Wakulima wa Newala wagomea bei ya korosho

Wakulima wa Newala wagomea bei ya korosho

Kweli nimesalimika kuingia mkenge, hii biashara nilishawishiwa sana kuifanya, nikamwambia nikafanye utafiti kwanza mwaka huu mwezi wa 9, nilichoshuhudia inavyofanyika niliamua kurudi kuja kuendelea na ninachofanya tu. Wanaopiga pesa ni watu wenye makampuni kununua kwenye minada na kupeleka nje.
 
Tandahimba na Newala mnada hauwi siku moja, hiyo inayoitwa Tanecu (Tandahimba and Newala cooperative union) ndio chama cha kuuza na huuza tofauti katika maghala yao yaliyopo Tandahimba au Newala kwa wakati tofauti, hakuna kipindi wanauza maghala yote kwa siku moja.

Nb: Nimeleta taarifa sio ubishi, taarifa yake haina source. Mnada bei chini ilikua 1711 na juu iliishia 2717 na wakulima wame opt kusubiri mnada ujao
Sasa tofauti ni nini hapo......bei uliyotaja inakaribiana na ya mleta mada na wakulima hawakuuza!
 
Wakulima wote wajichunge, utekwaji utapitia huko muda so mrefu.
 
Mwaka jana bei ya korosho ilipokuwa juu CCM walisema ni kutokana na juhudi zinazofanywa na Serikali katika kutekeleza sera za chama hicho. Sasa mwaka huu bei ya korosho imeshuka, nani wa kulaumiwa kama si CCM?

Kunguru wa Lumumba mizaha yenu ni maafa kwetu sote!!
Ndugu Allen kuna mambo mengine haifai kuingiza siasa, bei ya korosho duniani imeanguka na kuna korosho nyingi sana za mwaka jana hazijauzika, kama za Ivory coast na nchi zingine za west africa.

Bei elekezi iliyotolewa mwaka huu na bodi ya korosho ni zaidi ya mwaka jana. Korosho yetu karibu yote inakwenda nchi za nje hasa Iindia, na hua zinauzwa kwenye mnada, wanaonunu ndio wanaotoa bei. Sasa hapo serekali ama chama cha ccm, kimehusikaje kuangusha bei.

Tuwe wakweli
 
Back
Top Bottom