Picha za ngono na kupenda wanawake watu wazima

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
495
997
Habari zenu,

Kwanza ningependa kuipongeza Serikali yetu kwa kufungia wavuti (Websites) za ngono japo kuna watu wanaangali kwa VPN.

Wakuu mkiangalia jamii yetu kwahivisasa inazidi kuporomoka kimaadili kwasababu ya picha za ngono. Vijana wadogo tamaa zimewazidi kwa kutaka kuyatenda yale wanayoyaona kwenye video za ngono, imefikia hatua vijana wadogo wanawatongoza wanawake rika la wazazi wao kwasababu wanayaiga wanayoyaona kwenye video za ngono.

Sio ajabu sana sasaivi kuona vijana wadogo wakiwataka wanawake wakubwa kingono na ukiangalia sababu au Chimbuko ni hizo video za Ngono mitandaoni.

USHAURI
Jamii tupambane na huyu Adui Picha za Ngono kwa kuwaambia watoto athari za picha hizo mapema kabla hawajaharibikiwa.

Najua ni ngumu ila tukiamua kama jamii tunaweza kulishinda hili tatizo la picha za ngono kwenye jamii yetu.

NB: PICHA ZA NGONO NI KAMA MADAWA YA KULEVYA, TUPAMBANE NAZO KUILINDA JAMII YETU.
 
Jamii isiyomjua Mungu kwelikweli haiwezi pambana na msambazaji wa videos hizo katika ulimwengu wa roho, Lusifa .
Jamii yenyewe ni hii watu wanafanya ngono kabla ya ndoa na wanaona ni sawa. Impossible. Ishi maisha yako tu mkuu.
 
Yani wewe mimi ndiomana napenda kusoma comments zako, inaonyesha ni mtu mwenye hofu ya Mungu 🙏
Sijawahi kuona comment ya pumba kwako hata moja!!! Mungu azidi kukuinua viwango vya juu
 
Vijana hawàna ajira na hawataki kujishughulisha,wanaishia kubeti na kutongoza wamama ili wawaweke mjini.Jamii inazidi kutoka kwenye misingi yake hasa pia kwa ongezeko la single parents,hivyo vijana hawalelewi vema na kupelekea kuwa na kizazi hiki tulichonacho.
 
Wanawake bwana mambo ya dini yamewakaa sijui kwa nini ?

Haya nuambie kwa nini nyie wanawake dini na habari za Mungu hazikosekani vichwani mwenu ?
Wahala kumekucha 🤣🤣🤣
Dini na habari za Mungu ni km sheria, ukiwa na Mungu kuna vitu utaogopa kufanya.
Vivyo hivyo na sheria za duniani ukijua kuna jela utaogopa kufanya uhalifu!!
 
Tatizo limeanzia kwenye ubora wa elimu yetu. Shule za kata ndo zinaongoza kwa kutoa wahuni, vibaka na machangudoa. Kilaa kitu ili kiwe sawa kwenye jamii kinaanza na utimamu wa akili kwanza. Serikali ya ccm ni mnufaika mkubwa wa vijana wa hovyo, hizo habari za vijana kupenda wamama watu wazima ni sehemu tu ya athari za mifumo duni ya elimu ambayo hupelekea kuwa na vijana wasio na hofu ya kitu chochote. Ukosefu wa ajira nao umeleta athari kama hizi kwa sababu vijana wako loose tu mitaani.
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom