Wakuu huwa mnafanyaje kupata wanawake wa ndoto zenu

martial jb

JF-Expert Member
Oct 21, 2021
864
1,456
Habari wakuu,
Naomba nitoe heshima zenu kwa wale wote walio wakubwa kwangu na ni niende moja kwa moja kwenye mada kuhusiana na wenzetu wanawake, ambao ni wasaidizi wa maisha yetu kama muumba alivyoamrisha.

Maisha ya mapenzi siku hizi yamejaa visa na mikasa mbalimbali, wanawake wamejaa tamaa na kutoridhika, wanawake wamekuwa wasumbufu na wenye hila sana hasa linapokuja suala hili la mapenzi.

Inafikia hatua mpaka kuna vijana humu wanaeneza kampeni hasi za kukataa ndoa. Hii ni kutokana na mambo wanayoyaona yakifanyika. Kiukweli hii ni changamoto kwelikweli.

Swali langu kwenu wakubwa ni kuwa mnafanyaje mpaka mnafanikiwa kupata wanawake wa ndoto zenu ama huwa mnatumia vigezo gani kuchagua na mpaka kudumu nao kwenye ndoa ama mahusiano. Na pia ni muda gani sahihi wa kumtafuta mwenza wako wa ndoa ama mahusiano. Maana me kila nikiangalia naona kama kuna giza hivi.

Tupeane ushauri na uzoefu wakuu maana sisi wengine ni vijana na tupo katika safari ya maisha.

Sitaki watu wa komenti za kataa ndoa, TAFADHALI
 
Kipimo Cha chini cha uchunguzi miaka 2 na Nusu yaan hapo unamchunguza usije ukaoa shoga, kingine control wenge lako acha kua na wenge ukitaka kujenga maisha na mwanamke usije utavaba mapema
 
Kama una ndugu jaribu kuwatumia wao wakutafutie mwanamke mwema
Hata mama pia anajua familia nzuri zenye maadili

Ila najua kuna watu watapinga na hao wanaweza kuwa wale wanaoamini kujuana miaka kibao na mwanamke ndio kuja kuoana baada ya kuzaa nae

Mimi naamini kwa kuelekezwa kuliko kutafuta kwenye daladala au bar au barabarani na kuuliza namba maana hapo ndipo matatizo yanapoanza
 
Pamoja sana kiongozi, lakini sijakupata kuhusiana na wenge mkuu
 
Hakuna formula maalum. Kila MTU huwa ana njia zake. Wengine by coincidence tuu umekutana na MTU moja Kwa moja ukaamua kuoa.

Wewe mwenyewe ndio uweke vigezo vyako. Wengine wanaangalia makalio wengine Sura wengine Tabia.

All in all tafuta wa kuendana na wewe.....unaweza taka mchamungu kumbe wewe sio mchamungu..! Unaweza kutaka anayevaa Kwa stara kumbe wewe kucha kutwa unatamani wavaa vikaptura.

Eid Mubarak
Cheers

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daaaah!!! Umetisha sana kaka,
 
Minal faidhina, naamini Allah atanipa ninayeendana nae inshaallah
 
Pamoja sana kiongozi, lakini sijakupata kuhusiana na wenge mkuu
Emotional control ukiweza kujicontrol mwenyewe utaweza kuyacontrol mapenzi apart from that 'utabaa'

Nb: kwenye funga & fungua semi ni neno lisilo rasmi
 
eb6cd51a-da81-453a-99ed-caed24657098.jpg
 
Kama una ndugu jaribu kuwatumia wao wakutafutie mwanamke mwema
Hata mama pia anajua familia nzuri zenye maadili

Ila najua kuna watu watapinga na hao wanaweza kuwa wale wanaoamini kujuana miaka kibao na mwanamke ndio kuja kuoana baada ya kuzaa nae

Mimi naamini kwa kuelekezwa kuliko kutafuta kwenye daladala au bar au barabarani na kuuliza namba maana hapo ndipo matatizo yanapoanza
Hii inatumiwa sana na Jamii ya waislamu maana waislamu kufunga ndoa ni Suna, kwao hata buku 10 unapigwa mkeka km mahari unalipwa buku 10 ndoa unafungwa saaafi Ila wakristu kisanga Mzee Mushi anataka Ng'ombe 10 gharama yake kila Ng'ombe 500,000 piga mara 10 hapo bado koti la Babu makaja wa Bibi sijui makolokolo gani

Sasa dada/mama yako akushauri mke wa kumuoa yeye ndie anaekulipia mahari ?
 
Habari wakuu,
Naomba nitoe heshima zenu kwa wale wote walio wakubwa kwangu na ni niende moja kwa moja kwenye mada kuhusiana na wenzetu wanawake, ambao ni wasaidizi wa maisha yetu kama muumba alivyoamrisha.

Maisha ya mapenzi siku hizi yamejaa visa na mikasa mbalimbali, wanawake wamejaa tamaa na kutoridhika, wanawake wamekuwa wasumbufu na wenye hila sana hasa linapokuja suala hili la mapenzi.

Inafikia hatua mpaka kuna vijana humu wanaeneza kampeni hasi za kukataa ndoa. Hii ni kutokana na mambo wanayoyaona yakifanyika. Kiukweli hii ni changamoto kwelikweli.

Swali langu kwenu wakubwa ni kuwa mnafanyaje mpaka mnafanikiwa kupata wanawake wa ndoto zenu ama huwa mnatumia vigezo gani kuchagua na mpaka kudumu nao kwenye ndoa ama mahusiano. Na pia ni muda gani sahihi wa kumtafuta mwenza wako wa ndoa ama mahusiano. Maana me kila nikiangalia naona kama kuna giza hivi.

Tupeane ushauri na uzoefu wakuu maana sisi wengine ni vijana na tupo katika safari ya maisha.

Sitaki watu wa komenti za kataa ndoa, TAFADHALI
Unatandika kitanda, unashusha mosquito net, unapanda kitandani una lala, usingizi ukukuoitia unaanza kuota.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom