hapa kutokana na mapinduzi makubwa yaliyofanywa na TFDA katika biashara hii ya dawa baridi ambayo kwa sasa wanaziita dawa muhimu.

  Make sure you have all the details before jumping into it, si vibaya ukajaribu kuonana na watu ambao tayari wanafanya hii biashara, uhakika nilionao ni kwamba hii biashara inalipa, unachohitaji ni umakini na subira kwa siku za mwanzo za biashara.
   
 3. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #3
  Feb 18, 2011
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 986
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Kwa ufupi maeneo ya mijini huwezi kuanzisha tena duka la dawa baridi. TFDA ilishatoa tamko.. unatakiwa kuanzisha duka la dawa muhimu vijijini na pembezoni mwa mji ambapo inaelekeana na rural settings.

  Kwa maelezo zaidi wasiliana na TFDA, email info@tfda.or.tz . Pia kumbuka kuwa vibali vya maduka ya dawa baridi vinashughuliiwa na Halmashauri ya wilaya/mji/manispaa husika.

  Kama upo Kinondoni basi unawasiliana na mfamasia wa manispaa (Kinondoni anaitwa mabonesho) ila kama mdau aliyetangulia alivyosema nenda TFDA kaonane nao.

  Specifically kutana na Kitengo kinachohusika na Maduka ya Dawa muhimu (kwa kiingereza wanayaita ADDO).

  Upo hapo kama unataka namba zao ni-PM
   
 4. w

  wanan Senior Member

  #4
  May 24, 2011
  Joined: May 11, 2011
  Messages: 143
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  NISAIDIN JINSI YA KUPATA LESSEN YA DUKA LA MADAWA.Nataka kufungua duka la madawa ya binadamu mkoa songea naomba jaman anayefahamu njia za kupita ili nifanikiwe lengo langu anisaidie nawatakia siku njema
   
 5. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,865
  Likes Received: 2,805
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapo kwenye hospitali ya wilaya kuna mfamasia wa wilaya, nenda ukamwone atakupa utaratibu wote.
   
 6. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #6
  May 24, 2011
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 986
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Nenda kwa mfamasia wa mkoa au TFDA. TFDA wana ofisi ya Kanda pale Mbeya. ila kumbuka kwa Songea kuna maduka ya dawa aina mbili:

  1. duka la dawa muhimu- ADDO
  2. Pharmacy
  sasa wewe unataka kuanzisha lipi mana requirements zinatofautiana!
   
 7. w

  wanan Senior Member

  #7
  May 29, 2011
  Joined: May 11, 2011
  Messages: 143
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  La dawa muhimu mkuu,ahsante kwa ushauri nitafuatilia kaka.
   
 8. j

  joline365 Member

  #8
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 23, 2012
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naomba mwenye uzoefu na utaalamu wa biashara ya duka la dawa anisaidie, nataka kuanzisha hii biashara.
   
 9. a

  alph Member

  #9
  Oct 6, 2012
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nenda chuo kikuu entrepreneurship centre
   
 10. P

  Pharmaboy New Member

  #10
  Oct 6, 2012
  Joined: Oct 3, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aina gani ya duka la dawa?maana kuna duka la dawa muhimu na pharmacy
   
 11. M

  Mugaji Member

  #11
  Dec 7, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 13
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 3
  Ndugu wanajamii forum,

  Nahitaji kujua taarifa kuhusu biashara ya dawa baridi. Naomba msaada wa kujua mawazo yenu kuhusu hio biashara, walau mtaji kiasi cha chini ni kiasi gani inatakiwa, namna gani ya kuendesha na taratibu zote za kufungua hadi kuweza isimamisha. n

  Asante.
   
 12. S

  SN.BARRY JF-Expert Member

  #12
  Dec 9, 2012
  Joined: Oct 12, 2012
  Messages: 563
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 45
  milioni mbili hadi tatu, pia tafuta mfanyakazi mzoefu kidogo usije nunua madawa mengine yaka-expire store kukosa wtj.
   
 13. T

  Trance M Senior Member

  #13
  Feb 7, 2013
  Joined: Jan 27, 2013
  Messages: 183
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Malizia uzi wako na jaribu kuspecify ni Pharmacy au dawa baridi?
   
 14. laut

  laut Member

  #14
  Feb 7, 2013
  Joined: Feb 6, 2013
  Messages: 22
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  Ninalotaka kuanzisha ni duka la dawa baridi. Laut
   
 15. S

  Sumu JF-Expert Member

  #15
  Feb 7, 2013
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 6,233
  Likes Received: 3,218
  Trophy Points: 280
  Nasikia wakitangaza kuwa siku hizi ni siyo duka la dawa baridi ila ni duka la dawa muhimu.

  Kwa hisani ya watu wa Marekani.

  Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
   
 16. Erythrocyte

  Erythrocyte JF-Expert Member

  #16
  Feb 7, 2013
  Joined: Nov 6, 2012
  Messages: 44,593
  Likes Received: 25,516
  Trophy Points: 280
  Ili kuanzisha duka la dawa Muhimu ( zamani duka la dawa baridi , siku hizi yamefutwa , unayoyaona hayatafika july ) , kwanza ni lazima Iwe nje ya Mji ,

  Mahali ambako hakuna Maduka makubwa ( Pharmacy ), pia ni lazima uwe umepata mafunzo ya namna ya kuendesha Duka la dawa Muhimu yanayotolewa na TFDA on behalf of Ministry of Health and social Welfare ( hiyo ni lazima ).

  Kumbuka pia kuwa watoa dawa wako (wauzaji ) ni lazima wawe wamepitia Mafunzo ya utoaji sahihi wa dawa yanayotolewa na TFDA , ukikamilisha hayo nenda ofisi ya Mganga Mkuu ( pharmacy Department ) Kwenye halmashauri au Manispaa inayohusika utasaidiwa .
   
 17. k

  kibaravumba JF-Expert Member

  #17
  Feb 7, 2013
  Joined: Dec 21, 2012
  Messages: 3,661
  Likes Received: 1,593
  Trophy Points: 280
  Kuna ukiritimba mkubwa sana kama huna pesa ya kuhonga mfamasia wa wilaya usitegemee kupata leo.Ila kama ni famasi unatafuta cheti cha mfamasia unakilipia si chini ya sh.milion kila mwezi alafu unatafuta mtu yoyote anayejua majina ya dawa anakaa dukani kuuza dawa!

  Uzuri hawa jamaa ukishaweka cheti cha mfamasia tu dukani hilo duka wataliheshimu sana!Ole wako uwe afisa tabibu alafu ufungue duka la dawa baridi halafu wakukute unauza antibiotic,utadhalilishwa kama hujaenda shule ingawa ukiwa hospitali yoyote wewe ndo unawaandikia dawa hizo wagonjwa!

  Kifupi tu funguka mkwanja kwa mfamasia hata kama huna cheti huwa wanajua jinsi ya kufanya utapewa hata kopi ya mtu aliye dedi.
   
 18. laut

  laut Member

  #18
  Feb 7, 2013
  Joined: Feb 6, 2013
  Messages: 22
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  Nashukuru umenipa mwanga.
   
 19. M

  MINAKI Member

  #19
  Feb 16, 2013
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 41
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Habadi wana JF

  Nina mtaji wa Tshs. 20M na nimefikiria kuanzisha biashara ya duka la Dawa za Binadamu hapa Dar Es Salaam.

  Kwa wataalamu na wenye uelewa wa hii biashara, naombeni mnisaidie mnyambulisho wa nini kinachotakiwa kufanyika ili hii Biashara iwe na mafanikio na maendeleo zaidi.

  Taaluma yangu ni Mwalimu wa sekondari na ninataka kufanya biashara katika eneo hili linalooneka kuwa na mahitaji makubwa sana kwa Watanzania.

  Naombeni msaada wenu wa mawazo na kama kuna mwongozo naweza pia kuupata, naomba upost humu kwa manufaa wa watu wengine pia

  Shukrani na mapumziko mema nyote
   
 20. chaUkucha

  chaUkucha JF-Expert Member

  #20
  Feb 16, 2013
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 3,223
  Likes Received: 298
  Trophy Points: 180
  Kwa 20M iyo itakuwa ni Pharmacy na sio duka la dawa tena.
   
Loading...