Jifunze kilimo cha nyanya

mkuu mavuno ya nyanya yapo hivi,
sisi tunauza kwa box, na tunavuna kila wiki.

sasa ule mchumo wa kwanza tunaita fundisha, sasa mfano mchumo wa kwanza ukichuma box 20 utaangalia na bei itakavyokuwa sokoni mfano ikiwa 10000 utapata 200,000/=

utakuja mchumo wa pili box zinaongeza unaweza kupata box 60 pia utazidisha kwa bei iliyopo sokoni au tufanye ile ile 10000 utapata 600,000/=

mchumo wa tatu unaweza kupata box 120 pia utazidisha kwa bei

mchumo wa 4 utaweza kupata box 180 pia utazidisha kwa bei

mchumo wa 5 unaweza kupata box 240 utazidisha kwa bei,

baada ya hapo nyanya nitaanza kupungua mchumo unaofata zitarudi 180 alafu 120 alafu 60 mwisho 20 biashara imeisha

utajumlisha kila mchumo umepata bei gani utatoa na gharama ulizotumia

hizo bei ni mfano zinaweza kuzidi au kupungua
Mkuu yaani kwa michumo yote box zinaweza kupatatikana kiasi gani
 
Mkuu kwanza nitagulize shukurani zangu za dhati kabisa kwako na wengine walioshiriki kuchangia kwenye uzi huu hai tangu 2017, sasa 2020 na miaka mingi ijayo.
Leo asubuhi nimeamka nikaingia hapa
Business Ideas, Opportunities, Inspiration and Success Tips for African Entrepreneurs - Smallstarter Africa huyu ni mnaigeria anachambua sana mambo ya ujasiria mali hasa barani africa. Nikasoma chain value ya zao la nyanya "NIKAHAMASIKA SANA"
Nikaingia jamii forum niangalie tips zinazo elezea kilimo cha Nyanya, safi sana sijtumia nguvu sana uzi huu hapa umesheheni madini sana.
Mimi nimhanga wa awamu ya tano kwenye kupata kazi, toka leo naweka plan ya kuingia kwenye hiki kilimo.
Naombeni wapendwa kwa kuanza na ROBO HEKA na hitaji kiasi gani? au kwa mchanganuo huu
Katika:-
-Mkoa/wilaya mzuri kwa maana ya ardhi pamoja na upatikanaji wa masoko
-Kukodi robo heka na maandalizi ya eneo mpaka kupanda
-Mbegu nahitaji gm ngani na aina ipi ya kisasa itakuwa nzuri
-Gharama ya mashine ya umwangiliaji na mipira yake
-Gharama ya mfuta kwa kipindi chote mpaka navuna
-Msimu mzuri wa kulima ili kuwa na uwezekano mkubwa wa kupata soko zaidi kwa bidhaa hii
- Na gharama zingine najua muliopo kwenye hii kazi mnajua mengi.
Pia naomba kuunganishwa kwenye Group la Whatsapp la kilimo cha Nyanya Namba yangu
0759 071 297
Ahsanteni sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimependa hii. Naomba kujua mbegu ikisiwa nachukua muda gan mpaka kupandwa? Na je makadirio ya gharama za mpaka kuvuna inaweza kuwa sh.ngap kwa robo heka? Asante.
 
Nami nafikilia kulima kilimo hicho
Nami nafikilia kulima kilimo hicho
kilimo cha nyanya ni kizuri lakini ni kilimo chenye changamoto kubwa sana…ninachokushauri anza kwanza na bustani ndogo ya nyanya nyumbani kwako….ukimudu kuihudumia bustani tafuta eneo kubwa...ukikurupuka kwenye kilimo cha nyanya utajikuta unapata hasara.
 
kilimo cha nyanya ni kizuri lakini ni kilimo chenye changamoto kubwa sana…ninachokushauri anza kwanza na bustani ndogo ya nyanya nyumbani kwako….ukimudu kuihudumia bustani tafuta eneo kubwa...ukikurupuka kwenye kilimo cha nyanya utajikuta unapata hasara.
Mada nzuri sana.
 
kilimo cha nyanya ni kizuri lakini ni kilimo chenye changamoto kubwa sana…ninachokushauri anza kwanza na bustani ndogo ya nyanya nyumbani kwako….ukimudu kuihudumia bustani tafuta eneo kubwa...ukikurupuka kwenye kilimo cha nyanya utajikuta unapata hasara.
Huu Ni ushauri wa kiuzoefu, well said. Kila kitu unahitaji ujifunze kwanza, then utanue kidogo kidogo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
swali lako lina majibu mawili
Je, umeotesha mbegu katika kitalu ama katika trays?
Na
iwapo ni Trays huwa ni vizuri kununua na udongo wake kabisa hivyo tangu kusia hadi siku ya kupanda shambani huwa wanapendekeza iwe siku 21.
Ila iwapo ni kitalu napo pia wanapendekeza basi isivuke siku 30.

Mfano mwezi uliopita March 20
nilisia mbegu aina ya Imara F1
50gm kwa Ekari 1
makisio ni upate miche 4,500 hadi 4,800
Kwa Ekari moja coz ktk upandaji kuna nafasi unazoacha, mche na mche, mstari na mstari.
Na
Shambani nilipanda miche Tar 20 Mwezi huu!


Sent from my iPhone using JamiiForums
Umemjibu Vema kabisa
 
Duuh, nilichangia siku nyingi sana ila sasa post zimeshoot sana mpaka 800+. Hii ni kwa jinsi gani watu wana nia na uchu wa kuingia kwenye kilimo hiki.
Nami nikiungwa kwny group itakuwa vyema. 0712310605.

Ahsante.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom