Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,523
- 24,010
inaonekana team ya TP Mazembe imeacha kundi kubwa la wananchi raia wa Kongo hapa dsm. haijafahamika hasa sababu ni nini. lakini leo ofisini na Mjini sehemu Nyingi wamesikika wananchi wanaoongea kwa Lafudhi ya Kongo. Nimesikia watu hao wengi sana na kwa mshangao mkubwa nimegundua hata Jamaa kama wanne hivi ofisini kumbe nao Ni wakongo kwa namna wanavyoongea kwa madaha na kiswahili chao cha kikongo.
wakati huo huo nimeona watanzania wengine wakikasirishwa na jambo hilo la Raia hao ambao ni ndugu zetu kuongea kwa lafudhi ya Kongo. Jamaa mmoja alimshika shati mwenzie kwa sababu tu alimsikia akisalimia watu waliokaa pembeni yake kwa lafudhi ya Kikongo. Jambo hili lilivuta umati wa watu wengi waliotaka kujua kulikoni mpaka watu wazima hawa wapate kushikana mashati. ndipo jamaa huyu aliyetaka kumpiga mwenzie aliposikika akisema hapendi kumsikia Jumbe akizungumza kwa lafudhi ya Kikongo. watu wengi walijawa na udadisi kuwa sababu gani inamkwaza kiasi hicho....ndugu Hamidu alisema kuwa huyo jamaa Jumbe ni raia wa tanzania tena mswahili kabisa wa kutoka Zanzibar iweje azungumze kama Mkongo na kuvaa Kipapaa....
maeneo mengi mjini dar wamesikika watu wanaoongea kwa lafudhi ya kikongo na kuwa kivutio kikubwa sana. inawezekana watu wa TP Mazembe wengi wamebaki kusheherekea Ushindi wao hapo jana dhidi ya team inayopanda ndege ya Yanga afrikans. wakongo wengi hao walisikika wakisema wao issue kwao si kupanda ndege isipokuwa ni kuchukua point 3 kila wanapoenda. maana kama kupanda ndege basi air hostess wanapanda sana kuliko mtu yeyote mwingine.