Wakulima wa ufuta Lindi na Mtwara waililia serikali kushuka kwa bei ya ufuta

Shindu Namwaka

JF-Expert Member
Sep 22, 2014
4,911
3,082
16cc281d1dc67a0d8d943eaec1264131.jpg

Anaandika Mwl Razaq Mtele Malilo.

Katika misimu miwili iliyopita zao la ufuta lilinunuliwa kuanzia Tsh 2500 hadi Tsh 3000 hali iliyopelekea watu wengi kuhamasika kulima zao hili kwa wingi na vijana wengi walihamasika kurudi mjini hasa jiji la Dar Es Salaam baada ya kuvutiwa na ongezeko hilo la bei hali ilyopelekea uzalishaji wa ufuta katika nchi yetu kuongezeka na kuwa ya kwanza barani Afrika na ya tatu duniani.

Katika hali isiyotarajiwa bei ya ufuta mwaka huu imeshuka kati asilimia 45 hadi 50 na zao hilo limenunuliwa kwa bei ya Tsh 1600 hadi Tsh 1500 katika mikoa hiyo ya Kusini bei ambayo haina tija kwa mkulima hasa ukilinganisha na kupanda kwa gharama za uzalishaji wa zao hilo na gharama za maisha kwa ujumla.

Ikumbukwe kwamba kutokana na kupanda kwa bei ya zao hilo miaka miwili iliyopita watu walikuwa wakijikiti katika kilimo cha zao hilo la biashara na kupunguza kulima mazao ya chakula kama mahindi wakitegemea kununua chakula pale wauzapo ufuta.

Lakini pia mwaka huu katika mikoa hiyo yalitokea majanga ya mafuriko yaliyosababisha kusombwa kwa mazao ya chakula shambani kama mahindi, mihogo na mazao mengine. Hivyo, watu walitegemea zao la ufuta liwe kama mkombozi wao kwani walitegemea bei nzuri kama ya mwaka jana au kupanda zaidi hii ni kutokana na ahidi ya Mh Rais Dr. JOHN POMBE MAGUFULI akiwa kwenye kampeni katika kijiji cha NANGARU, jimbo la Mchinga mkoani Lindi, OKTOBA 13 MWAKA JANA aliwaahidi wakulima wa ufuta kuwa atahakikisha anasimamia bei ya zao la ufuta ili wananchi hao wauze mazao yao kwa bei ya tija ili nao wajikwamue na umasikini.

Ahadi iliwafanya wakulima hao wahamasike kumpigia kura nyingi na alipopita kuwa Rais walihamasika kulima ufuta kwa wingi wakitarajia bei ya tija zaidi ila hali halisi imekuwa kinyume chake mara dufu.

Hivyo basi, kutokana na kushuka kwa uzalishaji wa mazao ya chakula kwa sababu za mazao kusombwa na mafuriko na wakulima kujikita zaidi na mazao ya biashara na hii ni kutokana na kutokuwa na uwezo wa kugharamia mazao yote ya chakula na kilimo kwani wanatumia zana duni za kilimo kama jembe la mkono hivyo kushindwa kumudu kulima mazao yote .

Anguko la bei ya ufuta ni pigo kwa wakulima hao na uwenda hali hii ikasababisha maisha magumu kwao na pia kukabiliwa na njaa kali kwani wengi wao walitegemea kuuza ufuta ili wakipata pesa wanunue chakula na mahitaji mengine ya msingi.

Hivyo , kwa sasa wakulima hao wamebaki wakiwa wanyonge wakiwa hawana cha kufanya na wamekosa mtetezi.

Wakulima hao wanaiomba licha ya kutowasaidia kipindi cha kilimo, wanaiomba serikali na Rais Magufuli akumbuke ahadi yake kwa wakulima hao kwani wamekula hasara kubwa mwaka huu.

Wanaitaka serikali iwatafutie soko la uhakika na lenye tija ili nao waweze kujikwamua kimaisha na kuondokana na umasikini.

Kwa niaba ya wakulima natumaini ujumbe huu wa wakulima utawafika wahusika na wataufanyia kazi.

Ahsante.
Ni mimi SAUTI YA WANYONGE.

Mwl Razaq Mtele Malilo.
Mipingo, Lindi.

0763753832/0659913056.

Chanzo muungwana blog
 
Back
Top Bottom