Wakufunzi wengi wa chuo sio waalimu.

Kimbori

JF-Expert Member
Feb 21, 2012
5,458
3,206
Kwa uzoefu nilionao nimegundua ya kwamba wakufunzi wengi wa vyuo hapa Tanzania sio hawajawahi kusomea fani ya ualimu. Kibaya zaidi wanawafundsha wanafunzi kuwa waalimu bora.
Kwa mfano, mchumi ambaye hakuwahi kusoma kozi za elimu katika shajada anaandaa waalimu. Je huoni hilo ni tatizo?
 
Kafanye utafiti acha longolongo hapa.......eti uzoefu ulionao.......!!!!!!!!!!!

Are you telling us to bank on your experience???? Personal experience without data??????

Well tell us a bit of the so called ''uzoefu wako'' halafu tuanze kufanya mjadala hapa
 
Kuna vyanzo vingi sana vya maarifa ikiwamo tafiti. Pale ambapo ni nigumu tafiti kufanyika "observation" inafanyika na hivyo kutoa majibu. Nashindwa kukuelewa kwa nini unapaniki, je ikiwa kama waalimu wengi walio SUT, SUA, UDOM n.k walisoma kozi zisizo za ualimu na wanafundisha nisisema? USIWE KAMA WALE WATU AMBAO WAKISHINDWA KUTOA HOJA WANAKIMBILIA MAHAKAMANI NA KUWAZUIA WATU WASIJADILI KWA KUSEMA "TUSIJADILI HILO SUALA KWA KUWA LIPO MAHAKAMANI....
 
ni kweli kabisa, achana na huyo mlopokaji OLESAIDIMU aliyeshindwa kuutumia mtandao, kuna siku hili swala tulilijadili sana na wenzangu chanzo cha mjadala ilikuwa ni .. kwanini baadhi ya maprofesa hawana qualities za kufundisha au wanashindwa kudeliver kwa mwanfunzi ukilinganisha na profiles zao
 
Dah ndugu ilo suala lako ni zuri ila kama umu ndani kuna wahadhir, na washika dau wa elimu watatoa msaada tu ndugu!
 
Nahisi ni moja ya sababu za kufanya elimu na wahitimu wa vyuo kuwa na ufahamu mdogo.
Kwa mfano, mtu aliyesomea sheria moja mpaka udhamiri (masters) kisha kuajiriwa kama mhadhiri, atakuwa anajua sheria lakini atakuwa na uwezo mdogo wa kumudu mbinu za ufundishaji kwa kuwa hana misingi ya ualimu. Hivyo wanatumia mhadhara (lecture), mbinu ambayo haimfanyi mtu kuweza kufanyia kazi kila anachofundishwa.
 
handboy - je na wewe ni miongoni wa wale watumwa wa machapisho ya watu? Hizi mbinu ndio misingi ya hizo data unazotaka. Kama unaweza ichukue kama changamoto, ukafanyie tafiti, kisha utuletee data.
Ila naamini mtizamo wangu ni sahihi.
 
Nadhani kuna ukweli kwenye hoja yako. Wahadhiri wengi hawana vyeti vya ualimu. Ila kwa uelewa wangu kunakuwa na course/seminars/training ya kuwawezesha kutoa elimu kulingana na mahitaji na level ya chuo kikuu. Kwamba mhadhiri anashindwa ku deliver inaweza kuwa inasababishwa na mambo mengine kama kipaji na mengine. Kuna waalimu wanashindwa kabisa kufundisha japo wana vyeti hivyo na uwezo wanao.

Mwanafunzi wa chuo anapaswa awe na juhudi binafsi zaidi, anachofanya mhadhiri ni kidogo sana ukilinganisha na anachopaswa kutafuta mwanafunzi. Nadhani tatizo kubwa tulilo nalo sasa ni wanafunzi kutopenda kusoma. Wanataka notes za mhadhir; library vitabu vina vumbi.
 
Hoja nzuri na yamoto kweli kweli.....! Ukipata mkufunzi wa chuo ambaye amesomea ualimu utafaidi vilivyo!!!
Na aliyepitia kozi za ualimu atasikitika pale mwanafunzi wake atakapofeli wakati wasiopitia kozi za ualimu hufurahi kuona wanafunzi wengi wamefeli ...maarufu kama KUWASHIKA
 
mhadhiri na mwalimu ni vitu viwili tofauti.....kufanya hadhara sio mpaka uwe mwalimu bali ni uelewa wako ndo utakufanya udeliver kitu kizuri
 
Kwa uzoefu nilionao nimegundua ya kwamba wakufunzi wengi wa vyuo hapa Tanzania sio hawajawahi kusomea fani ya ualimu. Kibaya zaidi wanawafundsha wanafunzi kuwa waalimu bora.
Kwa mfano, mchumi ambaye hakuwahi kusoma kozi za elimu katika shajada anaandaa waalimu. Je huoni hilo ni tatizo?

