Wakulima wa Newala wagomea bei ya korosho

Wakulima wa Newala wagomea bei ya korosho

Bei ikipanda mnasema serikali ya CCM imefanya jitihada kupandisha bei ili kumjali mkulima(mnatumia fursa hiyo kupiga siasa),bei ikiwa mbaya,hamtaki siasa,badala yake mnasema uhalisia kua tatizo ni soko,tena yule jamaa mbana ajira mkuu anajitapa kwelikweli.

Tanzania hamna wachawi,haiwezekani CCM na jamaa watutese hivi,wamgeondoa vyote au kimoja kati ya chama na mtu.
Ndugu Allen kuna mambo mengine haifai kuingiza siasa, bei ya korosho duniani imeanguka na kuna korosho nyingi sana za mwaka jana hazijauzika, kama za Ivory coast na nchi zingine za west africa.

Bei elekezi iliyotolewa mwaka huu na bodi ya korosho ni zaidi ya mwaka jana. Korosho yetu karibu yote inakwenda nchi za nje hasa Iindia, na hua zinauzwa kwenye mnada, wanaonunu ndio wanaotoa bei. Sasa hapo serekali ama chama cha ccm, kimehusikaje kuangusha bei.

Tuwe wakweli
 
Mnunuzi nae wanahitaji faida hawezi nunua 3,400 kwa mkulima akauze 3400 sokoni mimi unafikiri ikiwezekana bodi iende ikauze yenyewe ndo iwaletee wakulima mipesa yao yote wanayoitaka.

Kugoma bei ya 2717 wakati sokoni ni 3400 ni upuuzi maana kuna bei ya kusafirisha kwenda bandarini pia kuna clearing cost. Sasa ukisema unataka yote 3,400 peleka sokoni mwenyewe
 
Big up hizo ndo faida za Vyama vya ushiriki wakulima kuwa na nguvu na kupambana na wanunuzi
 
Mnada wa korosho uliopigwa leo Newala sh 2700/= na Tandahimba sh 2717/= wakulima Newala wamegoma kuuza korosho zao bei wamesema ndogo
Jiwe lina gundu, ukiona limejichomeka kwenye kitu chochote ujue ndio basi tena.

Yawezekana JIWE ndio shetani mwenyewe.
 
Politics politics politics, ukiziendekeza unaweza ukaamini hata matatizo yako binafsi yameletwa na wanasiasa na mjadala ushavamiwa na makada.
 
Tandahimba na Newala mnada hauwi siku moja, hiyo inayoitwa Tanecu (Tandahimba and Newala cooperative union) ndio chama cha kuuza na huuza tofauti katika maghala yao yaliyopo Tandahimba au Newala kwa wakati tofauti, hakuna kipindi wanauza maghala yote kwa siku moja.

Nb: Nimeleta taarifa sio ubishi, taarifa yake haina source. Mnada bei chini ilikua 1711 na juu iliishia 2717 na wakulima wame opt kusubiri mnada ujao
Uliza vizuri uelewe mnada kwa newala tandahimba unapigwa siku moja
Ndiyo mana unakuta muunganiko wa (Ta). Tandahimba (Ne). Newala....hata kule Ruangwa kuna Chama kikuu kinaitwa Runali yani (Ru) Ruangwa (Li) Liwale (Na) Nachingewa.sehemu hizo mnada unapigwa siku moja na Newala na Tandahimba mnada unapigwa siku moja humo mote msimamizi ni chama kikuu jina TANECU hitimisho.
 
Ngoja niwaambie kitu...wakulima wa nchi hii wana nguvu kubwa sana kuilinda nchi kiuchumi na kiusalama. Wanachohitaji ni ushirikiano wa vitendo kutoka kwa serikali. Yaani serikali na wakulima wafike mahali waongee lugha moja na hakuna kati yao awe na wasiwasi na mwenzake. Kusema 'kuhakikisha' ni sawa mbegu lakini "kutekeleza uliyohakikisha kutekelezwa" ni sawa na mbegu hiyo kuwa mche wenye afya nzuri uliojaa mazao kwa ajili ya kuvunwa ingawa uangalizi wa mche huo ni wa mkulima.

Ni wakati sasa wa serikali baada ya kunadi mbegu bora za kilimo sasa mbegu hizo zipandwe na tupate miche yenye afya. Na nyinyi wakulima mkisha kupata miche hiyo palilieni na mvune mazao yake kwa uadilifu (siyo unachanganya korosho, kahawa, ufuta, mbaazi nakadhalika na mawe ama mchanga na kumuuzia mnunuzi).

Serikali tumieni mbinu hii ya serikali ya Russia. Russia imegundua nguvu kubwa iliyoko kwenye wakulima wa nchi hiyo, kwa sasa inaitunza nguvu hiyo kama mboni ya jicho lake kwa kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wakulima wake. Serikali pandeni mbegu ili mfaidi nguvu ya wakulima kulinda nchi kiuchumi na kiusalama.

Ebu kwa uchache msomaji wa post hii tazama namna serikali ya Russia inavyo tunza nguvu ya wakulima wake kupitia clip hii hapa chini.

 
Wakulima wa korosho wanapelekeshwa kama kitenesi!

Ova
HAPANA JAMANI, HII BEI YA KOROSHO YA MIAKA HII MIWILI ILIYOPITA IKAFIKA MPAKA ELFU 4, HAIKUWA BEI HALISI YA KOROSHO ILIKUWA NI KWASABABU YA UHITAJI HUKO DUNIANI. SASA SOKO LA KOROSHO DUNIANI LIMESHUKA KWA 50% MNATEGEMEA WANUNUZI BADO WANUNUE KWA BEI ILE ILE? NA TUKUMBUKE BEI YA SERIKALI NI 1550 SASA MTU ANANUNUA 2715 MNAKATAAJE?
 
Mnada wa korosho uliopigwa leo Newala sh 2700/= na Tandahimba sh 2717/= wakulima Newala wamegoma kuuza korosho zao bei wamesema ndogo
NA KWANINI HAWAKUIGOMEA BEI ELEKEZI YA SERIKALI? AMBAYO NI 1550, MAANA YAKE MNUNUZI ANAYENUNUA ASISHUKE 1550 SASA MTU KAFIKA 2700 MNASEMA NDOGO
 
Iligomewa shilingi 2700 enzi ya Magu mwaka 2018 leo 2021 bei shilingi 2280 duh noma sana hii nchi hii
 
Back
Top Bottom