Mkuu
Mshana Jr ,tumekuelewa
ila kwa sisi wa longi tunajua all the games people play,1995 ilikuwa hivi kwa NCCR Mageuzi na Lyatonga,2015 was the same kwa Chadema na moto wa Lowassa.
The game ya siasa zetu haichezwi kwenye zile dakika 90 uwanjani,the game inachezwa mezani!。
Huyu Maza kaingia na nia njema ya dhati,kaitisha timu zote zikae mezani,tujadili kwa pamoja the rules of the game,watu mkakataa!,akina sisi watazamaji wazuri wa huu mchezo,tukawashauri
Chadema, P'se, Msisusie Mkutano wa Vyama, Wasilisheni Hoja Zenu Mezani, Zitamfikia Samia, Ana Nia Njema na Nchi Hii, Mpeni Ushirikiano!.
mkagoma kwa kisingizio hamuwezi kukubali kukaa mezani huku mnene wenu yuko 'pahala salama'!。Tukamuombea msamaha
Watanzania tumshukuru Mungu kupata mtu mwenye moyo wa kusamehe. Je, tumuombe asamehe tu bila kuombwa msamaha au akomae naye? 。 Huyu mama alivyo Rahimu na asivyo mtu wa hiyana,akatusikiliza akatenda
Asante sana Rais Samia kwa kuliponya Taifa. Umeonesha kwa kauli na matendo; tunajenga nyumba moja, hakuna sababu ya kugombea fito! mnene wenu sio tuu akaachiwa,bali pia mapene mkavutishwa,mkamwagiwa!,ndipo mkakaa mezani!,mkakubaliana kugawana nusu mkate,mambo yalikuwa yanakwenda safi!
Mara Mbelgiji katua nchini akawavuruga!,sisi watu wa jicho la tatu takaona, tukawatonya kwa kuwauliza
Msikie Tundu Lissu Hapa, Anauliza Kama Wenzake Wana Akili Kweli! Maridhiano Ayaita Ujinga. Je, Lissu Bado ni Asset or Sasa ni A Liability?
Sumu ikawaingia,mara Kamanda akatangaza kukosa imani,na kujuta kukaa mezani, sisi watu wa ushauri,tukamshauri
Nimemwelewa sana Mbowe, usipoteze imani na Rais Samia. Alivyo kwa Kauli na Matendo hawezi kuwa ni yeye!
Kamanda akaamua Mbelgiji hatufai hivyo kwenye uchaguzi wa ndani mkamletea lile tutusa ,jamaa akasirika ndipo akaamua kumpandia kamanda kule kule juu kileleni na kumpopoa kwa mtindo wa tutabanana hapa hapa kwenye ile vita ya ama zake ama zangu!,ama zao,ama zetu!,mimi kama kawaida yangu kwanza nikawashauri Chadema
Japo Lowassa Alikuwa a Liability CCM, Akawa Asset Chadema. Lissu is a Very Bad Liability, but is The Only Asset Chadema Has Kuwangiza Ikulu!. Je... ?
Hapa na mimi naomba kukiri udhaifu wangu,sikuamini kama TAL angeshinda!hivyo nikamshari kukubali matokeo na kukubali kushindwa
Pre GE2025 - Baada ya Mbowe kutetea uenyekiti wake, masikini Tundu Lissu, kwishney! Je, atabaki ama atatimka? Lissu Cool down, usiitishe Press kumjibu Mbowe!
Najivunia kuchangia kufanyika uchaguzi wa haki Chadema kupitia onyo hili
The Voices From Within: Warning kwa Chadema, Be Very Careful, Msifanye Ujinga Wowote!, Mkileta Tuu Ujinga!, Tarehe 21 Jan. Kutakuwa Hakuna Uchaguzi!. mara ndio pap,kamanda chali!kichaa kachukua chama,kakamata usukani,mwendo ni mzobe mzobe!
NRNE ya kamanda sio kususia uchaguzi bali kushinikiza reforms na kama hakutafanyika reforms basi Chadema haitashiriki!,kamanda mpya katangaza vita na wenye mamlaka,kuwa bila reforms,hakuna uchaguzi!,kitu ambacho ni impossible!,sisi washauri wa bure,tukashauri tena。。。 si ndio akatangaza kukinukisha,, wenye mamlaka ndio kama hivyo wamemuhifadhi!
Kwa vile the real game inachezwa mezani,na matokeo yanapatikania mezani ila yanatangaziwa uwanjani , ile timu ya ushindi,tuliisha maliza kazi siku nyingi!,matokeo tayari tunayo kibindoni,uzuri wa jf ni kuwa wa kwanza kujua,nami mwana jf mwenzenu wa kule sina hiyana nimewajulisha wazi kabisa。。。
Hizi kukuru kakara zenu,ni kukuru kakara za mtu anayetafuta,bila kujua kuwa tafuta yote hii ni kujifurahisha tuu,na kuimalizia hiyo ruzuku ya mwisho mwisho!,wenzenu ni watu waliopata, ushindi tayari wanao kibindoni, wahangaikie nini?, ndio maana wametulia tuu,wamejituliza tuli ,wanasubiria tuu siku ya siku ya kipenga kipulizwe wapeleke timu na kuingiza uwanjani kukamilisha tuu zile taratibu za kumtangaza mshindi!
Siku hiyo ni siku ya
Unachukua。。 。
Unaweka。。。
malizia。。 。。
P