Kutoa mhadhara si sawa na kufundisha, ni vitu viwili tofauti.
 
We kijana dhaifu tofautisha mhadhiri na mkufunzi kwanza.Then nikufahamishe wahadhiri huwa hawafundishi hivyo usiwalaumu kazi yao ni moja nikukutwanga mhadhara alafu ukasome reference library.Mambo ya teaching methodology,saikologia na falsafa huko huko education sisi tunakupiga uchumi theories and practice na tunakupima through lectures,several quizes and assignments sawa mwalimu
 
ni kweli kabisa, achana na huyo mlopokaji OLESAIDIMU aliyeshindwa kuutumia mtandao, kuna siku hili swala tulilijadili sana na wenzangu chanzo cha mjadala ilikuwa ni .. kwanini baadhi ya maprofesa hawana qualities za kufundisha au wanashindwa kudeliver kwa mwanfunzi ukilinganisha na profiles zao

ualimu na uhadhili ni taaluma mbili tofauti. atakaye weza kuzifanya taaluma hizi kuwa ni moja na ni sawa aweza kujiongezea nafasi ya kushinda tuzo ya nobel.
 
Kwa uzoefu nilionao nimegundua ya kwamba wakufunzi wengi wa vyuo hapa Tanzania sio hawajawahi kusomea fani ya ualimu. Kibaya zaidi wanawafundsha wanafunzi kuwa waalimu bora.
Kwa mfano, mchumi ambaye hakuwahi kusoma kozi za elimu katika shajada anaandaa waalimu. Je huoni hilo ni tatizo?
ndugu yangu unatatizo la kuelewa tofauti kati ya hizo taaluma mbili, mkufunzi na mwalimu. hizo ni taaluma zisizofanana, ni duniani kote. lakini hii haikuzuuii wewe kuleta badiliko, endeleza mawazo yako , yakifanikiwa utajichukulia umaarufu mkuu duniani kwa mchango wako mkuu
 
ni kweli kabisa, achana na huyo mlopokaji OLESAIDIMU aliyeshindwa kuutumia mtandao, kuna siku hili swala tulilijadili sana na wenzangu chanzo cha mjadala ilikuwa ni .. kwanini baadhi ya maprofesa hawana qualities za kufundisha au wanashindwa kudeliver kwa mwanfunzi ukilinganisha na profiles zao

Kumbe na wewe ni mtu mzima hovyo na huna lugha ya kistaarabu......eti mi mropokaji!!!!!!!!

M sorry to mention but you look to be humble and poor thinker; the only good thing with you is that your still loyal to your narrow scope.....either way you are not totally useless.....If need be I can quote you as a bad example.......

1. Unajua induction course on teaching methodology?????
2. Unajua degree ya ngapi hutumika kama kigezo cha kuajiriwa in this cadre??????
2. Alokwambia quality ya mtu kufundisha huendana na hii mada ni nani???
3. Unajua hata kwenye vyuo vya ualimu kuna mwanafunzi bora, wa wastani na just a graduate na wote hawa ni walimu by profession?????
4. Check the GPA's at DUCE and make your own deductions in relation to quality and ability to deliver

Add; Check the differences between a teacher, tutor and lecturer...................leave aside the professorial achievement
 
Kuna vyanzo vingi sana vya maarifa ikiwamo tafiti. Pale ambapo ni nigumu tafiti kufanyika "observation" inafanyika na hivyo kutoa majibu. Nashindwa kukuelewa kwa nini unapaniki, je ikiwa kama waalimu wengi walio SUT, SUA, UDOM n.k walisoma kozi zisizo za ualimu na wanafundisha nisisema? USIWE KAMA WALE WATU AMBAO WAKISHINDWA KUTOA HOJA WANAKIMBILIA MAHAKAMANI NA KUWAZUIA WATU WASIJADILI KWA KUSEMA "TUSIJADILI HILO SUALA KWA KUWA LIPO MAHAKAMANI....

Kwanza kajifunze tofauti ya Mwalimu, Mkufunzi, na Muhadhiri halafu ndio upime kama mada yako ina mantiki na inahitaji kujadiliwa.

Kama njia za kufundisha kwa madaraja yote hayo zingekuwa sawa kuanzia mwanafunzi wa chekechea hadi chuo kikuu basi inawezekana ukawa na hoja.
 
handboy - je na wewe ni miongoni wa wale watumwa wa machapisho ya watu? Hizi mbinu ndio misingi ya hizo data unazotaka. Kama unaweza ichukue kama changamoto, ukafanyie tafiti, kisha utuletee data.
Ila naamini mtizamo wangu ni sahihi.

You are still in a metaphysical-cum- theological era.............. it might be a a good waste of time to argue with a brain in a skull that is still in the a fore mentioned state of mind...............''naamini mtizamo''.........haya bana karibu huku post industrial
 
Back
Top Bottom