Ilunda malimi
New Member
- May 27, 2024
- 1
- 0
Tunafahamu kuwa kilimo ndiyo sekta kubwa hapa nchini Tanzania ambayo imeajiri watu wengi sana kuliko sekta yoyote nchini hivyo basi ili wananchi wajikwamue kupitia sekta hii muhimu kabisa ni lazima serikali kupitia wizara ya kilimo kama mwezeshaji mkuu na mratibu wa mipango mikakati kuhusu kilimo ni lazima ifanye mambo yafuatayo;
(a) Kuwekeza katika kilimo cha umwagiliaji(irrigation schemes).
kutokana na mabadiliko ya hali ya tabia ya nchi miaka ya hivi karibuni kilimo cha kutegemea mvua kimekuwa kikipitia changamoto mbalimbali ikiwemo mvua kuchelewa kunyesha, mvua kunyesha kwa kuruka ruka baadhi ya maeneo hivyo basis serikali kupitia wizara ya kilimo iongeze bajeti katika kilimo cha umwagiliaji kwa kufanya mambo yafuatayo;
1: Kuanzisha mpango mkakati sehemu mbalimbali hasa mikoa yenye ukame mkubwa, nusu jangwa kwa kuchimba mabwawa na visima. Mpango huu ufanyike angalau kila kijiji ambapo yatavunwa Maji wakati wa masika, mvua kubwa ili baadae kuendelea na kilimo muda wa mvua chache ambapo pia utaratibu huu unaweza kufanywa na wakulima kipindi chote cha mwaka mfano wananchi wakulima wa kilimo cha mbogamboga,kilimo cha matunda, kilimo cha mahindi, kilimo cha mpunga, kilimo cha maharagwe, alizeti na karanga ili kufikia uchumi mkubwa wa kilimo na wenye tija ili kufanya wananchi wajikwamue kiuchumi. Serikali pia itoe Pesa kupitia wizara ya kilimo ili kujenga haya mabwawa kila kijiji na miundombinu wezeshi itakayo wafanya wakulima kujishughulisha na kilimo mda wote, mabwawa na visima yanaweza kujengwa kisasa zaidi ili kuruhusu matumizi ya mda wote
2: Serikali kupitia wizara ya kilimo kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa wakulima wadogowadogo kwa wakubwa. Mikopo hii itawawezesha wakulima kununua vifaa vya kilimo mfano matrekita,jenereta za kusukuma Maji kutoka kwenye mabwawa na visima, hivi vifaa vinaweza pia kutolewa kwa makundi au vikundi vya watu vilivyojisajili ili kuwa Fanya walime kisasa zaidi lakini pia viwatilifu vya kuzuia magonjwa ya mimea shambani ili kuwafanya wazalishe mazao yenye ubora na kuleta ushindani katika soko la ndani na soko la nje ya nchi
3: Serikali iwawezeshe wakulima wa kilimo cha umwagiliaji kutafta soko la nje ya nchi. Ili mazao yanayapatikana kupitia umwagiliaji yaweze kuleta ushindani zaidi na kuitangaza nchi nje ya mikapa yake na kuongeza kiwango na ubora wa uzalishaji katika kilimo husika mfano kilimo cha maboga na matunda kifanyike katika kiwango cha juu ili mazao yake yapate soko nje ya nchi ambapo makampuni mbalimbali na watu binafsi wavutiwe kuja kununua na kuwekeza nchini vilevile wakulima wapate kujikwamua kiuchumi na kuboresha maisha yao pamoja na serikali kujipatia kodi kupitia pesa za kigeni
4: Serikali ibuni mazao ya kimkakati kulingana na sehemu husika. Serikali ipendekeze mazao yenye tija kwa wakulima kulingana na maeneo husika haya mazao yapewe kipaumbele ili kutengeneze uchumi wa kilimo mkubwa katika taifa mfano mkoa wa Singida na Dodoma kilimo cha alizeti na ufuta, mkoa wa mbeya na Morogoro kilimo cha mpunga na matunda mbalimbali kwa sababu ni maeneo yanayoruhusu kilimo hiki kuanzia hali ya hewa na rutuba ya eneo husika basi serikali iwezeshe wakulima sehemu husika kwa kutoa sapoti ya mikopo yenye riba nafuu ili iwasaidie katika kuendesha kuanzia hatua ya kupanda, kupalilia, kuweka dawa na kuvuna na pia utafutaji wa soko la nje na ndani serikali iruhusu makampuni mbalimbali kuja kununua mazao ya kilimo wakiwatoza kodi rafiki ili wakulima wakubwa na wadogowadogo waweze kujipatia kipato kizuri kiuchumi na mwisho kabisa tupate uchumi mkubwa wa kilimo
5: Utoaji wa ruzuku pembejeo za kilimo. Moja ya kilio cha wakulima walio wengi hapa Tanzania ni mabadiliko ya bei za pembejeo za kilimo kila mwaka kama vile mbolea,mbegu na viwatilifu hivyo basi itoe ruzuka kwenye pembejeo za kilimo zitakazo leta ahueni kwa wakulima hasa wakulima wadogowadogo ili kila mkulima aweze kulima na kuzalisha mazao yenye ubora na ushindani katika masoko yote ya nje na ya ndani
6: Elimu kuhusu kilimo cha umwagiliaji. Serikali kupitia wizara ya kilimo iweke mpango mkakati wa kutoa elimu nzuri kupitia maafisa kilimo wa serikali na wataalamu mbalimbali wa kilimo kutoka sekta binafsi elimu hii itolewe moja kwa moja kwa wakulima kuanzia ngazi ya kitongoji ili kila mkulima awe na maarifa ya kutosha kuhusu anacho kilima na aweze kuzalisha mazao bora na ili elimu hii iwafikie wakulima vizuri Serikali iajiri maafisa kilimo wa kutosha ambao watatoa elimu kupitia semina mbalimbali za kilimo kwa ngazi ya vikundi vya wakulima na makampuni, kufanya hivi kutaleta ongezeko la ajira kwa vijana nchini na kupunguza wimbi la vijana wasiokuwa na ajira
(b) Kuweka Sera nzuri kwenye sekta ya kilimo. Serikali lazima iweke Sera nzuri zitakazo wavutia watu kuwekeza katika kilimo kama vile kuweka kodi rafiki kwa wafanya biashara wa mazao ya kilimo na makampuni mbalimbali yanayokuja kuwekeza kwenye sekta hii ya kilimo na kununua mazao ya chakula na biashara Sera hizi ziambatane na kuweka sheria nzuri kwa wawekezaji wote wa nje na wa ndani zitakawapa faida pindi wanapowekeza mbali na hili serikali pia ifanye mambo yafuatayo
1: Kuboresha Taasisi zinazo jihusisha na mambo ya utafiti wa kilimo cha kisasa. Serikali kupitia wizara ya kilimo iweke bajeti ya kukidhi kwa ajili ya tafiti mbalimbali za kilimo lakini pia iweke sheria zitakazowesha Taasisi zisizo za kiserikali kuwa huru kuutendaji zinapofanya tafiti mbalimbali za kilimo kama vile tafiti za magonjwa ya mimea, mazao pamoja na mbolea
2: Kukuza sayansi na teknolojia katika kilimo. Ili tupate uchumi mzuri na mkubwa katika kilimo serikali itoe mchango mkubwa wa kifedha kuhakikisha teknologia katika kilimo inapiga hatua ili kuzalisha mazao ya kilimo yenye ubora wa hali ya juu mfano teknolojia ya kusindika mazao kama vile matunda ili kuuza katika mitindo mbalimbali itakayofanya kujikwamua kiuchumi kuanzia kwenye ngazi ya mkulima mmoja mmoja mpaka ngazi ya taifa pia kuwepo na uvumbuzi au ununuzi wa vifaa mbalimbali vya kilimo mfano vifaa vya kulimia, kupalilia, kunyunyizia dawa na vifaa vya kuvunia kama vile ndege ndogo zitakazo tumika kunyunyizia dawa kwenye mashamba makubwa ili kuleta manufaa makubwa kwa wakulima na taifa pia mitambo mbalimbali ya kumwagilia Maji kwa njia ya matone kwa kilimo hasa cha matunda na mbogamboga, mashine za kuvunia kwenye mashamba makubwa mfano mashamba ya mpunga na mahindi