Wakuu, jambo hili limenitikisa

Wakuu, jambo hili limenitikisa

Huko kwenu hakuna vibinti vya chuo? Nasikia huwa vinaitibu hiyo hali.
Mkuu maisha yangu nikikuelezea utasema najisifia au kujikweza nimekuwa muumini wa karma na karma imeniletea majibu false kabisa mkuu nimeshindwa nikujibu nn..
 
Pole kwa changamoto unayopitia, kuna maswali ya msingi na hoja zifuatazo unapaswa kuzitafakari:

a) Je, huu ni mwisho wa dunia? Kwamba hili limetokea basi ndiyo kila kitu na hadi maisha yasimame?
b) Unaumia, unatetemeka je, aliyefanya kosa afanyeje? Aliyekukosea ndiye anayepaswa kuumia si wewe
c) Angalia thamani yako, unakubali kweli kuishusha kwa watu waliodhibitisha kwamba hawana thamani?
d) Look at your positive side, una watu wangapi wema wanaokujali na kukupenda (Ndugu, marafiki, n.k)
e) Tafakari picha kubwa, inawezekana kuna ujumbe hapa unapewa jipe muda kutafakari, jipe muda sana
f) Jifunze kusamehe and move on USILIPIZE KISASI kwa wote, muachie Mungu atakupa haki yako na wao atawapa haki yao pia
g) Kuna mengi ya kujifunza hapa, wewe binafsi hili limekufunza nini? nina hakika likipita hili utakuwa mtu bora, imara kuliko jana

Tafuta kitabu kinaitwa Fungate ya Milele, ukisome chote na ukikimaliza uje tena hapa utupatie mrejesho
 
Mkuu maisha yangu nikikuelezea utasema najisifia au kujikweza nimekuwa muumini wa karma na karma imeniletea majibu false kabisa mkuu nimeshindwa nikujibu nn..
Kawaida ukikosewa wewe ndio mwenye haki, itunze haki yako, pia tambua mwenzio kafungua mlango wewe unapaswa kuufunga na si kuung'oa kabisa.
Lakini hebu jitathmini je hakuna udhaifu mahala uliopelekea mwenzio kufungua mlango?.
 
Ni kweli mkuu ila sio kama huu, mtaa mzima unajua kitu yako inatumika na jirani yako hicho sio cha kutokujua!...wewe usipojua ndio mbaya zaidi..
 
Kawaida ukikosewa wewe ndio mwenye haki, itunze haki yako, pia tambua mwenzio kafungua mlango wewe unapaswa kuufunga na si kuung'oa kabisa.
Lakini hebu jitathmini je hakuna udhaifu mahala uliopelekea mwenzio kufungua mlango?.
Madhaifu kwenye ndoa hayakosekani Mimi sio Malaika hata kama ni kutoka nje....sio kwa ujirani huu hapo Panauma zaidi!!!!!pengine kwl niliufungua ila asingenifanyia na Jirani yangu hapahapa...
 
Sasa huyo jirani alikubaka bila kujua au?

Nyoosha maelezo sisi sio watabiri ndio tuweze kukushauri jambo ambalo hatulijui
 
Nimesoma uzi na comments ila sijapata kitu. Mtoa mada nadhani ana stress hawezi kuelezea vizuri walau tushauri chochote.

Kwa alieelewa basi amsaidie mleta mada kufafanua kidogo na wenzangu na mimi tupate mwanga tujue tunamnyakua vipi ndgu yetu na hilo jambo.
 
Kiasili sina maadui niwajuao direct humu duniani labda haters wa hapa na pale pamoja na yoooote sijawahi kubeba vinyongo kwenye moyo wangu sipendi mtu anidharau wala sidharau mtu,nikipita salamu simpiti mtu, kazini ndani siyo mtu wa vijiwe, bar wala chochote cha hivyo. Hizi social meetings labda msiba, jumuiya, sherehe ndio utanikuta na bado sina maneno mengi. Bhasiii bhana, ikaenda ikaenda nyie watu wazima wenzangu mtakuwa mmeshajua.

Kuna jambo nikawa nahisi muda mrefu linaendelea ila Mimi sina ushahidi nilihangaika nalo mwisho nikasema sifi na tai shingoni nikaingia mtaani nichukue data nikaongea na watu karibuni 9 hivi wote wakanambia mbona hiyo kitu inajulikana na MTT hata wa miaka 7 iko uchi ndio hivyo nikatajiwa hadi eneo pendwa la huo uovu unapofanyikia.

