Wakristo Wenzangu Hivi Kumchezea Mungu Ndombolo, Sebene Na Kwaito Alituagiza?

Msema kweli no mpenzi wa mungu hakika hii ni fedheha kubwa , hata kama mungu wetu ni wa furaha lakini kwa viwango vinavyostahili sio kucheza miziki ya ufuska.
 
Bro post yako Ina maudhui ya chuki dhidi ya walokole! Jinsi ulivyoandika, maneno uliyotumia, na maudhui kiujumla ni kandamizi na ya kudhalilisha makanisa ya kipentekoste, na nikwambie tu Kama imefikia hatua wakristo tunadhalilishana namna hii na kufikia hatua ya kuwaita waisilamu Kuja kujadili mambo yetu wakristo basi ni wazi kabisa hukusudii kujenga Bali kuharibu na kuleta migawanyiko baina yetu!
Ni Sawa kama umeona mapufungu basi Kuna namna nzuri tu ya uandishi wenye malengo ya kujenga.
Sio kwa staili hii!
Meseji senti mkuu, haina haja ya kujadili muandiko
 
Imeandikwa lkn Kwenye biblia japo kifungu sikijui vizuri
Kwamba mtukuzeni mungu wenu kwa nyimbo na vinubi
Aijaindicate watu wacheze stail gani labda kwa sababu teyali zina majina ndio maana imekua gumzo( kiduku,dombolo na style nyingine
Yakiandikwa sharti yatekelezwe??
 
Allah sw hapendi makelele anapenda aabudiwe kwa unyenyekevu kwani yeye husikia hata tuyawazayo, haina haja ya makelele na miziki
 
Hakuna jipya chini ya jua.
Mzikinulikuwa kwa Mungu na shetani alipofukizwa alikuja nao kwa kiasi kidogo na ndo disko likaamzishwa.

Daudi alimchezea Mungu mpaka nguo zikaanguka,wewe ndombolo umewahi cheza mpaka nguo zikaanguka.
Najua mleta mada ni dhehebu flani la kistaarabu linatoka ulaya ya kati,mnaenda kila kitu kwa mapokeo na hamchezi wala kuimba kitu ambacho si sahihi.
Okay sihukumu ila wasikilize hao waitalia wako.

Soma zaburi yote inasemaje?
 
kati ya nzuzi ulizowahi kuleta, huu umepwaya sana, nafikiri ingekuwa wewe mkristo kweli ungekoti hata vifungu vinavyokata au kuruhusu kucheza, hapa umechemka, rc asili ya uimbaji waujua watokea wapi, wasabato nao wanastaili yao, hata waislam pia wanachezesha vichwa nao wana asili yao urabuni, je sababu sebene ni staili ya aftica ndo haifai?
Kwa hiyo kukata mauno kama huko kwenye kigodoro ni sawa kwenye nyumba ya ibada..? Tatizo hayo makanisa yenu huwa tunayaita uchwara au ya vichochoroni..

Hivi unafahamu nidhamu ya kanisa..?
 
Shalom Nyote!

Leo Jumapili Hii Nipo KIROHO Zaidi Ila Sitaki Ipite Hivi Hivi Bila Kutoa DUKU DUKU Langu Nililonalo Kwa Kipindi Sasa.

Hivi Sisi WAKRISTO Ni Kwamba Siku Hizi Tumepiga MAENDELEO Ya KIROHO YALIYOTUKUKA au Ndiyo TUNAMKASIRISHA Mwenyezi Mungu Tu?

Siku Hizi Ukienda Kanisani Na Labda Tu Ukiondoa Kwa Sisi WAKATOLIKI TULIOTUKUKA Basi Humo Katika Kanisa Hizo Nyimbo Za DINI Ambazo Zitapigwa Hazitakuwa Na Tofauti Sana Na Masebene Ya Ndombolo, Zitutana, Kwasakwasa, Kibindankoi Na Ekotitee.

Jamani Hivi:

  • Kukatika KIUNO Madhabahuni Ni Halali Kwa Mungu?
  • Waumini Wanacheza Sebene Hadi Wanaelekezeana Makalio Yao Ni Halali Kwa Mungu?
  • Waumini Kucheza Pale Madhabahuni Hadi Wengine WANAJAMBA Na Harufu Sometimes Sisi Tuliokaa Tunaisikia Huku Wakitokwa Na MIJASHO Ni Kupena UPAKO Huko au Kutafutiana Tu NUKSI?
  • Muimbaji au Kwaya Husika Kuvalia Nguo ZILIZOBANA KUNAKOTUKUKA Hadi Unaona Kila Kitu Kilichoumbwa Na Mwenyezi Mungu Huyo Huyo Ni HALALI Kiroho?
Yangu Ni Haya Tu WATUMISHI Wenzangu Wa KIKRISTO Na Naomba ROHO MTAKATIFU AWAONGOZE KATIKA KUNIJIBU MTAKATIFU MWENZENU NILIYETUKUKA. Bwana Yesu ASIFIWE!

Karibuni Na Hata Ndugu Zangu WAISLAMU Nanyi Pia Mnakaribishwa Kuchangia Na Kutoa Pia Maoni Yenu Kwani Naamini Wote TUNAMWOMBA MUNGU Mmoja Ni Hizi Zingine Ni Mbwembwe Zetu Tu SISI Wanadamu.
Ndio Mungu alituagiza, reje pale Daudi alipokata mauno hadi Nguo zikamvuka madhabahuni akimchezea Mungu, na imeandikwa Muimbieni Mungu kwa kinanda na vinubi, una lingine?
 
Hakuna jipya chini ya jua.
Mzikinulikuwa kwa Mungu na shetani alipofukizwa alikuja nao kwa kiasi kidogo na ndo disko likaamzishwa.

Daudi alimchezea Mungu mpaka nguo zikaanguka,wewe ndombolo umewahi cheza mpaka nguo zikaanguka.
Najua mleta mada ni dhehebu flani la kistaarabu linatoka ulaya ya kati,mnaenda kila kitu kwa mapokeo na hamchezi wala kuimba kitu ambacho si sahihi.
Okay sihukumu ila wasikilize hao waitalia wako.

Soma zaburi yote inasemaje?
Wacha kutetea mambo ya kishetani na uhuni kwenye nyumba za ibada.....

Nidhamu ya kanisa ipo wapi...? Mnatakiwa kujitofautisha na Mataifa....kama imefikia hatuoni tofauti kati ya kigodoro na walokole hali mbaya....
Hivi kweli umetoa wapi ujasiri wa kutetea uhuni kama huu.....
 
Otoringongo punguza jazba.
Soma Biblia alafu Mwamini Yesu,ila kama unaomba kupitia mama yake Yesu hutaelewa haya mambo ya U-Ungu
 
Ndio Mungu alituagiza, reje pale Daudi alipokata mauno hadi Nguo zikamvuka madhabahuni akimchezea Mungu, na imeandikwa Muimbieni Mungu kwa kinanda na vinubi, una lingine?
Soma barua ya Paulo kwa kanisa la Korinto uone Paulo alivyokuwa anasisitiza nidhamu ya Kanisa, viongozi ws Kanisa...Mpaka wanawake walikuwa hawaruhusiwa kuacha kichwa wazi...

Sasa nyie walokole wenye laana aliyewaloga ni nani mpaka kucheza vigodoro huko kwenye makanisa yenu.....Unakata mauno kanisani...? Unaakili timamu wewe..? Unalaaana....???

Nyie walokole mna laana....???
 
Otoringongo punguza jazba.
Soma Biblia alafu Mwamini Yesu,ila kama unaomba kupitia mama yake Yesu hutaelewa haya mambo ya U-Ungu
Nisome biblia ili nijue kukata mauono...? Biblia inatupasa kuisoma ili kukata mauno...?

Kukata mauno ndio mambo ya rohoni...???
 
Back
Top Bottom