X_INTELLIGENCE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2014
- 10,344
- 14,116
Ndugu, jamaa na marafiki zangu habari zenu. Nikiwa mdau na mkeleketwa wa kilimo huwa napata uchungu sana pale mkulima anaponunua mbegu ambayo inamletea mavuno duni, wakulima wanashindwa kuendelea na hii yote ni kutokana na baadhi ya makampuni yanayouza mbegu kutokuwa na uhakika na mbegu zao...makampuni haya husifu mbegu zao na kuzipa ubora ambao haistahiri...utakuta mbegu inasifiwa na kampuni kuwa inahimiri na kutokudhuriwa na magonjwa kumbe ni kinyume...pindi mkulima anaponunua mbegu inaenda kumuangusha na kumrudisha nyuma kwani mazao huwa duni na yenye kushambuliwa kiurahisi na magonjwa...wakulima wengi ni masikini wanazidi kuwa masikini kutokana na ujanja wa haya makampuni yanayouza mbegu feki...
Naomba tushauriane juu ya wauzaji wa uhakika wa mbegu....
1.je nini mkulima azingatie pindi anunuapo mbegu...
2.je ni kampuni zipi zenye kuuza mbegu zenye ubora wa hali ya juu?
3.nini mkulima afanye pindi anapouziwa mbegu ambayo haijakizi vigezo¿
4.ni dawa zipi mkulima atumie kabla na baada ya kulima...kutibu ardhi na kuua wadudu hatari wa mazao