Kumbe watu walikuwa wanajisemea eti nilikuwa najua nikaamua tu kunyamaza! Nasikia mwenzangu aliwahi kuitwa akaonywa alichojibu ni kila mtu na maisha yake. Sijawahi kuvunjika moyo kiasi hicho, mtaani nikitembea kila mtu ananitizama kwa jicho ambalo silielewi mbaya zaidi aliyenifanyia ushenzi ni Jirani yangu pua na mdomo yaan sukari na Chai.

Hii kitu imeondoka na kilo zangu nyingi,nimeloose appetite kabisa wakuu najefeel soso down yaan sijui nielezeje sina hata hamu ya kupita barabarani kuna siku nilishindwa kuandika mikono ilinitetemeka plus machozi. Huyo mwenzangu ameniomba msamaha ,bado nafikiri cha kufanya moyo wangu umejeruhika mno kuliko maelezo najua kuna psychologist humu, kuna watu wenye maarifa na wasomi nifanyeje nirudie furaha yangu ya zamani.

Naomba kama utanikebehi don't comment maana itakuwa kunitilia chumvi kidondani msaada wenu wakuu, mahusiano hayo ni rasmi mbele za Mungu na wanadamu. Kwa Mara ya kwanza sisalimiani na huyo ibilisi aliyenizunguka! Bado sijajua nifanyeje na yeye nimuumize kama alivyoniumiza. Maumivu Niliyo nayo bora uchapwe fimbo kinachouma zaidi uaminifu uliotukuka nilio nao!
Muombe Mungu yakabidhi maisha yako kwa Yesy akupe amani nenda eagt city center kwa ajili ya maombi jifunze hili usilipize ubaya kwa ubaya bali wema kwa ubaya na mwenyez Mungu atakubariki kaa kimya usiache kuombe siku hizi za mwisho zinamapito sana uaminifu unajaribiwa sana ningekupa ushuhuda hapa muda hautoshi kumbuka usilipize samehe japo inauma sana na mwenyez Mungu atakusamehe barikiwa jitie nguvu
 
Madhaifu kwenye ndoa hayakosekani Mimi sio Malaika hata kama ni kutoka nje....sio kwa ujirani huu hapo Panauma zaidi!!!!!pengine kwl niliufungua ila asingenifanyia na Jirani yangu hapahapa...
Bado sijajua kama ww ni me/ke! Na pia ww kinachokuuma ni ujirani au usaliti? Unalalamika juu ya ujirani? Mengine hutokea ndani ya nyumba kwa rafiki au ndugu unaeishi naye! Anyway, pole sana kwa hilo lililokupata! Ni wazi muda tu ndio utakaoweza kukutibu jeraha hilo! The best revenge you can ever give ni KUSAMEHE na kumove on! Jipe muda, hili nalo litapita na kukupa mtazamo mpana zaidi ktk ndoa! Ni mambo magumu sana lakini yanawezekana, mkaribie Mungu, hojiana naye pia! Nikutakia kupona haraka ktk hili ktk jina la Yesu, amen!
 
Madhaifu kwenye ndoa hayakosekani Mimi sio Malaika hata kama ni kutoka nje....sio kwa ujirani huu hapo Panauma zaidi!!!!!pengine kwl niliufungua ila asingenifanyia na Jirani yangu hapahapa...
Kumbe Lulu kinachokusumbua ni ujirani sio?, kwa hiyo kama ni kosa rukhsa kulitenda mbali na nyumbani? Hapana! kosa ni kosa tu.
 
Hii uzi ili uielewe unatakiwa uwe mmbea sana hiv hiv huelewi hta moja
 
Nimesoma uzi na comments ila sijapata kitu. Mtoa mada nadhani ana stress hawezi kuelezea vizuri walau tushauri chochote.

Kwa alieelewa basi amsaidie mleta mada kufafanua kidogo na wenzangu na mimi tupate mwanga tujue tunamnyakua vipi ndgu yetu na hilo jambo.

Kuna harufu ya mtu kuchapiwa kwenye huu uzi. Mleta mada ni me/ke ambae amechapiwa na jirani yake sasa ndio kaja kulia lia humu. Kasahau kabisa kwamba kuchapiwa ni siri ya ndani.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom