DOKEZO Tunduru: Vyama vya Ushirika vinawadhulumu na kuwaibia pesa wakulima wa ufuta

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Jinsi Vyama vya Ushirika vinavyodhulumu na kuwaibia pesa Wakulima wa zao la ufuta Tunduru.

Mwaka huu soko la zao la ufuta linasumbua, hii namaanisha bei kushuka kila mnada Mfano Mnada wa kwanza bei Sh 3700 @kg na mnada wa pili ni Sh 3600@kg na wa tatu ni sh3500@kg

Hivyo wanadhulumu kwa kuchelewesha malipo kwa wakulima wakisubiri bei ishuke ili walipe kwa bei ndogo ilihali wameuza kwa bei kubwa.

Mfano mimi nimeuza mnada wa Kwanza kwa Sh 3700@kg. Wao wanasubiri bei ishuke Mfano Sh 3500@kg
hivyo wanaiba sh200@kg

Kuna baadhi ya Wakulima tumeenda kulalamika kwa viongozi wa kisiasa kama vile madiwani na kwa Mwenyekiti wa CCM wilaya lakini hakuna hatua iliyochukuliwa.

Ukweli ni kwamba hii tabia ya Vyama vya Ushirika kuibia Wakulima ilikomeshwa na aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya Tunduru, Julius Mtatiro lakini baada ya yeye kuondoka wemeanza tena.

Hivyo tunaomba mamlaka za juu kutusaidia.

Pia soma
- KERO - Tunduru: Vyama vya Msingi vinachelewesha malipo ya wafanyabiashara wa mazao
 
Back
Top Bottom